Dizasta Vina - Almasi (Feat Tk Nendeze)

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 15 มิ.ย. 2023
  • A video lyrics of Dizasta Vina perfoming Almasi from the Album The Verteller
    Stream and Download Almasi
    Boomplay - www.boomplay.com/songs/63553588
    Audiomack - audiomack.com/dizastavina/son...
    Mdundo - mdundo.com/song/2081301
    Spotify - open.spotify.com/track/3Kl6Y9...
    Apple Music - music.apple.com/us/album/alma...
    Other contents
    Audiomack - audiomack.com/dizastavina
    Boom play - www.boomplay.com/artists/3288611
    Mdundo - mdundo.com/a/2263
    Spotify - open.spotify.com/artist/1IC2b...
    Apple music - / dizasta-vina
    Connect with Dizasta Vina on social medias
    Instagram - / dizastavina
    Twitter - / dizastavina
    Facebook - / dizastavina07
    sw.wikipedia.org/wiki/Dizasta...
    Business: Pan.authentik@yahoo.com
    Website - bio.link/dizastavina
    Lyrics
    Nilikutana mtaani na Mzee mmoja
    Tukaketi chini akanipa soga
    Mimi sitamsahau
    Alisema wangapi walikuwepo namba moja
    Sasa wamerudi chini ni vioja
    Watu wamewasahau
    Utavamia kwenye tamasha la muziki
    Usoni bashasha huku rohoni umeikumbata dhiki
    Sanaa imesanda na sasa tena hauna kiki
    Utaigiza furaha kwa kunywa bia za mashabiki
    Zitaongea nguo ulizoazima kwa msela
    Hazitatosha kuficha ukweli kwamba hauna hela
    Hautakumbukwa kama mwanzo wakati unatisha
    Paparazi hawatakujua so hautapigwa hata picha
    hakuna atakayekuangalia usoni
    Tamasha utaingia kwa kuzidandia kuponi
    Mchumba uliyemmwaga atang'ang'aniwa kiunoni
    Utatabasamu huku hasira umeifungia moyoni
    Utapotaka kujichanganya utahisi haya
    Lipsi denda zitachakaa kusizi kaya
    Watasikika wadadisi wakiongea kwa kudisi
    Kamera zote zitamfata msanii uliyemu-Inspire
    Hayatakuwepo majumba magari na mapochi nene
    Milo ya hoteli za kifahari na ma-roast kede
    Zitasahaulika idadi ya tuzo ulizohodhi kwenye majukwaa
    Huku magazeti yakiku-Post mbele
    Hautatembeza tena rungu ka' Kipepe
    Hautavutia Wachuchu maana nyota haina nguvu
    Hautafatwa tena na Mashushushu kwa maseke
    Utakumbuka ulivyozungukwa na grupu la Vicheche
    Michuzi itakauka utapiga hodi ukame
    Hautawekwa kwenye ma-board ka' Van Dame
    Hautashawishi magari road yapangane
    Na utakuwa peke yako bila ya ma-Bodyguard nane
    Kipindi ambacho taswira yako ipo gado
    Ndo' kipindi cha kulikata shauri lako
    Kutambua nafasi na thamani ya sauti yako
    Kutambua dhamana mapema kabla ya mauti yako
    Dhamana yako ni zaidi ya kula na kupiga pamba kali
    Kununua Bupa na chupa ukizilaza chali
    Jina kubwa likikufumba ushindwe tafakari
    Utakufa masikini ukizubaa kuzichanga mali
    Usijesahau maisha yako halisi
    Yanayolingana na kipato chako thabiti
    Usijekufa kipindi ambacho michango haikidhi
    Haitoshi hata kujenga nyumba ya mama'ako Kibiti
    Uko wakati wa kumiliki idhini ya uwongo wako
    Wenzako wamedondoka, Je utajifunza?
    Unasifika mjini kwa wingi wa longo zako
    Ukifa tutasimulia nini watoto wako
    Tutasimulia idadi totoz ulizonusa
    Au gambe idadi ya Kopo ulizoruka
    Idadi ya mahusiano au idadi ya mioyo uliyoivunja
    Au idadi ya wasichana wadogo uliowavuruga
    Najua mwisho mwanangu hamna njia
    Utatokewa na kila hadithi uliyoisikia
    Sicho kitu ninachokihofia
    Hofu yangu kama umeshaiandaa saikolojia
    Ukija wakati pazia halifunguki
    Wadananda uliowadandia hawakukumbuki
    Najua itafanya akili ichoke utapagawa
    tafadhali usijegeukia pombe na madawa
    Kipandacho hushuka ulishawaza
    Si muiujiza ni asili inayoshangaza
    Wasahaulifu Walimwengu ilitangazwa
    Watataja mashujaa na jina lako halitatajwa
    Wanafki, Walafi na Mabishoo zako
    Wangapi watakuwepo kiu ikidaka koo lako
    Muda wa kuwasoma wote waliopo kando yako
    Maana hata pesa haitatibu jelaha la roho yako
    Maagano ya siri yatakuwinda
    Vyote walivyotabiri vitafika
    Maisha ya ndoto yataisha
    Utairudia kawaida utagundua kuwa haukuwa malaika
    Kiasi utajua dini
    Utajua harufu ya sakafu kwa maana utakuwa chini
    Hata maana ya maisha itapotea
    Sumu, Kisu na vitanzi vitasogea
    Sikutishi ila utakufa peke yako
    Jeneza lako halitabebwa na hao vicheche wako
    Sishangai wenge lako, Ng'ombe
    Nashangaa unapoyumba kwa kuzidiwa na ukubwa wa pembe lako
    Ni heri kuwa mwewe
    maana mwoga anajali kuwa uelewe
    Kundi la watoto nyumba wanakupenda
    Na wanaota siku moja waje kuwa kama wewe

ความคิดเห็น • 411

  • @charlesjuma5698
    @charlesjuma5698 ปีที่แล้ว +13

    G.O.A.T

  • @prof.abusakelsaleh3524
    @prof.abusakelsaleh3524 ปีที่แล้ว +19

    Almasi inaweza kuwa lugha ya picha tu katika fasihi,ina maana katika hali ya maisha hasa ujana kuna wakati tunapata fedha nyingi,badala ya kuwekeza tunafuja kwa pombe na wanawake,hivyo almasi inaweza kuwa muda wa ujana na pindi almasi itakapoisha na wakati huo huna kitu ndipo kila mtu atakuwa kinyume nawe....Almasi sio tu Diamondi Platnumz ila ni fumbo na picha kubwa ya maisha ya ujana na uwekezaji kuhusu kesho yetu.

  • @alphaabdallah1406
    @alphaabdallah1406 ปีที่แล้ว +21

    Watoto mnasikiliza hii ngoma mwaka 3000, huyu Jamaa zetu tulimfanya shule ngoma zake kadhaa tulitumia kutongozea mademu

  • @dillungajrgasper9178
    @dillungajrgasper9178 ปีที่แล้ว +28

    Wakwanza naombeni like zangu Kam unamkubali black maradona

  • @zuzubonye5243
    @zuzubonye5243 ปีที่แล้ว +3

    Hii ngma c kwa dis track kwa mond ila hii ngma inazungumzia maisha ya bnadam yoyote alie na nafuh ya maisha kwa mda furan na kushndwa kufanya v2 vya mana kma wakina mack muga

  • @abeidsocco6211
    @abeidsocco6211 ปีที่แล้ว +6

    Yaan huyu mjumbe wetu angekua mtu wa mitandao ya kijamii basi hakuna msanii wa hip hop angekua anasikika,,huyu ni genius ,anakuandikia,anakuimbia na anakusimulia,dizasta vina👐

  • @sebastianlubava1535
    @sebastianlubava1535 ปีที่แล้ว +1

    Ii Lesson inaenda kwa Mr Almass mwenyew ama?

  • @ramadhankakai7303
    @ramadhankakai7303 ปีที่แล้ว +1

    Mashabiki wa diamond platnumz hamjambo😂

  • @calvinloveambroce842
    @calvinloveambroce842 ปีที่แล้ว +2

    Mimi ni shabiki mkubwa wa dizasta na alichonifuraisha ni kwamba yupo one man army na huku akijua kuwa kwenye muzik industry ya Tanzania uwezi toboa bila kumhusisha diamond kwenye muzik wako kikubwa tutambue kuwa tumebarikiwa kupata rapper km dizasta lakini pia MUNGU amutupa zawadi kubwa sana kwa kumuumba diamond akiwa mtanzania ili kuwa msaada kwa vijana wa kitanzania kwa maana hii ngoma ya dizasta itakuwa kubwa kuliko zote kwakuwa diamond amehusishwa hapa MUNGU ibariki Tanzania mungu mbariki dizasta lakini MUNGU akubariki kwa ukubwa zaidi DIAMOND PLATNUMZ ili uendelee kuwa daraja kwa watanzania

  • @underratedspirit
    @underratedspirit ปีที่แล้ว +2

    Kwani hii ngoma ni special kwa Diamond Platnumz?!

  • @nokeytz
    @nokeytz ปีที่แล้ว +1

    Wasanii tumechanwa tuelimike

  • @southernboeofficial5490
    @southernboeofficial5490 ปีที่แล้ว +4

    HII NGOMA NI MOJA KWA MOJA INAMLENGA DIAMOND PLUTNUMZ😂😂😂 AISEEE NOMAAA...

  • @salutarisliganga7314
    @salutarisliganga7314 ปีที่แล้ว +20

    This guy is a genius🫡..

  • @hallowkij5677
    @hallowkij5677 ปีที่แล้ว +2

    amemzungumzia diamond platnm ,,,,hakumtaja ila ameeka diamond

  • @zainabmaulid9637
    @zainabmaulid9637 ปีที่แล้ว +2

    Rapcha mavi umesikia mistar kutoka kwa kichwa timamu yani haya maneno ni chakula cha ubongo %

  • @scarface_wilach
    @scarface_wilach ปีที่แล้ว +3

    Leo nakuwa viewer wa kwanza, piteni na kwangu🤐

  • @focusoscar9830
    @focusoscar9830 ปีที่แล้ว +2

    hii ngoma inamuhusu diamond platnumz

  • @dullywamashairi121
    @dullywamashairi121 ปีที่แล้ว +2

    Hakuna mayooyoo humu, n mawe tupu!! Dizasta Vina n Robot lakuandika, ama n Jini flani hv ambaye anatoka Dunia ya mbali huko ujinini kuja kutuelekeza duniani

  • @frankphilipo2930
    @frankphilipo2930 ปีที่แล้ว +3

    Kaa ameambiwa chid kwa namna Fulani hivi

  • @kareemmadusa4039
    @kareemmadusa4039 ปีที่แล้ว +2

    Ngoma yakitambo sana ila kama mpya asee siichokagi