Migogoro ya Wafugaji na Wakulima Iringa | DC Kheri James Aendesha Kikao na Wafugaji Afunguka Haya

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 16 ต.ค. 2024
  • Mkuu wa wilaya ya Iringa, Kheri James, amefanya Mkutano maalumu na Wafugaji wote Tarafa ya Pawaga iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mkoani Iringa kwa lengo la kusikiliza changamoto wanazokumbana nazo ili kutafuta Suluhu ya Migogoro inayoibuka kati ya Wafugaji na Wakulima katika tarafa ya Pawaga wilayani humo.
    Akizungumza katika Mkutano huo uliofanyika Oktoba 15, 2024 ukiwakutanisha wafugaji kutoka kata zote zinazounda tarafa ya Pawaga, DC Kheri James amewataka wafugaji hao kutoa ushirikiano wakutosha kwa Viongozi wa Serikali na Jeshi la Polisi ili kuwezesha mchakato wa kutafuta suluhisho la kudumu la Migogoro ya Wafugaji na Wakulima kufanyika kwa Wepesi na kwa wakati bila kukumbana na changamoto au vikwazo vyovyote vinavyoweza kuchelewesha mpango wa kumaliza migogoro hiyo.
    Sambamba na hilo, DC Kheri James, amewata Wafugaji hao kuwa wavumilivu huku wakitunza amani iliyopo kwa kipindi ambacho anashughulikia changamoto na kero zote walizowasilisha kwake ambapo amewaahidi kurudi tena akiwa na majibu kamili ambayo yatakuwa na manufaa kwa pande zote mbili kati ya Wakulima na Wafugaji katika tarafa ya Pawaga ili kumaliza migogoro iliyopo inayochangia kukwamisha baadhi ya Shughuli za uzalishaji na maendeleo kwa ujumla katika tarafa hiyo.
    Subscribe (Focus Digito TV) ili usipitwe na Video mpya zinazotoka kila siku.
    Focus Digito TV inakupa Maudhui Mazuri yanayohusu Habari, Elimu, Mitindo ya maisha, Michezo na Burudani.
    Focus Digito TV is here to provide you with contents about News, Education, Lifestyles, Sports and Entertainments.
    #FocusDigitoTV
    ..................
    Tufuatilie Zaidi kupitia:
    INSTAGRAM, TIKTOK, FACEBOOK, TWITTER (X), THREADS NA GOOGLE WEBSITE YETU YA FOCUS DIGITO TV
    Focus Digito TV is one of the best info-edu-tainment Online Media conveying contents for the Public Interest.
    Asante kwa kuchagua kutufuatilia | Thanks for Subscribing
    We Love You | Tunakupenda
    Regards
    Team FocusDigitoTV

ความคิดเห็น •