UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA MSALATO WAFIKIA ASILIMIA 72

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 15 ก.ย. 2024
  • Kamati ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar imeridhishwa na Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato jijini Dodoma ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 72 kwenye Barabara ya kuruka na kutua ndege huku Jengo la abiria likifikia asilimia 39.
    Hayo yamesemwa Agosti 30, 2024 na Msimamizi wa Mradi, Mahona Luhende wakati akitoa maelezo kwa kamati hiyo ilipotembelea mradi wa Ujenzi wa kiwanja hicho ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa ziara ya kutembelea miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
    Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Yahya Rashid Abdullah ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea na Ujenzi wa miradi ya Kimkakati inayotoa taswira ya Nchi Kimataifa ambayo inatekelezwa kwa matumizi ya muda mrefu.

ความคิดเห็น • 3

  • @mduda_i
    @mduda_i 16 วันที่ผ่านมา +1

    👏

  • @Ali-nl2du
    @Ali-nl2du 15 วันที่ผ่านมา

    Hili neno 'lakini' siku hizi linatumiwa sehemu siyo stahiki. Mara nyingi linatumiwa kwa kukusudia 'na', 'pia', 'vilevile' au 'aidha'. Tatizo la kuiga iga ndio inakuwa kama hivi. Chunguza kwanza halafu ndio uige, panapostahiki. Lugha siyo fashion.

    • @rayisadesigns2646
      @rayisadesigns2646 14 วันที่ผ่านมา

      Hao ndiyo waharibifu wa lugha, hayo wanayapata kutoka kwa wanasiasa na kwa baadhi ya viongozi wa dini flani wanaongiza manjonjo yao kwenye lugha kumbe ndiyo wanaharibu pasi na wao eidha kwa kujua au kutojua.