JERRY SILAA AAGIZA KUKAMATWA KWA BAKARI GONGO LA MBOTO

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 11 ก.ย. 2024
  • Jeshi la Polisi nchini kupitia kituo cha Polisi Gongo la Mboto limeagizwa kumkamata Bakari Shingo na wenzie akiwemo msimamizi wa eneo la maegesho ya Bajaji lililopo mtaa wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, kwa kudaiwa kusababisha migogoro.
    Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye eneo hilo baada ya kuwepo mgogoro huo ambao umezua taharuki hasa kwa Madereva bajaji waliokuwa wakifanya kazi eneo hilo baada ya kutolewa katika eneo hilo na anayedai kuwa ndiye Mmiliki.
    Aidha Silaa amemtaka pia Mkuu wa Mipango Miji Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kumilikisha eneo hilo la maegesho ya bajaji kwa Mkurugenzi wa Jiji na kumtaka aweke utaratibu mzuri wa malipo kwa Madereva waliokuwa waki-park eneo hilo ikiwemo kuwapunguzia ushuru kutoka Tsh. 2500 waliyokuwa wakilipa awali hadi kufikia Tsh. 1000.
    #eastafricatv
    Karibu kujiunga na group letu la What's app kwa Habari, Matukio, Burudani
    BONYEZA LINK 👉👉 chat.whatsapp....
    Subscribe hapa : bit.ly/2UBtyaG
    Tufuate Kwenye Twitter : bit.ly/2UFkrWH
    Like Ukurasa wetu wa Facebook : bit.ly/2XbYro5

ความคิดเห็น • 5

  • @kivatirokitojo657
    @kivatirokitojo657 4 หลายเดือนก่อน +1

    Waziri Jerry 😂😂 eti shekhee huko unkoenda utaharakisha jambo 😂😂 kweli Huyu jamaa mtoto wa Mjini kiongozi lazima awe Kama Huyu waziri

  • @user-oh6pc7zd4s
    @user-oh6pc7zd4s 6 หลายเดือนก่อน

    FIDDA. HUSSEIN NI MWIZI EA ARDHI ZA WATU

  • @thomastemu3332
    @thomastemu3332 6 หลายเดือนก่อน

    Tapeli jeuri 😅😅😅

  • @thomastemu3332
    @thomastemu3332 6 หลายเดือนก่อน

    Shingo ni mjeuri 😅😅😅😅

  • @mustaphersamson6174
    @mustaphersamson6174 6 หลายเดือนก่อน

    KIVULI CHA MAGUFULI KIMERUDI, PAMBANA MH WAZIRI, LAKN UWE MUANGALIFU, NA MWENYEZI MUNGU AKULINDE.