PRAISE & WORSHIP TEAM FPCT MAJENGO MOSHI (🎼 BWANA WEE UU MWEMA)26/05/2024.

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 11 ก.ย. 2024
  • (📖 ZABURI 136 : 1 - 25 SRUV)
    Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni Bwana wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyeumba mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyeumba mianga mikubwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Jua litawale mchana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wao wa kwanza; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akawavusha Israeli katikati yake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyewapiga wafalme wakuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akawaua wafalme mashuhuri; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Sihoni, mfalme wa Waamori; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Na Ogu, mfalme wa Bashani; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akaitoa nchi yao iwe urithi; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Urithi wa Israeli mtumishi wake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Aliyetukumbuka katika unyonge wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akatuokoa na watesi wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye akipaye kila kiumbe chakula chake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

ความคิดเห็น • 2

  • @IsackDominiko_
    @IsackDominiko_ 3 หลายเดือนก่อน +2

    Psalm 107:1
    [1]O GIVE thanks to the Lord, for He is good; for His mercy and loving-kindness endure forever!
    For a Few or Many Reasons God is to be Glorified and Let Men Sing of His Glory for he's the God Almighty who reigns above all things.
    Thank You God, Thanks Jesus! 🙌