Ole Sendeka alipuka bungeni akitaka shingo ya mtu, Venant akichangia; Mwigulu na Mhagama wasimama

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 1 พ.ย. 2023
  • Mbunge wa Simanjiro (CCM) Christopher Ole Sendeka amewataka Mawaziri ambao Wizara na taasisi zilizochini yao zimetajwa katika ubadhirifu, wawajibike wenyewe.
    Ole Sendeka amesema kama hawatawajibika basi bunge liondoke na alichokiita shingo ya yule ambaye wanamamlaka naye kwa alichosema “wanachezea sana.”
    Mbunge huyo ametoa kauli hiyo bunge leo Alhamisi Novemba 2,2023 alipokuwa akichangia kwenye taarifa za Kamati za bunge kuhusu ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
    Mkongwe huyo ametoa kauli hiyo alipoomba kutoa taarifa wakati mbunge wa Igalula Venant Protas alipokuwa akichangia.
    “Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kumpa taarifa mzungumzaji ambaye anachangia vizuri sana, napendekeza kuwa, mawaziri wote ambao taasisi zilizochini yao zimetajwa wawajibike haraka lakini wasipowajibika twendeni na shingo ya yule ambaye tuna mamlaka naye, wasituchezee,” amesema Olesendeka.
    Katika mchango wake Protas amemuomba Naibu Waziri Mkuu kwenda na kalandinga (gari la polisi) akabebe watumishi wote wa kampuni ya Tan Oil isipokuwa mhudumu pekee ndiye anastahili kubaki.
    Protas kwenye mchango wake amesema kuna mashaka hata katika ofisi ya mwanasheria Mkuu wa Serikali ambayo nayo amepombe ifanyiwe ukaguzi maalumu.
    Kwa mujibu wa mbunge huyo, kwenye kesi ya Escrow kampuni ya IPTL ilichukua mabilioni ya fedha lakini Mwanasheria alisimama hadharani na kusema kuwa fedha hizo hazikuwa za Serikali lakini inashangaza muda mfupi imekuja taarifa kuwa Serikali inadaiwa.

ความคิดเห็น • 65

  • @tusajigwe7491
    @tusajigwe7491 8 หลายเดือนก่อน +1

    Best speech mbunge, Mungu akulinde

  • @user-uy2dk2yv2c
    @user-uy2dk2yv2c 8 หลายเดือนก่อน +3

    Jizi kubwa et Tàarifa

  • @user-bd1zr4vn1b
    @user-bd1zr4vn1b 8 หลายเดือนก่อน +2

    Kazi kumfungia mwambukusi

  • @juliusmagunila6308
    @juliusmagunila6308 8 หลายเดือนก่อน +2

    Halafu mwigulu angetuacha kabisa tukimkamata kwenye kumi na nane we ngoja

  • @emmanueljoseph3812
    @emmanueljoseph3812 8 หลายเดือนก่อน +1

    Hvi kweli kwastaili hii Nchi hii kwa uongozi wa CCM hatutoboi na hata hivyo Bunge hili haliwezi tena kuishugilikia Serikali hata KIDOGO! Watanzania tujipange tu kupata Bunge lingine!

  • @mlumez
    @mlumez 8 หลายเดือนก่อน +1

    Kwa bunge hili, wakichukua hatua nmekaa palee👉👉

  • @musayohana3274
    @musayohana3274 8 หลายเดือนก่อน

    Ongera sana kiongozi olesendeka

  • @user-hb1iw9uj3x
    @user-hb1iw9uj3x 8 หลายเดือนก่อน +2

    😂😂mzee wa tozo,trab na trat, kodi ya stoo. 😅 😅 mwigulu mwizi wa kutupa.***Mwigulu mwizi afukuzwe kazi huyooo....kazoea kuhamishwa hamishwa.

  • @chademaelfhasmolell
    @chademaelfhasmolell 8 หลายเดือนก่อน +2

    Apo funika kikombe mwanaharamu apite wapigaji ni ccm haohao

  • @partysekemi5
    @partysekemi5 8 หลายเดือนก่อน +1

    Mbona wabunge wote kwenye ripoti ya CAG ya mwaka huu wote wamenyooka uchaguzi imekaribia e tunawaona vizuri sasa kila mwaka watanzania wenzangu kamati ya CAG inaleta taarifa za wizi na hakuna hatua kana kwamba mnafanya chombo hicho cha CAG na takukuru ndio zinatoa ripoti za uongo na kama ni wao sio waaminifu tuanze na hao!!!

  • @user-rs4vz2vt9z
    @user-rs4vz2vt9z 8 หลายเดือนก่อน +1

    Wacha mungu aitwe mungu wapinzani hawamo.

  • @aud548
    @aud548 8 หลายเดือนก่อน +1

    Mliye na mamlaka naye ....😂😂😂😂 yani mumpige chini Majaliwa

  • @williammwamalanga1065
    @williammwamalanga1065 8 หลายเดือนก่อน +1

    Mwigulu mwigulu mungu anakuona

  • @patrickngumbi2766
    @patrickngumbi2766 8 หลายเดือนก่อน +1

    Mwigulu kumbuka hapo hukujiweka, kwa nn mnadharau hivi au mnafikiri hatuon wala kusikia?!!! Au mnahisi hatuwezi chukua hatua za ghafla endeleeni tu

  • @ChristerShao
    @ChristerShao 8 หลายเดือนก่อน +3

    Akina Tundu Lisu wakisema juu ya mikata mibovu mnawatukana mlikuwa wapi.

  • @benedictchagula8739
    @benedictchagula8739 8 หลายเดือนก่อน +1

    Safi sana! Wote wangekuwa na mtazamo kama huyu mbunge tungekuwa mbali

  • @williammwamalanga1065
    @williammwamalanga1065 8 หลายเดือนก่อน +1

    Asante sana mh mbunge wa igalula

  • @marymchina6557
    @marymchina6557 8 หลายเดือนก่อน +1

    Kwani huyu Mwigulu nyuma yake kunanani? Subirini 2025 mtatujua vizuri

  • @mayrfrimi4759
    @mayrfrimi4759 8 หลายเดือนก่อน +1

    Huyu mwigur ajinyamauie tu maana kwenye wiz wa serekalini ni Nr 1, alafu hanaga huruma kabisa kwenye swala hilo.

  • @francismwantolwa2329
    @francismwantolwa2329 8 หลายเดือนก่อน +1

    Wezi wakubwa hawa

  • @HusseinseifSachirama-tn2fj
    @HusseinseifSachirama-tn2fj 8 หลายเดือนก่อน +2

    Mwigulu yani simpendi

  • @williammwamalanga1065
    @williammwamalanga1065 8 หลายเดือนก่อน

    Hongera ole sendeka

  • @zebedayokatamaduni9676
    @zebedayokatamaduni9676 8 หลายเดือนก่อน

    Ole Sendeka asante

  • @patrickngumbi2766
    @patrickngumbi2766 8 หลายเดือนก่อน +1

    Mbunge anaongelea wizi , huyu mama anataka kutufunika na maendeleo ya mchongo bado mnafikiri kuna watanazania wa hivyo kweli?!!!

  • @frankpeter4178
    @frankpeter4178 8 หลายเดือนก่อน +2

    ....among the worst Govt ever this country got, never even foreseen

  • @bahatiangle4424
    @bahatiangle4424 2 หลายเดือนก่อน

    Ongea baba

  • @user-bx2hd9ek4b
    @user-bx2hd9ek4b 7 หลายเดือนก่อน

    Serikali wenyewe ndio wezi wetu sasa

  • @kristiankitali5505
    @kristiankitali5505 8 หลายเดือนก่อน +1

    Huyu Mwigulu huyu sijui

  • @mudhihirugara8845
    @mudhihirugara8845 8 หลายเดือนก่อน

    Hamnalolote kilasiku hayohayo mbona enzi zamagufuli yalikoma raiya hatuna Imani nawabunge ninyi ibenitu kulenitu sisi hatuna chakufanya

  • @user-bg2zt8xw3d
    @user-bg2zt8xw3d 8 หลายเดือนก่อน

    Ni vizuri tukienda hvi

  • @alexkatama4341
    @alexkatama4341 8 หลายเดือนก่อน

    Kuchekacheka kwenye vitu serious ni ujinga

  • @IsraelMgilitwe
    @IsraelMgilitwe 8 หลายเดือนก่อน +1

    Sisi wananchi tunapambana kutafuta msosi kwa jasho ninyi mpo kivulini tusaidieni

  • @amizatibakari7385
    @amizatibakari7385 8 หลายเดือนก่อน

    Hatujawahi ona hatua zote zinachukuliwa juu ya ufisadi mna kazi yakupia kelele tu Kila siku kumeibiwa matilion ya hela wakati huku mtaan mtu Hana hata buku ya kula hanjui ni dhambi kubwa lkn mjue Kuna kufa na hukumu ipo Kodi za masikin Kila kukicha zinaibiwa watu wenye vyeo wale Bata na familia zao hii ni haki

  • @user-rh4qo6on4g
    @user-rh4qo6on4g 7 หลายเดือนก่อน

    Sekali ya ahamu ya tano inanyanyasa masikini kama ngombe zinauzwa efu kweli ni halalo tungalie hila

  • @user-bd1zr4vn1b
    @user-bd1zr4vn1b 8 หลายเดือนก่อน

    Pesa kapeleka fountain gates

  • @user-rh4qo6on4g
    @user-rh4qo6on4g 7 หลายเดือนก่อน

    Mali ya masikin tu ndiyò ya selikali lakin majiri niyakao

  • @joelramadhan6062
    @joelramadhan6062 8 หลายเดือนก่อน

    Mambo ya system nchi hii ya wandwale😂😂😂😂

  • @francismigongwa4146
    @francismigongwa4146 8 หลายเดือนก่อน

    Kazi iendelee

    • @robertphilip385
      @robertphilip385 8 หลายเดือนก่อน

      Weusidanganywe na Hawa kuku niporojotu

  • @epiphanmsolina5321
    @epiphanmsolina5321 8 หลายเดือนก่อน

    CCM wote ni wezi watupu

  • @m.m.tvmbebamaono
    @m.m.tvmbebamaono 8 หลายเดือนก่อน +1

    Mwigulu katubu umetuibia sana

  • @emmanueljoseph3812
    @emmanueljoseph3812 8 หลายเดือนก่อน

    Huyo Jennifer anaongea nini?

  • @ChristerShao
    @ChristerShao 8 หลายเดือนก่อน +1

    Mwigulu muogope mungu.

    • @emmanueljoseph3812
      @emmanueljoseph3812 8 หลายเดือนก่อน

      Tuanze na mwigulu!

    • @azizakiswili9063
      @azizakiswili9063 8 หลายเดือนก่อน

      Yaani utafikiri nchi hii ni mali yake😢😢

  • @HappinessminjaHappysiami-xx4df
    @HappinessminjaHappysiami-xx4df 8 หลายเดือนก่อน

    Tunaomba mheshimiwa sendeka uweze kuongelea swala la Barbara ya simanjiro ni mbaya mno

  • @KashindyeGidion
    @KashindyeGidion 3 หลายเดือนก่อน

    Tudamani

  • @IsraelMgilitwe
    @IsraelMgilitwe 8 หลายเดือนก่อน

    Tunaomba wabunge mtusaidie wananch

  • @robertphilip385
    @robertphilip385 8 หลายเดือนก่อน

    Huyu sendeka nae hajui chochote mlarusha wa simanjiro

  • @josephmkinga9509
    @josephmkinga9509 8 หลายเดือนก่อน

    Bunge la chama wanachoongea hata hakina utekelezaji hayo maneno ya hapo

  • @geraldadolf4928
    @geraldadolf4928 8 หลายเดือนก่อน

    Uyu jamaa kiboko

  • @user-cm1jo7jz5q
    @user-cm1jo7jz5q 6 หลายเดือนก่อน

    Paulo siria

  • @user-gg7ig1qc5o
    @user-gg7ig1qc5o 8 หลายเดือนก่อน

    Wewe mwigulu ni mpumbavu tu mwehu,watanzania wanaumia halafu unaleta ushuzi wako we mwehu

  • @m.m.tvmbebamaono
    @m.m.tvmbebamaono 8 หลายเดือนก่อน

    We mama umechanjwa chanjo ya korona hakuna kizuri

  • @sebastiansalamba313
    @sebastiansalamba313 8 หลายเดือนก่อน

    Sasa mmeanza kazi

    • @robertphilip385
      @robertphilip385 8 หลายเดือนก่อน

      Hamna kazi yeyote hawaniwapigaporojo hamna bunge hapa kazi Yao ndiyoooooo

  • @tumainimwaifunga3884
    @tumainimwaifunga3884 8 หลายเดือนก่อน

    ,🤣🤣🤣🤣

  • @emmanueljoseph3812
    @emmanueljoseph3812 8 หลายเดือนก่อน +1

    Tuwapeni Chadema hii Nchi

  • @m.m.tvmbebamaono
    @m.m.tvmbebamaono 8 หลายเดือนก่อน

    Mwiguru nchemba wewe chanjo ya korona inakusumbua mwizi wewe

  • @raymondkafyulilo6636
    @raymondkafyulilo6636 8 หลายเดือนก่อน

    Wote mliokaa hapo ni wezi tu. Mwigulu ndiyo mwizi mkubwa huyo. Mbunge Venant yupo sahihi

  • @user-sf3ou8uu8q
    @user-sf3ou8uu8q 8 หลายเดือนก่อน

    Mnaheshimika kwa wizi tokeni huko ndio maana mnatia Aibu sana

  • @mikemutabuzi3665
    @mikemutabuzi3665 8 หลายเดือนก่อน

    Ninaamini muda si mrefu bandari mtajirarua nyie wenyewe, 😂😂😂😂😂😂😂😂😂