Live ▶|| Ibada Ya Morning Glory | 25 - 06 - 2024

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 23 มิ.ย. 2024
  • Karibu katika Ibada ya Masifu ya Asubuhi kutokea hapa kanisa Kuu Azania Front Posta Dar Es Salaam.
    ▶ SOMO: USIOGOPE VITA SI YAKO, VITA NI YA BWANA NA USHINDI NI HAKI YAKO.
    1 Samweli 16: 1 - 3
    .............................
    ZABURI 90: 12 - 17
    12 Basi, utufundishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima.
    13 Urudi, Ee BWANA utakasirika hadi lini? Wahurumie watumishi wako.
    14Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako, Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote.
    15 Utufurahishe kwa kadiri ya siku ulizotutesa, Miaka sawa na ile tuliyopatwa na maovu.
    16 Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako, Na utukufu wako kwa watoto wao.
    17 Na fadhili za BWANA, Mungu wetu, ziwe juu yetu, Na kazi ya mikono yetu uifanye thabiti, Naam, kazi ya mikono yetu uifanikishe.
    1 SAMWELI 17: 38 - 47
    38 Ndipo Sauli akamvika Daudi mavazi yake ya vita, akamtia chapeo cha shaba kichwani, akamvika dirii.
    39 Naye Daudi akajifunga upanga juu ya mavazi yake, akajaribu kwenda; maana alikuwa hajavijaribu. Daudi akamwambia Sauli, Siwezi kwenda na vitu hivi, maana sikuvijaribu. Basi Daudi akavivua.
    40 Akaichukua fimbo yake mkononi, akajichagulia mawe laini matano katika kijito cha maji, akayatia katika mfuko wa kichungaji aliokuwa nao, maana ni mkoba wake, na kombeo lake alikuwa nalo mkononi mwake, akamkaribia yule Mfilisti.
    41 Huyo Mfilisti naye akamsogelea Daudi na kumkaribia; na mtu yule aliyemchukulia ngao yake akamtangulia.
    42 Hata Mfilisti alipotazama huku na huku, akamwona Daudi akamdharau; kwa kuwa ni kijana tu mwekundu, tena ana sura nzuri.
    43 Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake.
    44 Mfilisti akamwambia Daudi, Njoo huku kwangu; nyama yako nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni.
    45 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la BWANA wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.
    46 Siku hii ya leo BWANA atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.
    47 Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba BWANA haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya BWANA, naye atawatia ninyi mikononi mwetu
    MiTHALI 12:1
    1 Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa; Bali yeye achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama.
    ▶ Mhubiri: Ev. Geofrey Simon Mbwambo
    .............
    👇👇👇
    // NAMBA ZA SADAKA //
    ▶ LIPA KWA [ M-PESA ] - 579 579 4
    ▶ NAMBA YA MPESA - 0757 - 391 - 174
    JINA: KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
    ▶ MAENDELEO BANK
    A/C NO 0137 9274 6021
    JINA: LUTHERAN CHURCH AZANIA FRONT CATHEDRAL
    TUFUATILIE KWENYE MITANDAO KWA TAHARIFA ZAIDI:
    Instagram page:
    / kkkt_azaniafront_cathedral
    Website: www.azaniafront.org/
    Facebook:
    / kkkt-azania-front-cathedral-101434162039079
    #azaniafrontcathedral #ibada #lunchhour #morningglory #sundayservice #lutheran

ความคิดเห็น •