Sallam Afichua Walichokifanya WCB Baada Kufungiwa Na Media Zote Kubwa | SALAMA NA SALLAM SK PT 2
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 10 ก.พ. 2025
- #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Sallam Sharaff ni lejendari, na hilo liko wazi kwa anayetaka na asiyetaka, kwa umuhimu wake kwenye maisha ya msanii nambari moja kwa sasa ni kama nywele, usipomkuta kichwani basi hata kwapani hatokosekana. Na kwa utashi wangu nadhani kama wana Bongo Flava au wasanii ambao ‘wako tayari kuwekeza’ basi wangemkimbilia kwa kasi ya 4G ilimradi wapate mawazo tu ya jinsi gani wanaweza kufanya ‘meli’ yao ifike na pale panapotokea mrama wajue wimbi gani la kuliepuka na wimbi gani ndo walipandie kwa juu.
Sallam si muongo na hili ninalijua kwasababu ni rafiki yangu, atakavyokuambia ndivyo lilivyo, Sallam anapenda pesa na hilo liko wazi na wala hajifichi nalo ila kubwa zaidi Sallam anapenda MAENDELEO. Ukitaka msielewane naye milele na milele basi onyesha nia au muonyeshe moja kwa moja kama unataka ’kumharibia’ mkate wake. Hakika hatokuacha salama. Atahakikisha unaenda na maji kwasababu mkate wake ndo maisha yake. Tofauti yake na wengi wetu ni kwamba wengi wetu tukijua mtu anataka kukuharibia basi na wewe utajificha au utamuepuka au utamchukia tu, Sallam yeye atakuonyesha waziwazi kama HAKUPENDI.
Muziki anaufahamu vizuri tu na mengine anayang’amua as we go kama binadamu wa kawaida, mapenzi yake kwa mziki huu na kwa kupenda anachokifanya ndo kunamfanya awe THE BEST MANAGER. Maisha na mipango na maendeleo ya msanii nambari moja kwa sasa yalianza kubadilika sana mara baada ya Sallam kuingia kazini, na ilibidi aanze kama International Manager maana kwa upande wa ndani tayari Babu Tale na Said Fella walikua washapatawala. Haikua kesi kwake, ambacho alikifanya ni kuhakikisha Diamond anapata collabo na show nyingi za nje ambazo yeye alikua anaenda naye. Wakati akiwa wanapokua alitumia nafasi hiyo kutengeneza network nyengine. Mipango yake na uwajibikaji na jinsi vitu vilivyokua vinasogea vilimfanya Platnumz ampende zaidi, amshirikishe kwenye mambo mengi zaidi ambayo matunda na malipo yake ndo haya ambayo wanakula leo na kesho na keshokutwa ilhali mimi na wewe tunashuhudia historia inavyozidi kuandikwa.
Kwa Said Fella kupata udiwani nako pia kulimfanya Sallam apate majukumu zaidi ya hata ya ndani sasa maana kipindi kile cha Hayati JPM kazi ilikua inabidi ifanyike na Sheikh Said alipigiwa kura na watu, so mara nyingi ilikua inabidi afanye kazi za kutumikia wananchi wake, na huku nyuma Sallam akawa anaezeka banda lake la kuishi kwenye ufalme wa Diamond Platnumz.
Nakumbuka mwaka 2018, London Town, Diamond alimaliza show zake na Sallam akabaki nyuma, kilichowapeleka kule ilikua ni show ambayo yeye Sallam, my cousin Dulla Meru na moja ya mapromota hodari kutoka Nigeria ambaye anaishi London Ndugu Smed waliiandaa, ilienda poa na naamini ile ilifungua milango mingi sana. Alibaki nyuma kuhakikisha mambi yote yanakwisha freshi na pia kutengeneza network nyengine kwa matumizi ya baadae. Alibaki nyuma na mimi. Tuli enjoy, tuli jifunza na pia yeye aliweza kuweka MIZIZI yake vizuri ili mbuyu huu tunao uona leo usimame.
Mawe mengi mno kapigwa. Maneno mengi sana yamesemwa juu yake, kama binadamu hawezi kuwa amekamilika au kamaliza, ila jitihada zake na kazi ambayo anaifanya inabaki inamzungumza kwa niaba yake. Kama ambavyo yeye anasema, kwanza yeye ni MFANYA BIASHARA, mengine yanakuja baada ya hapo. Diamond anamlipa Sallam kwa asilimia kila mara anapoleta BIASHARA kwenye MEZA YAKE. Faida ni ya WOTE. Sio mmoja ananenepa na mwengine anakonda kama ilivyo kwenye mahusiano mengi ya biashara hapa nyumbani na pengine Afrika na duniani kwa ujumla.
Ukiniuliza mimi nitakuambia, hapa kuna mengi ya kujifunza.
Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahs...
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm
ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru
GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
Audiomack Link bit.ly/YahSton...
TH-cam Link bit.ly/TH-camS...
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz
Sipendi marafiki Ila nahitaji wafanya biashara wenzangu that's big point Salam salute.
Jamaaa anajua kuongea asee wasanii muweke heshima jamaa atawafikisha mbali Big Up SK
Duh yani huna marafiki wala huitaji marafiki kweli we mwamba😁😆
SALLAM
NI LEVEL NYENGIN
Great point, look at the top 100 of all African countries on Apple Music et al. You will agree with Salaam’s point the market reflect to what he is saying. Only, Northern African countries have high numbers of their musicians in those list.
Sipendi kuhulizwa maswali, so direct and straight forward salama. Keep it up miss
Hii jamaaa inawaza PESA tu.🙌 big up
Mwamba Salam hapa duniani hakuna marafiki wengi wanafiki sana wakiona una hela kidogo wanajisogeza , harmonize alipokua ananuka vikwapa hakuna aliyekua anajali wala kutaka kumsaidia, leo katoka anapata hela na mademu kila mtu anajifanya anampenda . bindadamu WANAFIKI kinoma noma
Nani aliye mtoa?
Napenda 'Kujiamini' kwa Salam SK, Big up, one of the people i would love kukutana nao FACE TO FACE niweze chimba madini mawili matatu.
Nakubal sana📢🥰🔞🧡
Marafik wanga tuu
Everytime ukimsikiliza salama unajifunza upya
THE SMART INTELLIGENCE MANAGER no need kuwa na friends oh yeah
Sallama hongera kwa kazi be blessed SK
"Mimi sina rafiki mimi ninawafanyabiashara" unyama ni mwingi sana.
azamzahoro6548 huyu jamaa ana maneno mazuri kweli unyama ni mwingi sana
Absolutely interview,big up sister Salama.
This guy is a good businessman
Big up SK kuazia leo nimekukubal salute 👏👏👏👏👏👏👏👏🍾🍾👑🤣🏃♂️🏃♂️
Jamaa kaongea point Sana
This man is businessman
Niliisubiri Sana Hii interview
Swali la mwisho zuri sana,Salama itabidi siku moja ujifanyie interview mwenyewe kwasababu unauliza vizur sana maswali nahisi hakuna anaekushinda.Halafu naomba niletee Alex Luambano wa Clouds
Show imekua Fupi Sana, Kuna Mambo mengi Sana yakuongea na Sallam Sk. Anamadini mengi Sana huyu mwamba.
*ila huyu jamaa ni kichwa asee 😂😂😂 hapa Diamond platnumz kapata meneja asee* 😂😂😂
Interview ya salama ni borrra 👏
Salam sk big up sanaaaaaaaaa
Naapa ....Najiona sahihi kwa mengi sana.
Biashara ina mambo mengi sana,hawa watu wanawekeza wanawekeza muda,pesa,na akiri zao halafu wewe unataka usaidiwe kwa huruma ya maneno.Hili haliwezekani hata kidogo.
Jamaa anaakili san
#Sallam ahsante kwa interview kali sana.
The man talk the truth
I feel like interviewing somebody like sallam you need more time..there were many issues about harmonize that were not asked e.g allegations he made at the airport,also issues around the exit of rayvanny and hanstone..
Let rat remain in the hole😒
P
Vijana wengi wakiweza kuiga mindset kama ya Sallam SK watafika itakuwa vizuri sana...
Jamaa anajibu maswal vizur sana, straight forward
Nimekuelewa sana salam
Mlete jamaa wa radio one wa habari nyepes
Bonge la interview ever huyu sallam ni intelligent sana
Is so real !
Hii nimependa sanaaa
Diamond
someone OG that's sallam SK Mendez 🤣🤣hataki unafiki
He is straightforward person!
@@rajabdibwa6415 yap
Nakubali hiki kipindi very 🔥🔥🔥🔥
Salama is best and first presenter in Tz and east africa since day one no cap
Salama your international for really 😘 may God bless you 🙏
Umetisha Sanaa sanaaa sk nakubariiiii sanaaaa
Ukiwa mnafiki huwez kumuelewa
Mendez Nimependa sn hii interview brother big up sn
Akili kubwa Mendez
HUU NI WAKATI WA MOND SASA ....WE NEED HIM
Nomaaaàa sana sallam
Salama na Diamond Platnumz next
Boss Mendez akili mingi sana. Anajua🙌
one thing i like about SK is that the man is real, hajui ku fake yan black is black
Wasafi itaendelea kuwa juu kwa menejas walionao jamaa yupo really anajitambua sana
I love Salam his business oriented
i like him🤣wao waseme sisi tunaenda kweli kweli
Yeah don Mendez🎹🎹
Big man congrats
Ninachokubali kuhusu hii shoo, yanaulizwa maswali yenye majib 'uncomfortable'....bonge la podcast!
That was life style harmonize issue
Salam maswali yako mazuri sana
Sk Multigenius
Safi
I like this guy
Hapo mwamba aksema ukweli... Tamaa ndio inasumbua wasanii, hilo nalifahamu... ata Rayvanny bado ni tamaa, ila tamaa mwisho wake mbaya sana... Ona Harmonize sahivi ana mihela na Range Rover, kajala atamlamba ata mkundu... mmakonde!! mumngu kamsaidie!!
namuelewa salaam bongo ukiwa na misimamo utetereki sio mnafiki lazima uchukiwe ndio kinachomtokea salama yuko straight msimamo hayumbishwi ndio maana anachukiwa
Wabongo ukiwachekea sana watakupanda kichwani ndio mana Saĺlam hana marafiki
Huyu jamaa kwenye issue ya business ni makin sana
Good interview
sk hakuwa na njaa nin
Don Mendez akili nyingi xna🙌🙌🙌
Diamond❤️❤️❤️
Wa kwanz
Bless
Ndo Boss Boing
Salam mtu mzuri ukiwa mnafki ndio utamuona anazingua .....but very straight guy👊
Ilauyo jamaa niatali 😂
Mendez kama Mendez
Boss Mendez
Alikiba anatchokwama ni views na consistently ya kutoa video za nyimbo haraka haraka kila mwezi kama mondi, hizo views haziji kwa fans tu, unaboost ili uonekane umefanya vizuri iyo season /12 months hii itamfanya apate nomination kwenye awards za nje ya nchi na kualikwa kwenye matamasha mbali mbali. Pia views ni ghali that's why mondi hana hata nyumba ameinvesting sana huko akipiga shows anaenda kuboosti ili ashikilie position ya juu.
Dada angu salama niweza pata angarabu nafasi nipige na ww pic tu....dada 😭
Waiting for Kitenge.
Interview ya salama.swal zur sana
Mwambaaaaa huyu hapaaaa ✌️✌️✌️✌️
We need a Salama na Platnumz Podcast And Harmonize Too✈️
jamaaa ana jiamini hatariiiii
Business, Mimi sina haja ya kukutana na sk ila he is a business minded
Good
#Mogul 🔥🔥🔥
He is mastermind
🙌
Boss kama boss
nakubali sanaaaa
Nice interview
Hamonize mibangi yule aache mibangi yule mibangi yake ndo inamharibu hamonize
Ht mm sipokei mkono. Wk ss msibani NDO nn kila. Kwani slm ndo mfiwa au korosho alitaka Kiki ndo maana alifanya vile
Jamaa anasauti kama ya ridhiwani kabisa
Sasa mbona hamjala hicho chakula jaman😪na mbona nyama tupu
😅😆😆😆
N'a base n'a kuskiliza WCB tuuuu
Salama aende The Joint
BossMendez
Hiv ile salama na Salma Msangi imeishia wapi mbona kila nikifungua nakutana tangazo tu kulikoni?
We needy part 3
Interview ya zuchu iko wapi
Huyu mkuu ako juu tu sana
Sallam is real!
Uyu ndo mwamba sasa...😂😂