SERIKALI YASITISHA UKAGUZI WA RISITI ZA EFD KARIAKOO

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 23 มิ.ย. 2024
  • DODOMA: SERIKALI imesitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia Mkoa wa kikodi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam, wakati ukiandaliwa utaratibu mzuri wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo.
    Hayo yamesemwa naWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo kwa niaba ya Serikali mkoani Dodoma leo wakati akitoa maazimio ya kikao kati ya viongozi wa wafanyabiashara Tanzania, viongozi wa wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara.
    KIkao hicho ambacho kiliitishwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) kilihudhuriwa pia na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.
    Imeandaliwa na Mwandishi Wetu
    Follow us on:
    FACEBOOK;
    SpotiLeo: / spotileo-176. .
    HabariLeo: / habarileo
    DailyNews: / dailynewstz
    INSTAGRAM;
    HabariLeo: habarileo_tz?ig...
    SpotiLeo: spotileo?igshid...
    TWITTER;
    Twitter HabariLeo: HabariLeo?s=09
  • กีฬา

ความคิดเห็น •