NAHODHA - Vitali Maembe (2021)

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 5 ก.ย. 2024
  • NAHODHA
    Wewe Nahodha x2
    Shusha tanga pepo zime chachamaa!
    Nanyi abiria pigeni mbizi,
    Muwezavyo chombo kimechota maji!
    Haya wanafiki, vishuka,
    Nipeni leo hilo jina baya mniue!
    Msoitakia mema nchi yangu,
    Nipeni leo hilo jina baya mniue!
    Mlidhani wamelala mkateta mbele yao,
    Mkadhani ni watoto mkasema mbele yao!
    Wamewasikia mkipanga mniue, eti mkate kauli, mzibe mdomo, ikibidi kwa kufuri, kama bado kiburi apewe nauli, arudi kwao Sumbawanga!
    Walipowauliza nyie, bila haya mkajibu,
    Eti anatusema wala rushwa na sisi tumezoea,
    Anauponda ufisadi na huo ni mradi wetu eeh,
    Anatuvunjia heshima na sisi ni wanadini eeh,
    Kwarezma tunafunga sie, Ramadhani tunafunga sie!
    Anaingilia maisha ya watu,
    Hiyo sio tabia ya watanzania,
    Kwanza tuna mashaka na uraia wake eeh!
    Na kuanzia leo ni marufuku radio yoyote kupiga nyimbo zake,
    Kiisaa anaimba ukweli eeh!
    Wewe Nahodha x2
    Shusha tanga pepo zime chachamaa!
    Nanyi abiria pigeni mbizi,
    Muwezavyo chombo kimechota maji!
    Haya wanafiki, vishuka,
    Nipeni leo hilo jina baya mniue!
    Msoitakia mema nchi yangu,
    Nipeni leo hilo jina baya mniue!
    Rushwa inakunyonya wewe mwananchi eeh!
    Ufisadi unakubonda wewe Mtanzania!
    Nataka kukuokoa unanigeuka!
    Wee jirani wewe, jirani yangu wewe!
    Nyumba yako inachomwa, unapiga kelele,
    “naona moto, naona moto” mi nnakuja kukusaidia,
    unaona wanao wanateketea bila haya unaguna
    eti “aah, kumbe taka za shimo tu zachomwa!”
    Muheshimiwa rais naomba kijembe mi nikalimie mpunga,
    Nnashamba kubwa linafika darisalama!
    Waheshimiwa wabunge nipeni vijembe vingi mi nikalimie mpunga,
    Nina shamba kubwa linafika Dodoma,
    Maembe Maembe mie, ng’ombe mwana yatima,
    Wacha nikimbie niponye wangu mtima,
    Ugali sinia zima waisha kwa yangu nyama,
    Ngozi yangu ndio njema kwa kuziwambia ngoma,
    Ikipigwa bagamoyo dunia nzima yavuma,
    Dunia nzima yavuma mama!
    Rushwa imepewa heshima!
    Ufisadi umesimama wima!
    Nami siwezi nyamaza kimya!
    Nchi inaangamia vijana tunaangalia!
    Nchi inateketea wasomi tunachekelea!
    Watu wa nchini kwangu eeh,
    Watanzania wenzangu tusijipake mavumbi,
    Mkole kuwa mwembeni sio kukosa ukumbi,
    Mijahazi imevunjika sembuse sie mitumbwi!
    Itakuwa sie mitumbwi!
    Wewe nahodha x2
    Shusha tanga pepo zime chachamaa!
    Nanyi abiria pigeni mbizi,
    Muwezavyo chombo kimechota maji!
    Haya wanafiki, vishuka,
    Nipeni leo hilo jina baya mniue!
    Msoitakia mema nchi yangu,
    Nipeni leo hilo jina baya mniue!
    #Nahodha
    #VitaliMaembe
    #Kaizari
    Copyright @ Motokaa Muziki

ความคิดเห็น • 24

  • @mukakathejoker6504
    @mukakathejoker6504 7 หลายเดือนก่อน +1

    The song song will always remind me of my back home (Chalinze -pwani Tanzania) .

  • @kissjohantho617
    @kissjohantho617 ปีที่แล้ว +3

    Daaah!!...braza Mungu akubariki daima.,unasema ukweli, unaelimisha, unaburudisha..hii maan halisi ya MwanaMuziki🔥🔥

  • @tonyspencer1928
    @tonyspencer1928 2 ปีที่แล้ว +4

    Unatamani wimbo usiishe unaburudika na kuelimika

  • @suleimankeya3592
    @suleimankeya3592 ปีที่แล้ว +3

    Congratulations kiongozi as an Activist Kenya am really appreciate your efforts towards corruption and Justice.

  • @abuuzainabukhalifa592
    @abuuzainabukhalifa592 8 หลายเดือนก่อน +1

    Nakupenda sana Kaka....

  • @bossjoetv2745
    @bossjoetv2745 2 ปีที่แล้ว +3

    Aisee mwafrika wa kwanza ni wewe bwana maembe vitali

  • @JuergenWStork
    @JuergenWStork 5 หลายเดือนก่อน +1

    ❤❤❤❤❤

  • @King_Of_Everything
    @King_Of_Everything 9 หลายเดือนก่อน +1

    🇹🇿🇹🇿🇹🇿✌*

  • @annasamwel1463
    @annasamwel1463 ปีที่แล้ว +2

    Hongera sana kaka Maembe.

  • @user-ue1ho2hz3u
    @user-ue1ho2hz3u ปีที่แล้ว +1

    Nzuri sana Iko poa

  • @jamesyohana12
    @jamesyohana12 ปีที่แล้ว +2

    Great

  • @ejtjr2647
    @ejtjr2647 2 ปีที่แล้ว +2

    Maana halisi ya sanaa, fasihi inayoburudisha, kuonya na kufundisha.

  • @edwinfelix6298
    @edwinfelix6298 2 ปีที่แล้ว +2

    RIP JPM

  • @PAZZY42
    @PAZZY42 ปีที่แล้ว +1

    Kazi NZURI SANAA

  • @badilusalummanzi1187
    @badilusalummanzi1187 ปีที่แล้ว +1

    Kazi zako nzuri kaka

  • @hamisjuma287
    @hamisjuma287 ปีที่แล้ว +1

    Safi sana

  • @davidmapogo3048
    @davidmapogo3048 2 ปีที่แล้ว +2

    Nakuelewa

  • @happinessmtani7621
    @happinessmtani7621 2 ปีที่แล้ว +1

    Hongera kwa kazi nzuri Maembe

  • @mambopoa0170
    @mambopoa0170 2 ปีที่แล้ว +1

    ....kazi nzuri

  • @deusmwando5706
    @deusmwando5706 2 ปีที่แล้ว +1

    I do it kaka

  • @sammabula7359
    @sammabula7359 2 ปีที่แล้ว +1

    Nakubali sanaa