Eng. Fatma Rembo Awafunda Wanawake UWT Kilolo-Iringa "Tuache Wivu, Tuinuane, Tugombee Uongozi"

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 16 ต.ค. 2024
  • Mhandisi Fatma Rembo ambaye ni Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) kutoka mkoa wa Iringa, ameahidi kuwaunga mkono wanawake wote watakaojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi ambapo amesisitiza kuwa wanahitajika wanawake wenye uwezo ili kuhakikisha ushindi unapatikana, kazi nzuri zinaonekana a maendeleo yanatokea baada ya kuchaguliwa.
    Fatma Rembo ameyasema hayo Julai 18, 2024 alipokuwa mgeni rasmi katika Kikao cha Baraza la Umoja wa Wanawake CCM Tanzania (UWT) wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ambapo ametumia fursa hiyo kuwataka wanawake kuacha tabia ya kuoneana wivu bali washirikiane kunyanyuana wenyewe kwa wenyewe bila kukatishana tamaa.
    "lazima kuwepo na watu wa kuwaunga wanawake mkono na kuhakikisha hawakatwi majina yao, tunaweza kuwahamasisha wakajitokeza wengi, wakikatwa majina yao tunakuwa tumepoteza, nawahakikishia, tutasimama kuhakikisha wanawake tunaingia kwa kishindo" - Amesema Fatma Rembo.Subscribe (Focus Digito TV) ili usipitwe na Video mpya zinazotoka kila siku.
    Focus Digito TV inakupa Maudhui Mazuri yanayohusu Habari, Elimu, Mitindo ya maisha, Michezo na Burudani.
    Focus Digito TV is here to provide you with contents about News, Education, Lifestyles, Sports and Entertainments.
    #FocusDigitoTV
    ..................
    Tufuatilie Zaidi kupitia:
    INSTAGRAM, TIKTOK, FACEBOOK, TWITTER (X), THREADS NA GOOGLE WEBSITE YETU YA FOCUS DIGITO TV
    Focus Digito TV is one of the best info-edu-tainment Online Media conveying contents for the Public Interest.
    Asante kwa kuchagua kutufuatilia | Thanks for Subscribing
    We Love You | Tunakupenda
    Regards
    Team FocusDigitoTV

ความคิดเห็น •