Vijana Mnakaribishwa katika kushiriki shughuli za kanisa-Askofu Jacob Mameo

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 1 ต.ค. 2024
  • Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania huonekana pia kung’ara katika uimbaji ndani ya ibada na pia katika wingi wa kwaya mbalimbali katika sharika na mitaa yake. Uimbaji kama sehemu ya ibada hufuata utaratibu na uchaji wa ibada. Sifa na shukrani ni kwa Mungu aliyeotesha punje ndogo ya haradali hadi kufikia kilele hiki cha kusherekea miaka sitini ya KKKT. Kanisa linaendelea kuwahimiza washarika wake kuendelea kutimiza wajibu wao kwa Bwana wao Yesu Kristo. Kwa kuzingatia tunu za Kanisa, washarika wanahimizwa kushiriki kikamilifu katika huduma zinazotolewa na Kanisa, huduma hizo ni Ibada ya neno na Sakramenti, elimu, afya, udiakonia, na huduma za kiuchumi.

ความคิดเห็น •