Wafanyabiashara Holili wafunga barabara kushinikiza ushuru uondolewe

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 11 ก.ค. 2024
  • Wafanyabiashara wa nafaka eneo la mpaka wa Holili, Wilaya Rombo, mkoani Kilimanjaro, wamefunga barabara kuu ya Holili-Moshi kwa zaidi ya saa mbili wakishinikiza Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, kuondoa ushuru wa Sh300,000 kwa kila gari lenye mahindi, linaloingia katika soko la nafaka Holili.
    Wafanyabiashara hao ambao walipanga magari yenye shehena za mahindi, katikati ya barabara katika eneo la Holili na kuzuia magari yanayotoka nchi jirani ya Kenya na yale yanayotokea upande wa Himo, wamesema wamechukua uamuzi huo, baada ya kuwepo kwa mabadiliko ya gharama za ushuru, kutoka Sh50,000 hadi 300,000 hali ambayo inawaumiza.
    Hatua hiyo ilimlazimu mkuu wa Wilaya ya Rombo, Raymond Mwangwala kufika eneo la tukio kuzungumza na wafanyabiashara hao, ambapo wamekubaliana kuzuia ushuru huo wa Sh300,000 na kuendelea na ule wa Sh50,000, kwa siku saba, ili kupisha mazungumzo kuhusiana na malalamiko hayo.
    Wakizungumza leo kwa nyakati tofauti katika Soko la Holili, wafanyabiashara hao wamesema, kabla ya kufikia mwezi Julai mwaka huu walikuwa wakitozwa Sh50,000 kama ushuru wa mazao wakati wanapotoka sokoni Holili kwenda nchi jirani ya Kenya lakini kwa sasa wameshtushwa na ushuru huo kuongezeka hadi kufikia Sh300,000.
    Wamesema mbali ya Sh300,000 pia wanatozwa Sh10,000 kwa kila gari inayopita bila kujali kama ina mzigo au haina mzigo wakiambiwa ni tozo ya maegesho ya magari, huku wakikalamika kutozwa wakiwa wanapita bila kuegesha gari.
    Akijibu malalamiko hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rombo, Godwin Chacha ambaye aliongozana na Mkuu wa Wilaya kufika eneo hilo, amesema wamepokea kero hizo na kwamba wataka na wafanyabiashara hao ili kutafuta suluhisho.
    Akizungumza Mkuu huyo wa Wilaya, Mwangwala amewataka wafanyabiashara kuwa na subira na kutoa siku saba kwa watendaji wa halmashauri kukaa na wafanyabiashara kuzungumza ili kupata suluhusho.

ความคิดเห็น • 8

  • @hassankongolilo8408
    @hassankongolilo8408 23 วันที่ผ่านมา

    daah serikal inahimiza ugunduzi na uvumbuzi wa kukusanya kodi. Vichwa maji washagudua sasa

  • @kajugaa4537
    @kajugaa4537 24 วันที่ผ่านมา +1

    Mmmh yaani hichi kipindi kigumu unaweza hisi kama matatizo yanatengenezwa ili yatatuliwe watu wapige makofi au basi bwana Wacha nilale tu

  • @kaaakwakutuliaa5179
    @kaaakwakutuliaa5179 23 วันที่ผ่านมา

    kumanina mpaka kieleweke

  • @MajutoElliasi
    @MajutoElliasi 23 วันที่ผ่านมา

    Hii nchi gumu kuishi watedaji wetu hawatupendi wanajipenda wawo daa 😂😂😂

  • @kaaakwakutuliaa5179
    @kaaakwakutuliaa5179 23 วันที่ผ่านมา

    samia ndo anatoa maelekezo

  • @kaaakwakutuliaa5179
    @kaaakwakutuliaa5179 23 วันที่ผ่านมา

    mchawi ni ccm

  • @user-wj6zj1ly4e
    @user-wj6zj1ly4e 24 วันที่ผ่านมา

    Hyo ipo tu, kule mtukula kiaka kuna 150000 na sirari pale kachuma kuna 120000

  • @user-il5pk2dr5n
    @user-il5pk2dr5n 23 วันที่ผ่านมา

    Sasa hii biashara ya nafaka ishakuwa ngumu shamba ushuru sokoni ushuru,stakabadhi ghalani ndo tafrani kabisa waweza kununua mbaazi au ufuta kg 2500, ukasikia mnada wamepiga 2200,unashika kichwa