MWANZO MWISHO TUKIO LA AJALI YA HELKOPTA ILIYO MUUA RAIS WA IRAN || MABAKI YALIONEKANA
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 19 พ.ค. 2024
- Televisheni ya taifa ya Iran imethibitisha kifo cha Rais wa nchi hiyo Ebrahim Raisi aliyefariki dunia kwenye ajali ya helkopta iliyotokea hapo jana Mei 19, 2024.
Taarifa inasema pia Raisi alikuwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Hossein Amir-Abdollahian ambaye pia amefariki dunia wakati walipokuwa wakirejea kutoka nchi jirani ya Azerbaijan kwenye hafla ya uzinduzi wa bwawa.
Wawili hao wamefariki baada ya ajali hiyo iliyotokea eneo la milimani katika jimbo la East Azerbaijan, ijapokuwa chanzo hakijatajwa lakini inaelezwa hali mbaya ya hewa ya ukungu ilikuwa imeenea eneo hilo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la IRNA, wengine waliokuwemo ndani ya helikopta hiyo ni pamoja na Gavana wa Mkoa wa Azerbaijan Mashariki, Malek Rahmati wa Iran na mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Mkoa wa Azerbaijan Mashariki, Ayatollah Mohammad Ali Ale-Hashem pamoja na walinzi.
Hata hivyo, vikosi vya uokoaji ambavyo vilipata shida kufikia eneo la ajali kutokana na ukungu na mvua, lakini baadaye vilipata mabaki ya helikopta hiyo kando ya mlima.
Mkuu wa Shirika la Hilali Nyekundu la Iran, Pir Hossein Kolivand, amesema waokoaji walipoona mabaki hayo, walisema hakuna dalili za uhai.
Serikali bado haijatoa tamko rasmi lakini shirika la habari la IRNA limesema kikao cha dharura cha baraza la mawaziri kimeitishwa kikiongozwa Makamu wa Rais Mohammad Mokhber baada ya tukio hilo.
Kwa mujibu wa Katiba ya Iran, iwapo Rais atafariki akiwa madarakani, kifungu cha 131 kinasema makamu wa kwanza wa Rais ndiye atakayeshika madaraka huku baraza linalojumuisha makamu wa kwanza wa rais, spika wa bunge na mkuu wa mahakama lazima lipange uchaguzi wa Rais mpya ndani ya muda usiozidi siku 50.
Kiongozi mkuu wa nchi hiyo, Ayatollah Ali Khamenei amewataka Wairani wasiwe na wasiwasi kuhusu uongozi akisema nchi itaendelea bila usumbufu.
Salamu za rambirambi zimeanza kutolewa akiwemo, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi aliyesema kwenye X kwamba, ‘ameshtushwa na kifo hicho cha kutisha’ huku akitaja mchango wake katika kuimarisha uhusiano wa pande mbili za India na Iran utakumbukwa daima.
Imeandikwa na Sute Kamwelwe kwa msaada wa mashirika ya habari ya kimataifa.
Kila chenye mwanzo hakikosi mwisho wa mwanadamu ni kama maua tuendelee kuandaa safari ya maisha yetu Kwa kumwamini Mungu na kujikita katika misingi ya dini 🎉
Mwenyezi mungu azidi kuwasamehe mazambi yaoo amiiiiiiiiin
Inalillah Allah akujaalie kauli thabit umetutangulia nasi tupo nyuma yako Nakuombea kwa Allah akusamehe pale ulipokosea mtetezi wa uislam tunakupenda sana natutazidi kukuombea dua kwa allah wema wako Allah akuhifadhi na adhabu za kabur
Ya Allah Warehenu Viongozi hawo kwa Msiba Mnzito Kwa Taifa La Irani Polesana Wanchi Wa Taifa Hilo Mkono Kwa Mkono Hadi Palestina Hadi Peponi Insha Allah
Mungu awalaze mahala pema Kwan na sis pia kwake tutarejea
Hiyo video na tukio tofauti acheni kupotosha
Mungu huhuzunishwa na kifo cha mwenye dhambi YESU ni mwokozi wa ulimwengu
Yesu nae alikuwa nadhambi nyingi nandomana akafa tena msalabani
@@AbuuAnuwar-ip7dr Ndivyo ulivyo fundishwa na Majini Kiarabu?
@@AbuuAnuwar-ip7drHata Yesu alisema Mungu uwasamehe kwa kuwa hajui walitendalo, sasa ni hivi Mungu akusamehe kwa kuwa hujui usemalo.. Au tusema hunamafundisho kuhusu hilo ndio maana..
@@AbuuAnuwar-ip7dralikufa Kwa dhambi nyingi za ulimwrngu mzima ili tupokee msamaha unapokataa msamaha huo itabidi dhambi zako uzibebe mwenyewe na mshahala wa dhambi mauti ya milele
Hakuna Rais niripenda falsafa zake kamahyo lnnalillah wainna illaihi Raajiun 😭😭🤲 from 🇹🇿
Mbona wengine wanamwita kafiri kulikoni??
Afadhari mungu kakuchukua umeua wengi wasiokua nahatia uliua mwanamke ambae hajavaa kiremba unafadhiri magenge yakigaidi mungu kaona utaimaliza Dunia ngojakirus ww uondoke
Nchi ya Irani inaongozwa kwa mujibu wa Sheria na misingi ya dini ya kiislamu, kupitia kitabu Cha Qur-an na Sunna za Mtume! na Ibrahim rais kabla ya kuwa rais wa Iran alikua mkuu wa mahakama!
Kesi kama ya kuzini na mke wamtu kwa mujibu wa qur-an Mzinifu huyu anatakiwa kupigwa mawe mpk hadharani mpk afe, Mwizi akiiba anatakiwa kukatwa mkono, ukizini hujaoa utandikwe viboko.
Na Sheria hizi zote alizisimamia kwa weredi kama misingi ya dini inavyoitaji ndo mana Leo mnamuona muovu Muuaji. Musimuhukumu yeye mchukieni Mungu wenu alieweka Sheria hizi maana yeye alikua anatekeleza TU maarisho ya Mungu wake na Hana hatia kwenye Hilo
Tanzania yetu Haina dini ndomana watu wanazini, wanaua, mashoga, wachawi na wanaendelea kukumbatiwa na Tz yetu kwasababu haiendeshwi kidini hawa wote wangekua Iran wangekua n marehemu
Poleni sana Ndugu zetu
Innalilahi wainna ilayhi ranjiuun allah akupe kauli thabit ameen mtetez wa palestin
tunauzuni sana wana wa east Africa mashariki poleni sana Irani Allah blessing all netanyau we need peace free palestina
Huzuni unayo wewe na magaidi wa Iran sisi ni wayahudi na hiyo ni kazi ya Israel
@@nicholauskilosa5336 Ukiwa wapi Ume pakatwa Nakupakwa mafuta Matakoni kwako😋😋
Unahuzunika peke yako mchijaji mkubwa wa raia wa persia ameaga
Siss. WA Israel tunafrah Sana
Sasa mukifurai kwamba hamutakufa mutaishi milele au 😏
Dah moyo unaniuma wallah Ibrahim Rais nampenda sana ❤😢
Iran 🇮🇷 Mungu awape rais mwenye msimamo thabiti kama wa Ibrahim Rais 😢😢😢
Acha uongo
@@justardzelphine6526😂😂😂
Mm kama nimewazaa, moyo unauma mpaka unataka kutoka😢😢😢😢
But he killed a lot of people
@@user-nb2jw4km6f hizi nchi Zinaongozwa na Sheria za kiislami , watu kuuwawa kwa sababu ya Sheria ni kitu cha kawaida si Sheria za mungu Wala si zake
Viongozi wjitambue huu usafiri wa anga unahitaji umakini sana tumepoteza wengi Kenya saitoti msumbiji Samora Burundi Habriamana Tanzania mbunge wa ludewa huko kwa wenzetu zinakotoka mbona hatusikii haya poleni ndugu zetu wairani b ; wote tuu safarini tuu Duniani sio mjii udumuooooo wamemaliza mungu awajalie mapuziko mema mbinguni& peponi ameni
Tena sanaa
🙏
Wa kwetu hapa amegeuza kama ndege kama daladala za kariakoo na mbagala
Kila mtu ataonja mauti kipi cha ajabu tangulia mwamba utalipwa kwa matendo yako
Sasa hapa Israel & Marekani wanahusikaje hata ukiangalia? Watu bwana daah! 😊
Sema Mungu hafurahii kufa kwa mwenye dhambi. Yesu Kristo ndiye njia kweli na uzima. Pole familia
Zambi Zauliziona wekafiri ww
Wewe nikondoo ulietajwa kwnye yeremia 50:6
Kafiri hanaga akili
Wewe hauna dhambi yesu ndiye njia yakuenda wap motoni?
Utajua yesu NI njia kweli na uzima usipomwamini yesu utabaki mtumwa wa shetani na majini mwanzo mwisho @@assfzainab912
Watakawia. Sana kumufaham mungu. Wa islael
Ukweli mungu wa israeli ni mungu wa kweli
Mungu mwenyewe kasema Alisha baliki Taifa la Israeli na watu wake pia nawanaolitakia mema but unakrupuka. Kushambulia. Bila kujua Mungu kawekeza nini pale ujuaji na kibuli Cha uzima kinatuondolea hekima Mungu bado hajafuta Wala kutengua. Alicho sema kuhusu taifa la Israel tusimfundishe kaz Mungu poleni watu wa Iran Mungu awape hekima yake
Nimekuelewa ndg yangu mungu alitoa mungu ametwaa sote ninjia hiyo
Hiyo NI mipango ya Mwenyezi Mungu kumchukua Mja wake. Maana ukiwasemea eti Mayahudi wanaishi miaka mingi mbona ata shetani toka Dunia imeumbwa umesikia amekufa?
@@saliminyusuph6122ameondoshwa na Mungu iyo ipo wazi dua ya wayahudi imefika kwa Mungu❤
Acheni ujinga kuwatukuza wapuuzi na serikali yao ya mabarsdhuli, hivi wewe unajua kuwa Israel ndio nchi inayo adhimisha sherehe za mashoga unajua kuwa mawaziri wa serikali ya Israel ni mashoga miongoni mwao, kama ilikua watukufu ni hapo zamani, sio wayahudi hawa wakizungu walikotoka ulaya na kujiweka mashariki ya kati kwasababu za kimaslahi, unajua kuwa wayahudi si wakristo na mungu amewalaani kwa kumkana aliewaumba, wewe ni wamaana kuliko hawa wayahudi tambua hilo, wewe haujalaaniwa na muumba wako kama wao
Dah nakumbuka niliongea nae juzi😢😢😢
Innallillah wainalilah rajiun
Inna llaah wainnailehi rajiuuni.
Poleni
Poleni wana wa Mungu
Poleni sana
SubhanAllah so sad
Inalilah wainalilah rajighun
Allah awastir Rais w iran na wenzake
Tayari wamemuuwa 😢
Inaniuma sana.😢😢😢
Pole sana ni huxunii kabisaa wapumxike kwa amanii
Hua siamini ndege maisha yangu yote
Mimi Pia ndege na Mzungu (Mkoloni)siezi kuviamini
@@evelynemugeni2369lakini hiyo niya mwarabu siyo mzungu sasa sjui mzungu anaingiaje hapo😂😂😂
Mimi meli sismini
Kifo ni popote tu kuogopa usafiri haimanishi kuwa ukipanda ndo utafia ndegen
@@mariamdullazy8166😂😂😂why ndegen lakini????😂😂😂😂
Ooooh! Jaman R. I. P
😢😢😢😢😢Innallillah wainnaillah rajeun Allah amsameh pale ambapo amekosea amin amin amin 🤲 🤲 🤲 ✍️
Pole Kwa taifa na familia zilizowapoteza wapendwa wao
Kwa kweli kifo ni haki ya mwanadamu
innalillahi wa innailayh rajiun
Inalilahi wa Ina ilaihi rajiun
inaumiza sana
Poleni wafiwa
M.mungu wasemeh makoda yao yoote na uwafanyiye wepes ktk kabri lawo
Teali
Sasa hawa wanao chukuwa vidio dunianzima au vip kumbe walikuwa wanaona 😢😢 munguu awasamehe wote waliyo tanguliya😢😢amin
Tamka Iran vizuri jamani unaitamka sio japo makala nzuri safi
Inalillahi wa inailayihi rajuhuni
Poleni ii ilitutokea watanzania kiongozi kuondoka akiwa madarakni mungubawarehem marehm wote
Daah!!!!,,polen sana kwa msiba huoa mkubwa wakuokewa na rais wenu mpendwa,,""Mungu ametoa mungu ametwaa jina lake lihimidiwe,,amen😂😂😂😂¡!!!!!.
Needs more forensic and analysis investigations required together with the technical teams and aviation teams to be investigated too
Akome kumtisha israel
Innalillah wanna ilaihi rajiuun
Innalillah wainna ilayh rajighun
Inalilah waina ilayh raajiun
😢😢😢😢 Dah basi tu
Polensana mungu moyo wauvumilivu
Hili ni pigo kwa irani kuanzisha choko choko kwa israel. Helikopta haikuwa ya jeshi?
Mungu azilaze roho zamarehemu pema peponi😢
Mungu hatumwi KAZI ya kumlaza MTU yoyote Kwanza huko mbinguni hakunaga usingizi wa kuwalaza watu mwanadamu anakabiliwa na mambo mawili Tu Moto Kwa waovu na paladiso Kwa watakatifu mambo ya kulala au kulazwa pema hayapo huko unawekwa unaposthili kuwekwa Kwa kadli ya matendo yako
Eehee
Innalilah wainna ilayhi raajiun
Innalilah waina illah rajiun 😢
parachuti awakua nazo uo ni uzembe
Pumzika kwa amani
Iran wanakatiba nzr sana,na si ya Tanzanie
Innalillah waiina ilayhi rajiuun
Daa! Helicopter ciyo usafir mzur kwa rais.
Ingekuwa ile ya rais wa marekani ingepaki angani hadi ukungu uishe ndo safar iendlee.
Tembo hawezi kufanana na sisimizi
Mungu ibaliki Eslael🇮🇱 na president wake pamoja na keshi lake).,,,,,,ma Irani wamezoea kuingilia vita isiyo wahusu ,ne nditigila de nguluvi kisonzo,,,
Kumbe mpowengi njo upigane namim usiejitambua
Habar nzur lakin kigugumiz kikubwa mno kwenye kuriport
Niunge kwenye group la aqaz
Mimi huu usafiri na Wa majini mmmm
Rest in peace 😢Iran president
Raisi samia unaona kazi ya mungu jitahidi utende haki kwenye utawala wako wewe hukuchaguliwa na wananchi Bali amekuchaguwa mungu a kwa ajili ya wale mahehe walio magaidi mungu aliwanusuru kupitia wewe chengine nakushauri wamasi wa ngorongoro Kam hataki kuhama usiwafosi maisha ya mwanadamu ni madupi San usikubali kweny utawala wako uharibu usisikilize ushauri ambao sio sahihi
😂😂😂😂 yaani wee jamaa nimecheka
Makafiri mnazani kua kufa niadhabu kufa nisuku2 zikifika acheni ufara nyie
😂😂😂😂😂yan samia amechaguliw na mungu 😅😅😅😅jaman samia yup hyu hyu au mwingne
Jaman kwann hawakuruka au hapakuwa na parachuti
Ndege imepigwa hiyoo.
Mungu atupe hekima ya kuongea jamani
😢😢😢
إنا لله وإنا اليه راجعون
Hata yaweza kuwa Israeli inawakataa magaidi wanaoichukia bure tu. Lakini magaidi wanaifuatia kwa kudanganywa na akina Ayatollah! Shetani ni muongo na ni baba wa uongo!
Sasa kama kulikuwa ma hali mbaya ya hewa kisha kukawa na tatizo la helcopta je hakukuwa na mawasiliano kupeleka ndege nyengine kuwaokoa kabla ya kuanguka. Je hakukua na parachuti kujiokoa mbona hilo tukio lipo halifahamiki taarifa zak. Allah awasamehe makosa yao.
Poleni kwamsiba mkubwa
Very sad
So sad
MSOMAJI VIPI.....HAKUNA NCHI DUNIANI INAYOITWA AZIZI-BAIJANI........
Nadhani amemaanisha ghaza
Imetunguliwa hiyo
Rip
Huyu raisi wa irani nilikuwaga nampenda sana
Mwongo sema unapenda ugaidi bwana
Rest in peace.
😢
Furaha ya milele uwape ee bwana na mwanga wa milele uwaunganishie wapumzike kwa amani
Kumradhi 👉 sio aziz ni Azbaijan
😢😢😢😢
Viongozi wenye kauli tata na msimamo huwa nawaaminia Sana Ila ndo hivo
Anasubiliwa. Mwingine ajipendekeze
There’s more to this story than what’s been let out, you’ve got to read between the lines people!!
Huwezi cheza na Israel , ukaishi.
Hakuna kitakqchotokea,ndege imeqnguka ndani ya territory yao ,yaani ndani ya anga Lao ambalo kimsingi lilikuwa likilindwa na Jeshi la anga la nchi yake .hapo watanyoosheana vidole wao kwa wao.
Innallilaah wailaaillaajun
Hivi Ericopter hazina parachuti ? kwann wasingeruka ?
Hata mm najiuliza hilo
Mimi pia nawaza ndege ya rais Haina hata self defense 😭
@@user-ju4md1yq6oMungu akitaka kitu fulani kifanyike hata parachuti ikiwepo haitatumika😮
Mungu akitaka kufanya kitu chake hata psrachuti ikiwepo haitatumika..
Incoherent story
Islaeli hapa naihisi sana!
Naona kweli kabisa maana sio Kwa makombola Yale alipanga kuwanyoosha islaeli wamemnyoosha yeye kinyozi kanyolewa Kwa wembe butu
Hiyo video na alichukua
MUNGU HAFURAHII KIFO CHA MWENYE DHAMBI.
ACHENI KUFURAHIA KIFO CHA MTU HUYO.
IJAPOKUWA INAONESHA KITU.
Wekafiri funga makalio ayo
mpumbavu huna ata moyo wauruma
Mbwa koko unaongea nn
Mkoa wa azizibeijan???
Hakukua ata na parachute 😢
Helicopter ilikosa muelekeo kama vile ilipigwa
Haujui KUTOA news 😅 ila enye itakufanya watu wachekii hii vedio ni hiyo sauti tu😅