EQUITY BANK YANZINDUA MWANAMKE PLUS/ MIKOPO, BIMA, ELIMU YA BIASHARA

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 8 ก.ย. 2024
  • samiasuluhuhassan #wanawake
    Takwimu zimeonesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa Nchi yenye idadi ndogo ya wanawake wanaotumia teknolojia katika sekta ya fedha huku serikali ikichukua hatua mbalimbali ili kukabiliana na changamoto hiyo ikiwemo kuhamasisha matumizi ya pesa kidigitali.
    Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Waziri mwenye dhamana ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum Dkt Dorothy Gwajima wakati akizindua dirisha maalum la wanawake la benki ya Equity lililopewa jina la ‘’Mwanamke plus’’.
    Amesema dirisha hilo litasaidia kuleta uchechemuzi katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu na Biashara pamoja na kuongeza kuongeza uelewa kwa wanawake kuhusu ujumuishi wa kifedha na jinsi ya kukuza mitaji yao huku akitoa rai kwa benki hiyo kuleta huduma zinazomjumuisha mwanaume.
    Kwa upande wake mchumi kutoka benki ya maendeleo ya Afrika -AFDB, Prosper Charle amesema benki hiyo imeendelea kuweka kipaumbele kwa wanawake ili kuleta uhimilivu toshelezi wa uchumi pamoja na kung’amua fursa zilizopo katika
    Bi Isabela Maganga ni Mkurugenzi Mtendaji benki ya Equity amesema mahitaji ya mikopo kwa wanawake Nchini ni zaidi ya trilioni 4.4 ambapo kwa sasa hayajafikiwa na taasisi za kifedha hivyo dirisha la mwanamke plus itasaidia kuyafikia makundi hayo.
    Uzinduzi huo umehudhuriwa na wanawake zaidi ya 200 ili kufaham kazi ya dirisha hilo

ความคิดเห็น •