MABADILIKO MAKUBWA YA KIUCHUMI BAADA YA TIC KUSAINI MIKATABA 10 YA UTEKELEZAJI.

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 16 ก.ย. 2024
  • Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC kimesaini mikataba ya utekelezaji na miradi kumi ya kimkakati inayotekeleza miradi kwenye sekta mbalimbali hapa nchini ambayo inatarajiwa kuleta mafanikio makubwa katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini hapa nchini .
    Akiongea baada ya zoezi la kusaini makubaliano hayo waziri wa Uwekezaji viwanda na biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema kusainiwa kwa mikataba hii ni uthibitisho kuwa serikali ya awamu ya sita imedhamiria kukuza uchumi kupitia uwekezaji na kuzitaka Taasisi zote zinazotoa huduma kutoa ushirikiano kwa wawekzaji ili kuhakikisha mikataba ya wawekezaji hao inatekelezwa kwa wakati.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Gilead Teri amesema hii ni mara ya kwanza kwa TIC kusaini mikataba 10 kwa wakati mmoja ambapo miradi hiyo kwa pamoja inathamani ya dola za kimarekani 1805.15 na inatarajiwa kuleta ajira zipatazo 16355 na ajira 244400 zisizokuwa za moja kwa moja.

ความคิดเห็น •