MKONO WA MUNGU - PASTOR SUNBELLA KYANDO

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 6 ต.ค. 2024
  • Kuna gharama kubwa sana ya kuanzisha kitu ambacho Mungu amekiweka ndani yako.Mungu anachohitaji sio wewe upate hofu kutokana na ukubwa wa kitu alichokwambia bali anataka uchukue hatua ya Imani na uanze kufanya,ukianza tu na mkono wake unakuwa juu yako.Na kuna nyakati mkono wa Mungu unaweza kuwa juu yako lakini usijifunue,na hata ukimuuliza unaona amekaa kimya.Kukaa kimya kwa Mungu sio kuwa hayupo au hasikiki,anasikia na anatenda kazi.Meshaki,Shedraki na Abednego wakati wanakamatwa na kuingizwa kwenye tanuru la moto hauoni Mungu akisema chochote,lakini katika ule moto alikuwa nao na wala haukugusa hata nguo zao.Unachotakiwa kuwa na uhakika nacho ni kuwa katika kila hali unayopitia au utakayopitia Mungu yupo pamoja na wewe,hajakuacha na hatokuja kukuacha.
    #PastorSunbella#Mkono#Mungu .

ความคิดเห็น • 24