UZALISHAJI MAGARI YA UMEME UGANDA, MCHONGO TANZANIA

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 10 ก.ย. 2024
  • Wakati Uganda ikifungua kiwanda kutengeneza magari ya umeme, wadau wameeleza kuwa hatua hiyo ni fursa kwa nchi jirani ikiwemo Tanzania kupunguza matumizi ya fedha za kigeni zinazotumika kuagiza mafuta kila mara.
    Kiwanda hicho kwa kwanza Afrika kuzalisha magari ya umeme, Kiira Motors Coorporation (KMC), kinatarajiwa kuzalisha magari 5,000 kwa mwaka yatakayohusisha magari mabasi madogo ya abiria na yale ya masafa marefu.
    Takwimu zinaonyesha Tanzania kwa mwaka Tanzania hutumia wastani wa lita bilioni 4 za mafuta ambazo gharama yake hubadilika mara kwa mara kutokana na kupanda kwa thamani ya dola na gharama za usafirishaji.
    Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), Joseph Priscus amesema kuanzishwa kwa kiwanda hicho ni hatua kubwa katika biashara ya usafirishaji na utekelezaji wake utakuwa na manufaa pia kwa nchi.
    Akizungumza leo Agosti 16, 2024 wakati wa ufunguzi wa kiwanda hicho sambamba na maonesho ya vyombo vya moto vinavyotumia umeme, Priscus amesema endapo teknolojia ya magari ya umeme itashika kasi, itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za uendeshaji na nchi itapata mapato yatokanayo na mauzo ya umeme.
    Amesema Tanzania inatumia kiasi kikubwa cha fedha za kigeni kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi hivyo endapo magari ya umeme yataanza kutumika, fedha hizo zitabaki nchini kwa ajili ya matumizi mengine.
    Amesema kwa muda mrefu kumekuwa na mabadiliko katika bei za mafuta, hali inayosababisha kuyumbisha biashara ya usafirishaji, hivyo teknolojia ya gesi na umeme ni mkombozi.
    “Hiki kiwanda kipo Uganda lakini sisi kama nchi jirani naona tunaweza kuitumia fursa hii na kupata manufaa. Kama nchi tunatumia fedha nyingi kuagiza mafuta lakini tukiwa na magari haya, hatuna sababu ya kutumia fedha hizo kwa sababu umeme tunao.
    “Tunaona hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha tunakuwa na umeme wa uhakika, ikiwemo ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, hivyo nishati ya umeme tunayo ya kutosha kwa ajili ya magari haya,” amesema Priscus na kuongeza:
    “Mbali na faida ambazo Serikali itapata kupitia mauzo ya umeme, kwa upande wetu wafanyabiashara magari haya yatapunguza gharama za uendeshaji kwa kuwa teknolojia hii haina matumizi makubwa ya vilainishi wala matengenezo ya mara kwa mara.”
    Mkurugenzi Mkuu wa Kiira Motors, Paul Musasizi amesema Serikali ya Uganda imetumia dola 85 milioni (Sh230 bilioni) kufanya uwekezaji huo unaoenda kuifanya kuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki na kati kuwa kiwanda cha kutengeneza magari ya umeme.
    Amesema tayari kiwanda hicho kimeshazalisha magari 40 ambayo yameanza kutoa huduma ya kubeba abiria katika miji ya Entebe, Jinja na Kampala.
    Amesema mpango wa kuwa na kiwanda hicho ulianza 2007 kwa kupeleka wataalamu nje kujifunza tekinolojia hiyo na hatimaye waliweza kutengeneza magari hayo nchini Uganda kupitia kiwanda kidogo, kabla ya kuanzisha kiwanda kikubwa ambacho kitazinduliwa Oktoba mwaka huu.

ความคิดเห็น • 12

  • @allykassim1120
    @allykassim1120 25 วันที่ผ่านมา

    big up uganda!

  • @edwinalexander1170
    @edwinalexander1170 25 วันที่ผ่านมา +1

    Kwa hiyo ni jambo la kufurahia kwamba miaka michache ijayo Uganda itakuwa inatuuzia magari? Kwanini tusitengeneze na sisi kiwanda chetu? Wao wameweza sisi tunashindwaje?

  • @emmanueltillya2017
    @emmanueltillya2017 25 วันที่ผ่านมา +1

    Mbona uwekezeji wake ni hela ndogo sana kwa Tanzania.haifiki hata bilioni 500.nchi yetu haijataka tuu kuamua.mimi nilijua ni matrilion ya pesa.

    • @amanijampion3045
      @amanijampion3045 24 วันที่ผ่านมา

      Sio lazima Tz nayo izalishe magari. Tungekuwa na akili ni kujenga reli za zaidi kila korido na ruti mpya

  • @mmarandu2417
    @mmarandu2417 25 วันที่ผ่านมา +1

    Hatuwezi kuzalisha hayo magari Tanzania? Tunahitaji Magufuli mwingine aanzishe magari ya umeme mijini na kiwanda kama hicho Tanzania.

  • @Fidia-ie3fi
    @Fidia-ie3fi 26 วันที่ผ่านมา

    Nawzfata sana wangu ni docta sule allhaj pa mwenga kamituga

  • @fidelfidel-jz4iw
    @fidelfidel-jz4iw 25 วันที่ผ่านมา

    Hakika serikali inunue magari ya umeme ione faida yake hasa utumiaji wa mafuta

  • @omarybakunda2554
    @omarybakunda2554 25 วันที่ผ่านมา

    Bora mafuta yamekua yakiumiza watu sana

  • @phare_tz
    @phare_tz 25 วันที่ผ่านมา +1

    Sisi nchi yetu bado inaongelea matundu ya choo wakati tunapaswa kukimbilia soko la technology sasa wanataka watu wasomi sasa hawaoni uganda jmn

  • @abuuramadhan8093
    @abuuramadhan8093 25 วันที่ผ่านมา +1

    Tanzania hata baiskael bado hatujaweza kutengeneza

    • @mosesnyelo1380
      @mosesnyelo1380 25 วันที่ผ่านมา

      Wew ndo huwez kutengeneza