Operesheni Kubwa Yazima Uzalishaji wa Bangi Bonde la Mto Mara. Kamishna Jenerali Lyimo asema haya...

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 22 ต.ค. 2024
  • Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo jeshi la polisi, jeshi la akiba pamoja na wananchi imefanya operesheni kubwa ya kihistoria kwa muda wa wiki tatu katika wilaya ya Tarime na Serengeti, mkoani Mara kwa lengo la kukabiliana na tatizo la uzalishaji na usambazaji wa dawa za kulevya, hususan bangi.
    Operesheni hiyo imefanyika katika vijiji vya Matongo, Nyarwana, na Weigita vilivyopo bonde la Masinki, pia vijiji vya Nkerege, Kembwe, Nyakunguru na Iseresere pamoja na eneo la bonde la mto Mara.
    Akizungumza mara baada ya operesheni hiyo leo tarehe 8 Oktoba, 2024 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema, jumla ya ekari 3,007.5 za mashamba ya bangi zimeteketezwa katika operesheni hiyo. Aidha, kilogramu 7,832.5 za bangi kavu, na kilogramu 452 za mbegu za bangi zilikamatwa, ambapo watuhumiwa 17 walikamatwa na tayari wamefikishwa mahakamani.

ความคิดเห็น •