NDOA ZA MITALA: JE KUNA KOSA LOLOTE KUOA WAKE WENGI? MBONA WATU WA AGANO LA KALE WALIOA WAKE WAKE?

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 24 ก.ค. 2021
  • Ndoa ya Kikristo ni ndoa ya mke mmoja na mume mmoja, na inapaswa kufungwa kwa kuzingatia sheria za kanisa, serikali na tamaduni husika. Hata hivyo, katika jamii nyingi duniani tangu zamani kumekuwepo na ndoa za mke zaidi ya mmoja.
    Waafrika wengi hawaoni kwamba ni jambo geni kuingia katika ndoa za mitala. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mwanaume wa kiafrika anaweza kuoa mwanamke mwingine wakati wowote ule bila shida. Nakumbuka kanisa moja nililowahi kusali nilipokuwa kijana mdogo lilikuwa linaitwa Last Church of God, ambalo kwa lugha ya Kisukuma linajulikana kama “Bhatola Mhali” yaani “waoao wake wengi,” kanisa hili lilikuwa linahalalisha kabisa kuoa wake zaidi ya mmoja. Mwinjilisti wa kanisa hilo alikuwa na wake wawili. Kanisa hili hudai kwamba mpango wa Mungu kwa wanadamu ni kuhakikisha kwamba mwanaume anaoa wanawake wengi kwa kadri awezavyo, ikiwa tu ana uwezo wa kuwahudumia.
    Hata hivyo, mpango wa Mungu haukuwa kwamba aweze kuoa wake wengi, kwani alipomuumba Adamu alimwumba na Hawa nao walikuwa wawili tu. Hata hivyo kwa sababu ya anguko la mwanadamu, kwa sababu ya dhambi mwanadamu alijitwalia wake zaidi kwa kadri alivyotaka.
    Ndoa ya mitala ya kwanza katika Biblia ni ile ya Lameki katika Mwanzo 4:19 "Lameki alioa wanawake wawili." Na baadaye tunaona watu wengi muhimu katika Agano la Kale wakiwa na mitala; kwa mfano Ibrahimu, Yakobo, Daudi, Sulemani, na wengine. Katika 2 Samweli 12:8, Mungu, akizungumza kupitia nabii Nathani, alisema kwamba kama wake na masuria wa Daudi hawakutosha, naye angempa Daudi zaidi. Hii inamaanisha nini? Pia, Sulemani alikuwa na wake 700 na masuria 300. Kuna maswali ambayo pengine yangefaa kupatiwa majibu kadhaa; Kwa nini Mungu aliruhusu mitala katika Agano la Kale? Mungu anaionaje mitala leo hii? Hebu kwanza tuone ndoa kadhaa za wake wengi katika Biblia.
    FUATILIA SOMO HILI.
    USISAHAU PIA KUPATA KITABU CHA MAADILI YA KIKRISTO

ความคิดเห็น • 49

  • @williamogal2840
    @williamogal2840 หลายเดือนก่อน +1

    Mume ni Askofu mkuu nyumbani mwake, basi mutu asie na mke achukue huduma aama awe na mke Moja.Tmoth 3:1_ .

  • @festinamwakipale3919
    @festinamwakipale3919 17 วันที่ผ่านมา

    Kwanza ukioa wanawake wengi lazima wakufundishe uchawi na uganga na ufreemasoni wanaume yeye Mungu anasema lakini mke mwema Mungu ndie anaemjua ko msifikili kila mke nikuowa noooo

  • @ZakayoYohana
    @ZakayoYohana 2 วันที่ผ่านมา

    Sio msimamo wakanisa nimsimamo wako

  • @williamogal2840
    @williamogal2840 หลายเดือนก่อน

    Daudi /Solomoni Jehova aliwapa wake kulingana na uwezo aliwapa na huduma.Tunona Mungu akisema ukioa mke wapili mpe sawa na yule wakwanza.

  • @faustinconrad2554
    @faustinconrad2554 20 วันที่ผ่านมา

    Nashukuru kwa ufafanuzi, ila nimegundua kuwa wazungu walituathiri sisi Wakristo.

  • @mmasaalonda499
    @mmasaalonda499 25 วันที่ผ่านมา

    Ubarikiwe nimekuelewa mimi
    Wegine hawakuelewa nakutowa matusi nimewatambua

  • @user-bw1wn3sz4z
    @user-bw1wn3sz4z 2 หลายเดือนก่อน +1

    Mwenye wake wengi,afundishwe na achaguwe nini?Kama ameingiya kanisani akiwa na wake wengi apokelewe hivo na aendeleye alivyoitwa.kufukuza mke Kwa mujibu wa mafundisho ya kanisa ni uongo,

  • @williamogal2840
    @williamogal2840 หลายเดือนก่อน

    Tusiache neno ndoa kuwa fumbo.Mungu alimanisha mume kuwa(mbegu) mke kuwa(shamba).Nina semanini? Uwe na shamba Moja hau mbili Niya mtu Moja.

  • @AliSalim-yu4mo
    @AliSalim-yu4mo 3 หลายเดือนก่อน

    Nimekuelewa mchungaji yeye haitaki Bibilia kama muongozo wake Bali yeye anafuata utaratibu wa Kikristo,na kama amechambuwa Kwa mujibu wa Bibilia basi itabidi akakae Chino aiangslie vizuri maana ktk bibilia sio Tu ni matala Bali kuwa watu walioa wake mia❤🎉

  • @KasmiryKados
    @KasmiryKados หลายเดือนก่อน

    Mitala sio dhambi kwa mungu.ila ni dhambi kwako.toka na ushetani wako.kwanza nimegundua hujui kanisa nini nenda darasani upya.

  • @Nurumidia
    @Nurumidia ปีที่แล้ว +3

    Mchungaji mahesabu yako yako tofauti na neno la Mungu kabisa mbona huja toa ndiko ambalo Mungu anasema "" usiongeze mke mwingine ??"" Unamsingizia yesu juu ya ndoa kwamba hakutaka kabisa duhbh wachungaji washile mna chekesha sana

    • @revdrseni
      @revdrseni  หลายเดือนก่อน

      Usioe wake zaidi ya moja

  • @MSOMBAAlon-gh3ps
    @MSOMBAAlon-gh3ps 14 วันที่ผ่านมา

    Kuoa mke wa pili ni zambi ila ndo za jinsia moja hizo ndo hakuna shida

  • @BM_Smart2-6
    @BM_Smart2-6 หลายเดือนก่อน +2

    Ukristo ni mzuri sana ila naamini wazungu walituchakachua mahali kwenye dini ya Kikristo kulazimisha kuwa Kikristo; mume anapaswa kuoa mke mmoja tu, hili halikuwekwa sawa. Kwa sababu hiyo wanaume wanakufa mapema na kuziacha familia na wajane wengi, wanaume wengi wamekosa furaha na kuwa na msongo wa mawazo ya mke mmoja na kufa kimya kimya. Dunia hii ni ngumu hivi sasa ukahaba na ushoga ndiyo umeshika kasi balaa, hilo jambo la kuoa bado ni fumbo

    • @user-ki6mk5xx5g
      @user-ki6mk5xx5g หลายเดือนก่อน +1

      Wake wengi ndio mpango wa Mungu tuache kupotosha ukweli mume mke ndio kiwanda cha Mungu mkubali ushoga mujengee nyumba

    • @mathiasmuhochi435
      @mathiasmuhochi435 10 วันที่ผ่านมา

      Wazungu wamelisha watu matango pori.....baba wa Imani Ibrahim, Jackobo, daudi, suleman , Musa aliyekabidhiwa amri kumi na Mungu ....wote hao walikuwa na wake zaidi ya Moja...lakini Mungu hakuwaonya kuwa Hilo ni kosa.......Pia Mungu hakosei Kwa kuumba wanawake wengi kuliko wanaume... Ili waje kuteseka duniani Kwa kukosa waume wa kuwaoa....alijua Mwanaume ataoa mke zaidi ya mmoja

  • @herbertbathlomeo4650
    @herbertbathlomeo4650 29 วันที่ผ่านมา

    swali la msingi sio visingizio onesha wapi Mungu kazuia kuoa wake wengi msimamo wa Mungu ni upi? ukianza kusema ohhh walikuwa wanauawa vitani ndo maana Mungu aliruhusu wapi aliruhusu kwa kauli yake? kama hajaweka msimamo waambieni watu wawe huru kuoa muhimu watimize mahitaji ya wake zao maana wanaume hawajawahi kukosa wanawake wa kuoa ila wanawake wanakosa wanaume wa kuwaoa kisa ratio yao kuwa kubwa kuliko ya wanaume

  • @user-oq6sh8qh5g
    @user-oq6sh8qh5g 9 หลายเดือนก่อน

    Waisrael ambao na waasisi wa iman na manabii mpaka leo wao wanaoa wake wengi na hakuna tatizo ,iman ya kuto kuoa wake wengi ni iman ni wa mangaribi na siyo msimamo wa Mungu kwa kawada hana neno ni uwezo wake tu

  • @JeromeBuretta
    @JeromeBuretta หลายเดือนก่อน +1

    Kwenye hiyo hesabu sijaelewa. Swali: NI NANI ANAYEENDA KUUNGANA? NI MKE AU MUME? Maana kama mke anaenda kuungana na mume basi yaweza kuwa hivi:
    1+1=1
    1+1=1
    1+1=1
    Maana 1=Mume na 1=Mke
    Yaani kila mke anaolewa kivyake

  • @tendomakori1917
    @tendomakori1917 ปีที่แล้ว +3

    Hizo ni Propaganda tu.Huo ni mpango wa wazungu tu.Mbona Mungu aliwatumia Poligamists kufikisha ujumbe wake na aliwabariki sana.Suleman, Yakobo, Ibrahim, etc.Hata agano jipya limeruhusu.Soma timotheo vizuri.

  • @HenrickMhema
    @HenrickMhema 2 หลายเดือนก่อน

    Sisi wakristo ndo tumesababisha kuwe na makahaba wengi,ubakaji,na hata ushoga na usagaji.

  • @sosmakanya4901
    @sosmakanya4901 2 หลายเดือนก่อน

    Inashindikanaje kama moja jumlisha moja, ni moja kama hesabu hiyo ipo sawa basi moja jumlisha mbili ni sawa na, moja hadi hapo utakapi nipa logic ya 1+1= 1. Logically chungwa, moja ukiongeza machungwa mawili jibu sio limao Bali ni chungwa tu. Kwa hiyo mtu mme ongeza mtu mke jibu ni mtu

  • @user-ki6mk5xx5g
    @user-ki6mk5xx5g หลายเดือนก่อน

    Hujui chochote usilukie mada fundisha ushoga na usagaji Huna lolote

  • @KasmiryKados
    @KasmiryKados หลายเดือนก่อน

    Mitala sio dhambi kwa mungu.ila ni dhambi kwako.toka na ushetani wako.kwanza nimegundua hujui kanisa nini nenda darasani upya.😂😢

  • @Nurumidia
    @Nurumidia ปีที่แล้ว +2

    Mtumishi soma biblia vizuri kila andiko linatafsiri yake sahii katika biblia tafadhali usitafsiri biblia kwa elimu yako tambua neno la Mungu ni ufunuo wala sio elemu kutoka kwa watu ipo sheria ambayo Mungu aliiweka endapo mtu atataka kuongeza Mke Mwingine azingatie nini kwamujibu wa Mungu hivyo watu wawili wanakuwa Mwili mmoja mara baada tu ya kujamiana hivyo mwanaume akienda tena kujamiana na mtu mwingine anakuwanaye mwili mmoja tena mwanamke anakifungo kwa mwanaume mwanaume hana kifungo chochote kwa Mujibu wa neno la Mungu ndoa ya wake wingi sio mpango wa mwanadamu ni mpango wa Mungu kama hautojali nakupa maandiko

    • @lenardkenedy542
      @lenardkenedy542 8 หลายเดือนก่อน

      Jifuze Zaid Ndugu

    • @mathiasmuhochi435
      @mathiasmuhochi435 หลายเดือนก่อน +1

      Jaribu kusoma andiko na kulielewa..... Abraham, Jackob, sulemani, Daudi na hata Musa hao wote walioa mke zaidi ya mmoja...

  • @user-ox6rb3wj5w
    @user-ox6rb3wj5w 8 วันที่ผ่านมา

    Akuna mwanA ume mwenye mke moja ni uongo tu,wanasema kwa midomo tu,miyoni ni uhongo tu,Wana mahawala kibao,je kipi kizuri kuoa wake zako au kuwa na mahawala?

    • @odilomwemeziernest646
      @odilomwemeziernest646 8 วันที่ผ่านมา

      Huo ni mtazamo wako kulingana na udhaifu wako,ila mimi nipo nimeokoka,sina hawala ninaishi na mke wangu na watoto wangu.hilo wazo lako ni la wale watetea tamaa.

  • @athumanijumanne4685
    @athumanijumanne4685 ปีที่แล้ว

    Usizunguuke waislam wako sawa kuoa wake wengi wakilisto nyie oeni kama wsislam ili kupunguza wimbi la wanawake wanao ongezeka kila uchwao badilikeni

  • @ayubutwalbu6594
    @ayubutwalbu6594 2 หลายเดือนก่อน

    Wewe huna elimu kabsa unapga kelele tu

  • @silveriusfungilwa5995
    @silveriusfungilwa5995 5 วันที่ผ่านมา

    Wee mwongo hujui hata kufafanua wapi biblia au mungu anasema mke zaidi ya mmoja nidhambi. Msilete shiria za kishetani huku. Huo ni mpango wa shetani kuua ukristo biblia inasema yafaa askofu awe mume wa mke mmoja. Sio wakristo wawe na mke mmoja.

    • @revdrseni
      @revdrseni  5 วันที่ผ่านมา

      Ndugu, kama unataka kuoa wake wengi, oa tu

  • @faustinconrad2554
    @faustinconrad2554 20 วันที่ผ่านมา

    Hakuna kifungu ndani ya Biblia kinacho mzuia mtu kuoa wake wengi.

    • @Wamisangi
      @Wamisangi 6 วันที่ผ่านมา

      Hujakutana na huu mstari
      Mathayo 19:9. Ukimuacha Mke wako wa ndoa ukao mwengine umezini. Hapo hamna uwingi ni umoja.
      Lakini ukisoma hapo hapo Mathayo 19:1-12 ambapo Bwana Yesu alikuwa akifundisha kuhusu baada ya kutaka kujarubiwa na Mafarisayo, utaona mstari/aya wa 4 na 5 utaelewa tangu manzoni mungu aliumba mtu mke na mtu. Na kama haitoshi watakuwa mwili mmoja wakiona. Sasa ni ukuulize mwanamune atakuwaje mwili mmoja na wakened zaidi ya mmoja? Ama mwanamke anakuahe mwili mmoja na mumewe wakati wako wengine wanaochangia naye huyo mume?
      Hosea 4:6a.😢

  • @HenrickMhema
    @HenrickMhema 2 หลายเดือนก่อน +1

    Mi nahisi sisi wakristo tunaenda kinyume Sana na biblia kwasabu Katka mitume walioandikwa kwa biblia wote walikua na wake Weng isipokua isaka Tu yeye ndo alikua na mke mmoja

    • @mathiasmuhochi435
      @mathiasmuhochi435 หลายเดือนก่อน +1

      Abraham, Jackob, Mfalme Suleiman, Daudi na hata Musa aliyewatoa wana wa Israel utumwani Misri.... Wote walioa wake zaidi ya mmoja

  • @festinamwakipale3919
    @festinamwakipale3919 17 วันที่ผ่านมา

    Jaman lakin mbona Yesu agano jipya ametoa maamuzi na msimamo wa Mungu mathayo 19 Yesu anasema ni kwa ugumu wa mioyo yenu aliyeumba aliumba mke na mume na.anasema na hao wawili hawatakuwa wawili watakuwa mwili mmoja kuoa mke.zaidi ya mmoja ni ugumu.wa moyo wanaume acheni.tamaa ndio mAana mnakufa haraka mnasingizia majukumu machozi ya.wamama.na.watoto ni.mengi.kila.sehemu tulien.mheshimuni Mungu na neno lake na ukioa mke sio kwamba majukumu yameisha kuna majukumu ya familia mbili.haya ukioa wanawake sita utahudumia familia saba ndo mnaingliwaga na maloho mabaya mnaanza kuombewa mfe wanaume nawashauri mkioa.mke zaidi ya mmoja.sio kwamba Mungu awaue ila mnamchukiza

    • @williamogal2840
      @williamogal2840 5 วันที่ผ่านมา +1

      Festina mwakipale,Yesu anasema kwa ugumu wa moyoyenu yakupenda Talaka haikua hivio tangu mwanzo.Mtu ashikamane na mkeo,Kutoka 23:21mke apate huduma sawa,si Talaka.

    • @festinamwakipale3919
      @festinamwakipale3919 5 วันที่ผ่านมา

      @@williamogal2840 ndio logo wa bwana akitaka uhubili.watu mambo ni mengi kuhusu.ugumu wa mioyo Moja Musa.aliwaona Wana mioyo migumu ma'ana waliishi.kwenye makambi lakini waliachana kwA talaka jaman hivi umewahi linyumbulisha neno mioyo migumu lakini yeye aliyeumba aliumba mume na mke nao hawatakuwa wawili bali mwili mmoja hapo.sasa.wenye.mioyo migumu hawakubali

  • @athumanijumanne4685
    @athumanijumanne4685 ปีที่แล้ว

    Mkiishi kwa kumfata yesu alikua msela hajaoa kabisa asinge weza kuwashari kitu yeye mwenyewe hajaoa

    • @Nurumidia
      @Nurumidia ปีที่แล้ว

      Habari za kufanana na yesu tuna fahamu sisi wa kristo tuna fanana na bwana wetu yesu kristo katika jambo gani so kuoa hakuna faida yoyote katika kupata uzima wa milele au kukombolewa katika dhambi yesu akuja kwaajili ya faida ya mwili bali kwaajili ya roho zetu ili sisi wanawe tulio potea tumjuwe yeye aliye wa kweli mwisho wa ndoa ni hapa duniani

  • @constantinebugingo5988
    @constantinebugingo5988 2 หลายเดือนก่อน

    Fundisha kwa mwongozo wa biblia si kwa mawazo yako.

  • @ramadhanmwandambotuntufye5972
    @ramadhanmwandambotuntufye5972 หลายเดือนก่อน

    Yaani wewe mchungaji ni muongo, ukifa jahannam inakuhusu utakuwa ni kuni katika kuni za watu

  • @KasmiryKados
    @KasmiryKados หลายเดือนก่อน +1

    Mitala sio dhambi kwa mungu.ila ni dhambi kwako.toka na ushetani wako.kwanza nimegundua hujui kanisa nini nenda darasani upya.

    • @revdrseni
      @revdrseni  5 วันที่ผ่านมา

      basi mpendwa, oa mke mwingine