TRA: NJOONI TUWAPE MISAMAHA YA KODI, BIDHAA NYINGI ZA KILIMO ZIMEFUTIWA KODI IKIWEMO MATREKTA

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 16 ก.ย. 2024
  • Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamesema ni muhimu kwa kila Mtanzania kuwa na namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN NUMBER) ambayo inapatikana bure.
    Afisa Msimamizi Mwandamizi wa TRA Philip Eliamini amesema kuwa namba hizo zinapatikana bure ikiwemo ushauri kwa walipa kodi katika ofisi zozote za Mamlaka hiyo.
    Eliamini amewataka Watanzania wote waliofikisha umri wa kuanzia miaka 18 kwenda kuhakikisha wanakuwa na namna hizo lakini kwa watakaotembelea kwenye mabanda ya maonyesho ya Wakulima ikiwemo Nzuguni wakifika kwenye banda lao watapatika ushauri na kupewa utambulisho huo.
    "Lakini kingine tunatoa elimu ya misamaha ya kodi, watu waje tuwapatie na kuwaambia kipi kinafaa kuwa msamaha na kipi hakistahili kwenye msamaha ili kuondokana na usumbufu wa baadae," amesema Eliamini.
    Kwa mujibu wa kiongozi huyo, baadhi ya watu wanashindwa kutambua ni bidhaa zipi zimetolewa misamaha na akazitaja baadhii ya bidaa ikiwemo za kilimo.

ความคิดเห็น •