Watatu wafariki kwa ajali Lindi, wapo mapadri wawili

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 11 ก.ค. 2024
  • Watu watatu wamefariki dunia wakiwemo mapadri wawili na wengine wawili kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wamepanda kupata ajali katika eneo la Mtama mkoani Lindi.
    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi ACP, John Imori akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Ijumaa Julai12, 2024 amesema kuwa ajali hiyo imetokea saa12.00 asubuhi katika eneo la Mtualonga Barabara ya Masasi -Mnazi Mmoja katika Halmashauri ya Mtamaa mkoani Lindi.
    Amesema gari aina ya Mitsubishi Outlander iliyokuwa ikitokea Ndanda kuelekea jijini Dar es Salam ililipiga shimo na kupoteza mwelekeo na kuacha njia kisha kutumbukia kwenye shimo la karavati na kusababisha vifo na majeruhi wawili.
    Kamanda Imori amewataja waliofariki kuwa ni Cornelius Modoe (55), Padri wa Kanisa Katoliki wa jijini Dar es Salaam, Pius Boa (51) na Padri wa Kanisa Katoliki na mkazi wa Tanga Haphymark Mkenda (51).
    Imeandikwa na Bahati Mwatesa

ความคิดเห็น • 14

  • @fridanguli2271
    @fridanguli2271 23 วันที่ผ่านมา

    Mungu awapokee kwake watumishi wake na majeruhi wapate matibabu na wapone haraka. Pole kwa kanisa Katoliki kwa kuondokewa na watenda kazi wake

  • @seciliaduma2944
    @seciliaduma2944 22 วันที่ผ่านมา

    Polen Sana mapadre wetu kwa kuondokewa na watumidhi mungu azilaze roho za marehemu mahala pema pepon Amina😭😭😭

  • @ElishaSolomoni-kc4zk
    @ElishaSolomoni-kc4zk 23 วันที่ผ่านมา +1

    DAH AISEE R.I.P MAPADRI WETU 😭😭😭😭😭

  • @hawaelymaricca7602
    @hawaelymaricca7602 24 วันที่ผ่านมา

    Eeh Mungu turehemu, Wapumzishe Roho za marehemu salama na uwapunguzie adhabu ya kaburi.Poleni sana ndugu wa marehemu Mungu awatie nguvu kwa kipindi hiki kigumu mnachopitia.

  • @chikujuma18
    @chikujuma18 24 วันที่ผ่านมา +2

    Inalilaahi wainalilah rajighun polen jaman wanafamilia pamoja na jamaa zenu wote walio fariki😢😢😢

    • @user-ns1dg4jd7q
      @user-ns1dg4jd7q 18 วันที่ผ่านมา

      Sisi sote ni wa mwenyezi Mungu na kwake tutarejea ubarikiwe sana kwa pole yako 😭😭😭

  • @RICHARDMICHAEL-o1e
    @RICHARDMICHAEL-o1e 23 วันที่ผ่านมา +1

    Wapumzike Kwa aman

  • @GrandYounaitha
    @GrandYounaitha 24 วันที่ผ่านมา

    Yesuuu wangu wabariki wote

  • @YOHANAKIHEDU
    @YOHANAKIHEDU 24 วันที่ผ่านมา

    Jamani da siamin macho yangu

  • @magdalenamushi8081
    @magdalenamushi8081 24 วันที่ผ่านมา

    Pumzikeni kwa Amani ndugu zetu

  • @YOHANAKIHEDU
    @YOHANAKIHEDU 24 วันที่ผ่านมา

    Jamani dah paroko zangu 😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢

  • @germanasondoka9057
    @germanasondoka9057 24 วันที่ผ่านมา

    RIP Wapendwa wetu

  • @joycehaule9717
    @joycehaule9717 24 วันที่ผ่านมา

    Mwaka wa mapadre huu