#breaknews

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 8 ก.ค. 2024
  • Lori la mizigo lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Burundi, limepata ajali baada ya kupinduka leo Julai 9 saa 2:00 usiku wilayani Kilosa Mkoa wa Morogoro na kisha kuwaka moto, ambapo dereva wa lori hilo anahofiwa kufariki.
    Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, akisema chanzo cha ajali hiyo imehusisha gari dogo lililokuwa linatoka Dodoma kwenda Morogoro baada ya kuyumba na kuligonga lori hilo.
    Dereva wa gari dogo imeelezwa amepelekwa hospitali kwa matibabu.
    Akitoa taarifa ya awali, Shaka amesema chanzo cha ajali hiyo kimetokana na dereva wa gari ndogo kushindwa kuhimili gari lake kwenye kona kisha kugonga mti na baadaye kuparamia lori hilo na kusababisha gari hilo kutumbukia darajani.
    Hata hivyo hadi sasa haijajulikana alipo dereva wa lori hilo ambaye anahofiwa kufariki dunia.

ความคิดเห็น • 8

  • @husseinhemedi9314
    @husseinhemedi9314 19 วันที่ผ่านมา +1

    Mungu atujaalie wenye kufanya kazi ya udereva Insha Allah

  • @lugendotv6359
    @lugendotv6359 18 วันที่ผ่านมา

    Mwenyezi Mungu awarehemu wote waliopoteza maisha

  • @Glorykitosi
    @Glorykitosi 10 วันที่ผ่านมา

    jamani baba davis umeacha wtt wadogo

  • @paulajohn7901
    @paulajohn7901 20 วันที่ผ่านมา

    Ooooh!!

  • @florianhenry7198
    @florianhenry7198 19 วันที่ผ่านมา

    Morogoro waganga wengi wanatoa kafara

  • @issaalfani1030
    @issaalfani1030 20 วันที่ผ่านมา

    Nimekosa chakusema kwa sababu ya masikitiko

  • @mabulajoel1967
    @mabulajoel1967 20 วันที่ผ่านมา

    Wengine husabisha wenzao kutumia kwa kweli!!!😂😂