MTOTO ALIETUPWA KWENYE KATANI ASAIDIWA NA MASHABIKI WA YANGA MASUMBWE APEWA JINA LA ALLY KAMWE.

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 15 ธ.ค. 2024
  • Mtoto Musa Masala Alietupwa akiwa na siku 3 baada ya Kuokotwa na Ndugu.MARY LUMAMBO amesaidiwa na Shabiki wa timu ya Yanga SC Masumbwe Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita Ndugu REVOCATUS TANGAJO ambae pia ni Katibu hamasa na Chipukizi UVCCM Wilaya ya Mbogwe.
    REVOCATUS amemhakikishia mama huyo kulipia gharama za usafiri Kila atakapokuwa akifata maziwa Mkoani Geita kwaajili ya kufata maziwa ya mtoto huyo.
    Wakizungumza MASHABIKI wa YANGA SC Masumbwe wamesikitishwa na kulaani Kitendo Kilichofanyika na mama mzazi aliemtupa mtoto Musa masala kwenye katani Akiwa na siku Tatu baada ya kuzaliwa. MASHABIKI hao Wamembatiza jina la Ally Kamwe ambae ni msemaji wa timu ya YANGA SC Ili kuenzi Siku Ya Yanga Day iliyowakutanisha na mtoto huyo.
    Hata hivyo Mama Mlezi wa Musa masala ambae ni Mary Lumambo amewashukuru MASHABIKI wa YANGA kwa msaada wao huku akiomba wadau na viongozi Mbalimbali wa serikali kumsadia jukumu la Malezi ya mtoto huyo ikiwa ni pamoja na Nauli na matumizi ya mtoto.
    Amesema alimuokota mtoto huyo Mtaa wa Nyambogo, iliyoko kata ya Nyakafulu Wilaya ya Mbogwe akiwa ametupwa katika katani Akiwa na siku Tatu ambapo Hadi Sasa mtoto huyo ana umri wa miezi 9 na mama huyo anamlea kama mtoto wake na epewa jina la MUSA MASALA jina la Baba wa Mme wake baada ya kuruhusiwa na serikali kuwa umiliki Rasmi wa Mtoto na kutoa idhini kutumia ubini wake amletee kama mtoto wake.
    #mbogweupdates #mfianchi

ความคิดเห็น • 2

  • @neemakageye
    @neemakageye 4 หลายเดือนก่อน +1

    aliye 2pa mtoto Mungu amlaani kabisaa wengne wanawatafuta kwa dawa yeye ana2pa