UJENZI WA BANDARI YA BAGAMOYO / MKURUGENZI TPA AZUNGUMZA MAZITO

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 8 ม.ค. 2024
  • #TPA
    BANDARI ya Dar es Salaam katika kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba 2023 imefanikiwa kufanya huduma zaidi ya malengo yake ambapo imehudumia takribani meli 979 kati ya meli 792 zilizokuwa zimekusudiwa.
    Ameyasema hayo leo Januari 9,2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mbossa wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali katika ofisi za TPA.
    Amesema kuwa katika kipindi hicho bandari imehudumia abiria takribani milioni 1 kati ya 900,000, makasha 990,000 kati ya lengo la kuhudumia makasha 500,000, huku mizigo ikiwa ni tani milioni 17.2 kati ya tani milioni 15.6 zilizokusudiwa.
    Aidha Bw. Mbossa amesema kuwa kutokana na maboresho ya bandari meli hadi 12 zinahudumiwa kwa wakati mmoja, hivyo kupelekea wastani wa meli 100 kuhudumiwa kwa mwezi mmoja, kutoka meli 70 ndani ya mwezi mmoja.

ความคิดเห็น • 1

  • @salimukimwaga-fu8cc
    @salimukimwaga-fu8cc 27 วันที่ผ่านมา

    Kwa nini kuwe na usiri wa mikata a mikubwa ya nchi Kuna undani Gani