Salama Na DULLA Ep 39 | GO HARD OR GO HOME... Part 1

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 22 ม.ค. 2025
  • #SalamaNa #SendTip #0762797291
    You Can support US through anchor.fm/yahs...
    SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
    Listen our Podcast on
    Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
    ‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
    GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
    Audiomack Link bit.ly/YahSton...
    ‪TH-cam Link bit.ly/TH-camS...
    Abdallah Khamis Ambua ndo jina halisi toka kwa wazazi wake ambao hawana asili ya kisiwani wala kuwahi kuishi huko kwa muda mrefu ambako pengine ndo kukamuwezesha kupata hiyo lafdhi. Kabla hatujafika kokote kwa kuskia kutoka kwangu, ningepeda ufahamu kwamba mimi si mmoja ya watu walotaka Dulla apewe kipindi cha Planet Bongo mwaka 2018 wakati naenda zangu Cardiff kushangaa kondoo, na moja ya sababu zangu kubwa ilikua yeye kutokua na lafdhi nzuri ya maneno kwenye lugha yetu adhimu ya Kiswahili. Na hilo nililiweka wazi haswa. Lakini pia nilikubaliana na matokeo baada ya viongozi kuamua kumpitisha yeye, na kwa heshima zote leo napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza kwa kazi nzuri waliyoifanya, kwa kuona kijana ambaye alikua na utayari kwa kujifunza, wa kujua kwamba alikua hajakamilika na mlango ukawa wazi kwake kutaka kujifunza na kuwa bora.
    Tupeleke miaka mbele mpaka 2020, ingawa hapo nyuma tushakutana mara kadhaa na nikamuambia jinsi ambavyo ananifurahisha kwa kukuwa kwake na kwamba mimi ni mmoja wa watu wanao jivunia yeye. Na hata wakati tunafanya maongezi yetu haya, nilimfahamisha pia. Mwanzo wakati naanza kuandika nilianza kwa kukuambia kuhusu asili yake, sababu ilikua ni juu ya lafdhi yake ya kimwambao ilonyooka haswa. Mimi wakati nakutana na Dulla kwa mara ya kwanza kwenye usaili hakua na hiyo accent, alikua na matatizo ya R na L na pia hakua ‘original’, alikua ana tangaza na kuongea kama B Dozen, ambaye tayari alikua amesha ji establish vizuri tu na anga yote alikua anaunguruma yeye mara ifikapo saa nane kamili ya mchana. So kama mtangazaji mpya anayechipukia, Dulla hakua na nafasi ya kuweza kutamba mbele ya Dozen, na wala hakua na uwezo wa hata robo yake. Kwa yeye kutoboa na kuweka alama yake ilikua inambidi awe YEYE na aje na ladha YAKE.
    Leo hii, mimi na enjoy haswa ninapomsikiliza Mjukuu wa Ambua radioni, sauti tamu, matamshi yamenyooka, ladha ya maneno inatulia maskioni, hapayukwi kwenye kipaza sauti na pia kubwa kuliko yote ana akili, akili ya kusema na kuuliza maswali muafaka na muda muafaka. Na kwa hilo namheshimu.
    Basi nikataka kujua vile alijiskia alipong’amua kama mimi sikua shabiki yake hata kidogo? Na Kama ilimtoa katika ‘mchezo?’. Wakati mshindi wa mtangazaji mpya wa Planet Bongo anatangazwa tayari Mimi nilikua nishafika zangu Cardiff kwahiyo sikuwahi kuongea nae tena kuhusu uchaguzi wake na wala maendeleo yake kwahiyo hii imekua mara ya kwanza tuna discuss. Pia nilitaka kujua kuhusu mke wake, watoto, Kaka yake ambaye naye ndo alimfanya kwa kiasi kikubwa achague kazi hii anayofanya sasa. Pia kuhusu mahusiano yake na Diamond Platnumz na Ali Kiba, muziki wa Bongo Flava kwa ujumla. Kazi, mapenzi, ujana, dini na yeye kama binadamu. Haya yalikua maongezi flani ya kikubwa ambayo nimefurahi tuliyafanya mimi na mdogo wangu huyu.
    Kama kawaida, yangu matumaini hii pia itakufunza jambo, itakutaka uwe bora na kutokubali kushidwa hata kama ulokua unapenda sana akupe sapoti akawa haamini juu ya uwezo wako, hiyo ndo iwe chachu ya wewe kutaka kufanya vyema zaidi.
    Love,
    Salama
    Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
    Follow:
    Twitter: / yahstonetown
    Instagram: / yahstonetown
    Facebook: / yahstonetown

ความคิดเห็น • 145

  • @mozasaid3869
    @mozasaid3869 4 ปีที่แล้ว +14

    Mashaallah Dullah unaongea kiswahili kizuri sana, Sauti yako inakuja km Charles Hilary

  • @aishahussein3879
    @aishahussein3879 4 ปีที่แล้ว +7

    Kweliiiii, nimepata experience kubwa sana kupitia ww na nyota njema huonekana asubuhi coz tangu tupo p/r ulikua unahii kitu Dee wote tuliosoma wote shule ya msingi kipindi kile tunalijua hili, big up sana Allah azidi kukufungulia zaid na zaidi my classmate 💝

  • @islandgirl4578
    @islandgirl4578 4 ปีที่แล้ว +2

    Nampenda Sana dulla nakumbuka Nilikua 4m4 natoroka vipind vya jion niwah kutizama kwanjika mkwanja ya EATV2016

  • @fatmasalim8122
    @fatmasalim8122 4 ปีที่แล้ว +14

    I wish siku atokee mtu akuhoji wewe salama ili tujue story yako na wewe, ili tupate kukujua zaidi.....big up, huge fan of your work 😊

    • @WASHATube
      @WASHATube 4 ปีที่แล้ว

      TOP 10: WAREMBO WA INSTAGRAM WALIO-TREND ZAIDI 2020👇👇👇
      th-cam.com/video/mJ5_G0bF-uw/w-d-xo.html
      NI UPDATE AMAIZING🔥🔥🔥🔥

    • @goodluckjulius3258
      @goodluckjulius3258 4 ปีที่แล้ว

      Role model wangu

    • @allyarmanou3549
      @allyarmanou3549 4 ปีที่แล้ว

      Iko interview alifanyiwa na Lil ommy akiwa times fm, go check it out

  • @blandinamnyinga8318
    @blandinamnyinga8318 4 ปีที่แล้ว +12

    Salama I love your honesty on point,mimi nilikuwa mmoja kati ya watu ambao hawakutaka wewe upate ile kazi""nice one""

    • @WASHATube
      @WASHATube 4 ปีที่แล้ว

      TOP 10: WAREMBO WA INSTAGRAM WALIO-TREND ZAIDI 2020👇👇👇
      th-cam.com/video/mJ5_G0bF-uw/w-d-xo.html
      NI UPDATE AMAIZING🔥🔥🔥🔥

  • @blandinamnyinga8318
    @blandinamnyinga8318 4 ปีที่แล้ว +7

    I love and enjoy seeing dula grow cause I was a fan since planet bongo star search.nakumbuka cku ya kutangazwa mshindi alivaa sendo zake flani simpoooo.

    • @lulumoses2130
      @lulumoses2130 4 ปีที่แล้ว

      Na ndo siku ya kwanza ulichezwa sana wimbo wa ngweir nipeni dili na ukavuma kupitia hii siku

    • @blandinamnyinga8318
      @blandinamnyinga8318 4 ปีที่แล้ว

      @@lulumoses2130 yaa!!👌

  • @ms_caramel2688
    @ms_caramel2688 4 ปีที่แล้ว +5

    Nmependa hyoo kaka anavoongea jmn mashaAllah anaonekana mstaarabu sana

  • @fra_nyuki
    @fra_nyuki 4 ปีที่แล้ว +12

    Two talents facing each other... So much to learn...

    • @emariusrush3285
      @emariusrush3285 4 ปีที่แล้ว

      Salama is talented,the isn't!!!.

  • @aminanamoyo83
    @aminanamoyo83 4 ปีที่แล้ว +13

    Nampenda dullah, nimefurahi kumuona sauti yake mimi hoi,hana skendo thanks Salama ❤

  • @ashasiaga3197
    @ashasiaga3197 4 ปีที่แล้ว +1

    Nimependa sana salama hongera sana dulla yupo vizur kajielezea vya kutosha

  • @wanzakleruu
    @wanzakleruu 4 ปีที่แล้ว +2

    Ombi langu kwenu Salama na team yako. Mimi km shabiki no1 wa hii show yetu hii pedwa. Tuleteeni Mussa Hussein na Sky wa sns🙏🙏🙏

  • @hamambuka5616
    @hamambuka5616 4 ปีที่แล้ว +3

    Kazi nzuri Salama na Dullah.Love from 254

  • @didahbebe3866
    @didahbebe3866 2 ปีที่แล้ว

    Kwakweli salama unatulisha madini mazuri love you so much darling

  • @annaonesmo1934
    @annaonesmo1934 4 ปีที่แล้ว +1

    Uko vizuri sana Dada angu mm nishabiki yako no. Moja

  • @nasraiddy9678
    @nasraiddy9678 4 ปีที่แล้ว

    Dullah mashallah unarafudhi nzuri yaan kama nasikiliza BBC swahili Wale watangazaji wake

  • @salometz9572
    @salometz9572 4 ปีที่แล้ว

    I love him the way he is kuanzia utangazaji wake kipindi chake and everything😘

  • @saudatkiuta5060
    @saudatkiuta5060 4 ปีที่แล้ว +4

    Watangazaj watatu ambao nawakubal pamoja na mjukuu dula na zamarad na salama

  • @stephanokigosi656
    @stephanokigosi656 4 ปีที่แล้ว +13

    dulla, mtangazaji wangu no moko wapili ni MILLARD Ayo

  • @sherrysalim50
    @sherrysalim50 4 ปีที่แล้ว +1

    Watu wa pwani tuna kiswahili kitamuuuuuuuuuuu 🤩🤩

  • @deusntobi1450
    @deusntobi1450 4 ปีที่แล้ว +4

    Nafatiliaga lakini huwa sicoment ila leo nimefrahia sana. Ninyi watu mnakunywa nn muagize nami nitawalipia

  • @edwinmbugua7738
    @edwinmbugua7738 4 ปีที่แล้ว +6

    Kipindi hicho Dulla kwenye Planet Bongo ndani ya eatv.. young d kapiga promo moja kali ya hiyo show

  • @ujudiabdull9442
    @ujudiabdull9442 4 ปีที่แล้ว +3

    Salama yani leo apo mlivoua gemu mpk mnakera...misichoki kukupenda Salama hata watu wote wakuchukie hahaaa

  • @khaulatmohammed3765
    @khaulatmohammed3765 4 ปีที่แล้ว +2

    Dula mwenye udula wake💓💓

  • @queenseptember4640
    @queenseptember4640 4 ปีที่แล้ว +21

    Salama na Millard Ayo, hiyo siku nitawanunulia Kvant wote humu ndani,
    😄😄

  • @nalipodaud4493
    @nalipodaud4493 4 ปีที่แล้ว +2

    Fireeee

  • @michaellagwen8198
    @michaellagwen8198 4 ปีที่แล้ว +12

    Wa kwanza Leo kwenye kipindi chetu cha stone town please like hata kumi tu🤛🤙

    • @magangakayola4175
      @magangakayola4175 4 ปีที่แล้ว

      Kwa hiyo kama wa kwanza tukufanyaje ssa?

    • @ujudiabdull9442
      @ujudiabdull9442 4 ปีที่แล้ว

      @@magangakayola4175 hahaaa nimecheka kifala ..

    • @WASHATube
      @WASHATube 4 ปีที่แล้ว

      TOP 10: WAREMBO WA INSTAGRAM WALIO-TREND ZAIDI 2020👇👇👇
      th-cam.com/video/mJ5_G0bF-uw/w-d-xo.html
      NI UPDATE AMAIZING🔥🔥🔥🔥🔥

    • @samoocoolingsystem93
      @samoocoolingsystem93 4 ปีที่แล้ว

      Tafadhali tembelea chaneli yangu

  • @barakabahati4315
    @barakabahati4315 4 ปีที่แล้ว +1

    Salama na jembe ni jembe was agreat interview naicheki kila siku

  • @georgeludakulo6848
    @georgeludakulo6848 4 ปีที่แล้ว +3

    Salama Jabir tuletee @jonijoo itakuwa pow xn

  • @shanishosho911
    @shanishosho911 4 ปีที่แล้ว +1

    Dullah kama dullah😍💕

  • @saumuhassan6365
    @saumuhassan6365 4 ปีที่แล้ว +2

    Mashallah, Interview ya kizazi sana, good job salama, nime enjoy sana 😘👍

  • @telengoboy
    @telengoboy 4 ปีที่แล้ว +3

    Sio PRANET bongo, ni PLANET bongo.. 😂😂😂, dah mwana alikuvumilia Salama

  • @mwajabumasawanga4662
    @mwajabumasawanga4662 4 ปีที่แล้ว +5

    Such a good voice

    • @WASHATube
      @WASHATube 4 ปีที่แล้ว

      TOP 10: WAREMBO WA INSTAGRAM WALIO-TREND ZAIDI 2020👇👇👇
      th-cam.com/video/mJ5_G0bF-uw/w-d-xo.html
      NI UPDATE AMAIZING🔥🔥🔥🔥

  • @najma3268
    @najma3268 4 ปีที่แล้ว +3

    Dullah nimekupenda bure, matamshi,hekma, busara mashaallah

  • @attemptenacity8735
    @attemptenacity8735 4 ปีที่แล้ว +1

    Mawazo Ya bure: I think it is very possible for the government to allow the current presenters and journalists to take a night time course or rather a journalism exam that makes it eligible for all of the 'non' qualified to be legit. It is very doable!

  • @tumatijr_9142
    @tumatijr_9142 4 ปีที่แล้ว +11

    Acha nishare hili Hadith inasema huolewa mwanamke kwa Mambo manne
    1: dini yake
    2: nasaba yake(ukoo au familia)
    3: uzuri wake
    4: mali yake
    Ndo hivyo hapo ndugu zangu

    • @ginnimoreno6239
      @ginnimoreno6239 4 ปีที่แล้ว +1

      Huolewa (normally) mwanamke kwa mali yake nasabu yake na uzuri wake.. basi tafuta mwenye dini itatulizana mikono yako

    • @nasraiddy9678
      @nasraiddy9678 4 ปีที่แล้ว +1

      Na Mtume akatusisitizia uoeni wenye dini mtapata utulivu ndani ya majumba yenu

    • @rashidyjuma2195
      @rashidyjuma2195 4 ปีที่แล้ว

      @@nasraiddy9678 hakika

  • @damasshija6190
    @damasshija6190 4 ปีที่แล้ว +7

    Salama na B Dozen ije plz

  • @ginnimoreno6239
    @ginnimoreno6239 4 ปีที่แล้ว +1

    Bwana Abdullah

  • @enocksilungwepondajr9707
    @enocksilungwepondajr9707 4 ปีที่แล้ว +3

    Hajaelewa swali...

  • @khadejarajab8007
    @khadejarajab8007 4 ปีที่แล้ว +1

    Tunajifunza mengi kwenye intav zenu

  • @sleyyummalick9459
    @sleyyummalick9459 2 ปีที่แล้ว

    Pande znz upo sawa kaka

  • @ephrahimkamenge321
    @ephrahimkamenge321 4 ปีที่แล้ว +2

    ila jesca wa samaki samaki mmmh....aya bana salama....chakula chao kizuri

  • @vicentflavour9992
    @vicentflavour9992 4 ปีที่แล้ว +4

    Oooyeeah

    • @WASHATube
      @WASHATube 4 ปีที่แล้ว

      TOP 10: WAREMBO WA INSTAGRAM WALIO-TREND ZAIDI 2020👇👇👇
      th-cam.com/video/mJ5_G0bF-uw/w-d-xo.html
      NI UPDATE AMAIZING🔥🔥🔥🔥

  • @gtunewaves2867
    @gtunewaves2867 2 ปีที่แล้ว

    shida sio elimu shida mtu sahihi mwenye talent hii ishu ya utangazaji ukiondoa elimu kipaji ndo husimama zaidi sababu msikilizaji anavutiwa na uzungumzaji wa mtangazaji the way anaongea style yake elimu ni kwa ajili ya muongozo so huwezi mtoa millard ayo au dullah ambua arudi shule sababu hana diploma asee redio zitapoteza audience wengi sana na kiukweli wengi sana wenye elimu huwa hawana kitu yan talent

  • @abelyalexkagori9799
    @abelyalexkagori9799 4 ปีที่แล้ว

    Da sharapp MANGWAIR mnyamwezi san nkbl

  • @nadrasalim
    @nadrasalim 4 ปีที่แล้ว +4

    Huyu kaka napenda sauti yake

  • @samoocoolingsystem93
    @samoocoolingsystem93 4 ปีที่แล้ว +4

    Achia like kama umeona picha ya Baraka Mpenja kwenye ukuta like haiuzwi ni bure tu basi achia hiyo

  • @brokenigga2842
    @brokenigga2842 4 ปีที่แล้ว +1

    Jamaa lina voko ya maana

  • @makulerobert2916
    @makulerobert2916 4 ปีที่แล้ว

    sauti ya charles hilali kabisaaaa!

  • @alieththomas8505
    @alieththomas8505 4 ปีที่แล้ว +5

    Nice interview

    • @WASHATube
      @WASHATube 4 ปีที่แล้ว

      TOP 10: WAREMBO WA INSTAGRAM WALIO-TREND ZAIDI 2020👇👇👇
      th-cam.com/video/mJ5_G0bF-uw/w-d-xo.html
      NI UPDATE AMAIZING🔥🔥🔥🔥

  • @mbwanadavid4371
    @mbwanadavid4371 4 ปีที่แล้ว +1

    Namtaka Ally Choki mzee wa farasi

  • @asyamasoud2438
    @asyamasoud2438 4 ปีที่แล้ว +3

    Nampenda sn huyu dulla

    • @WASHATube
      @WASHATube 4 ปีที่แล้ว

      TOP 10: WAREMBO WA INSTAGRAM WALIO-TREND ZAIDI 2020👇👇👇
      th-cam.com/video/mJ5_G0bF-uw/w-d-xo.html
      NI UPDATE AMAIZING🔥🔥🔥🔥

  • @jacksonsawan9606
    @jacksonsawan9606 4 ปีที่แล้ว

    east Africa wanajua ejamaee wambua nakubali unachokifany

  • @makulerobert2916
    @makulerobert2916 4 ปีที่แล้ว

    jamaa namkubali mnooo aseee

  • @ingabireritha3740
    @ingabireritha3740 4 ปีที่แล้ว +1

    Very nice I like your choice woooh

  • @rahmajuma7410
    @rahmajuma7410 4 ปีที่แล้ว +3

    Dullah fanya mpango na ww umuhoji salama hapo hapo kwenye kiti chake

  • @hubertanthony7846
    @hubertanthony7846 4 ปีที่แล้ว +5

    Natamani sana nielewe mnachoongea ila tatizo mimi sielewi Kiswahili kabisa

  • @mr.performance2533
    @mr.performance2533 4 ปีที่แล้ว +4

    Dullah vry humble

    • @WASHATube
      @WASHATube 4 ปีที่แล้ว

      TOP 10: WAREMBO WA INSTAGRAM WALIO-TREND ZAIDI 2020👇👇👇
      th-cam.com/video/mJ5_G0bF-uw/w-d-xo.html
      NI UPDATE AMAIZING🔥🔥🔥🔥🔥

  • @mwahijalukali2387
    @mwahijalukali2387 4 ปีที่แล้ว

    Ambua kama ambua yaan nawapenda wewe na mkeo hatari chimiyna ni mzuriii jmn

  • @saumusalimuhassan2499
    @saumusalimuhassan2499 2 ปีที่แล้ว

    Interview imetulia hatariiii, nime Enjoy

  • @lareineminah1353
    @lareineminah1353 4 ปีที่แล้ว +5

    Iyo sheria inge chukuwa watu wenye wata ajiriwa baada ya sheria kuwekwa
    Sio walio ajiriwa kabla ya sheria husika

  • @winfridamdaki5699
    @winfridamdaki5699 4 ปีที่แล้ว +3

    Salama izo skafu ukimaliza kutumia unatupa? Mbona kila siku mnaweka zingine na mamrudii
    Tufanye biashara tuuze

  • @safiyatheonlything7848
    @safiyatheonlything7848 4 ปีที่แล้ว +4

    leo wa Kwanza like zenu hapa kwa salama kama unamkubali

    • @WASHATube
      @WASHATube 4 ปีที่แล้ว

      TOP 10: WAREMBO WA INSTAGRAM WALIO-TREND ZAIDI 2020👇👇👇
      th-cam.com/video/mJ5_G0bF-uw/w-d-xo.html
      NI UPDATE AMAIZING🔥🔥🔥🔥🔥

  • @augustinojonas2643
    @augustinojonas2643 4 ปีที่แล้ว

    Nikimuona Dulla Planet nahizi tupo kwenye dakika 10 za maangamizi

  • @stanleynorbert493
    @stanleynorbert493 4 ปีที่แล้ว +2

    me leo niko wa kwanza ku coment

    • @ghanimaali4507
      @ghanimaali4507 4 ปีที่แล้ว

      salama ana akili lkni mwehuuu ila nampenda kwakua binaadamu mwezangu

    • @ujudiabdull9442
      @ujudiabdull9442 4 ปีที่แล้ว

      @@ghanimaali4507 wehu wake nini he!

    • @ghanimaali4507
      @ghanimaali4507 4 ปีที่แล้ว

      @@ujudiabdull9442 jamani mawigi yke tu

    • @WASHATube
      @WASHATube 4 ปีที่แล้ว

      TOP 10: WAREMBO WA INSTAGRAM WALIO-TREND ZAIDI 2020👇👇👇
      th-cam.com/video/mJ5_G0bF-uw/w-d-xo.html
      NI UPDATE AMAIZING🔥🔥🔥🔥

  • @nasmafarmsltd9146
    @nasmafarmsltd9146 4 ปีที่แล้ว

    Mtu mwéńýë Bongo planet yake

  • @erickendrick3330
    @erickendrick3330 4 ปีที่แล้ว +3

    Kwann malume

    • @WASHATube
      @WASHATube 4 ปีที่แล้ว

      TOP 10: WAREMBO WA INSTAGRAM WALIO-TREND ZAIDI 2020👇👇👇
      th-cam.com/video/mJ5_G0bF-uw/w-d-xo.html
      NI UPDATE AMAIZING🔥🔥🔥🔥

  • @gildadeane1960
    @gildadeane1960 4 ปีที่แล้ว +1

    Salama naomba utuletee Ben Paul please

  • @nasmafarmsltd9146
    @nasmafarmsltd9146 4 ปีที่แล้ว

    Had leo waarabu wana chaguliwa

  • @facebmzeewakimba1546
    @facebmzeewakimba1546 4 ปีที่แล้ว +8

    Mlete NASH MC NEXT TIME

    • @ibrahimkanuto3514
      @ibrahimkanuto3514 4 ปีที่แล้ว

      Nash nilimpgia kasema hakanyagi media yoyote nw

    • @facebmzeewakimba1546
      @facebmzeewakimba1546 4 ปีที่แล้ว

      @@ibrahimkanuto3514 duuuh.basi poa pamoja mkush👊👊

    • @facebmzeewakimba1546
      @facebmzeewakimba1546 4 ปีที่แล้ว

      @@ibrahimkanuto3514 duuuh.basi poa pamoja mkush👊👊

  • @japhetbarton8268
    @japhetbarton8268 4 ปีที่แล้ว

    Kwan utaratibu wa kurasimisha ujuzi huku haufiki?

  • @BMT2023
    @BMT2023 4 ปีที่แล้ว

    Huyu jamaa kanifanya Ni subscribe hii Chanel baada ya kuuuona upande wapili unamlea zaidi.

  • @asiajuma8330
    @asiajuma8330 4 ปีที่แล้ว

    Salama uko vizuri ila punguza kingereza ongea kiswahili mwanzo mwisho usichanganye kiswanglish

  • @abdulfirst_pilot6479
    @abdulfirst_pilot6479 3 ปีที่แล้ว +1

    List ya watangazaji bora kwangu mimi ni
    Dullah planet
    Millardayo
    B dozen
    Jonijooo
    Sallam jabir
    Adam mchomvu
    Momy baby
    Kama na wewe una ikubali list hii tujuane

  • @franknganga5358
    @franknganga5358 4 ปีที่แล้ว +2

    Dah uchawi sielewi kiswahili tu

  • @lulumoses2130
    @lulumoses2130 4 ปีที่แล้ว +4

    Kabla sijaangalia hii leo jesika amebadirisha lile gauni lake la kitenge????

  • @salama2625
    @salama2625 4 ปีที่แล้ว +2

    Salama kumpa taarifa mke mkubwa kubwa unataka kuowa siyo lazima kumuambia

  • @khadijahali4837
    @khadijahali4837 4 ปีที่แล้ว

    Kipindi kitraaamu hd raha

  • @Bm_Mwakalobo
    @Bm_Mwakalobo 4 ปีที่แล้ว

    Dada salama Tutafutie Darasa tumuoji

  • @evelynmon6491
    @evelynmon6491 4 ปีที่แล้ว

    Kwani si uende tu shule ukachukue hiyo diploma dula au

  • @fahadalismaily9370
    @fahadalismaily9370 4 ปีที่แล้ว

    Fanya enterview na alikiba basi

  • @ajaxjunior4151
    @ajaxjunior4151 4 ปีที่แล้ว

    Ninaomba umletee na watangazaji wengine wengi kama Jonijoo na Millard Ayo tuendelee kupata madini zaidi au pia niendelee kupata madini zaidi kwani ninajifunza vitu vingi

  • @dizodi_vituko
    @dizodi_vituko 4 ปีที่แล้ว

    nyimbo ya daimond ineshindwa kwenda kisa mtaandao haupo th-cam.com/video/5LyZGBcW2UE/w-d-xo.html

  • @barakabahati4315
    @barakabahati4315 4 ปีที่แล้ว +3

    Salama na jembe ni jembe was agreat interview naicheki kila siku

  • @mwahijalukali2387
    @mwahijalukali2387 4 ปีที่แล้ว

    Ambua kama ambua yaan nawapenda wewe na mkeo hatari chimiyna ni mzuriii jmn