NGUVU YA DAMU YA YESU - PASTOR JOHN SEMBATWA

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 8 ก.พ. 2025
  • Waebrania 12:24
    [24]na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.
    Mjumbe ni nafasi ambayo huwakilisha kiti chenye mamlaka zaidi.
    Warumi 8:6
    [6]Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.
    Kama mwili umebeba mauti na lengo la roho ni uzima na amani.Neno la Mungu linasema kuwa msinywe damu maana ndimo kuliko na uhai..kama mwili umebeba mauti ili uhai uweze kurudi basi inahitajika damu maana damu ndio uhai wenyewe. Yesu alipokuja na kutukomboa ilihitajika damu yake ili kuhuisha miili yetu na roho zetu kutoka kwenye umauti na kurudi kwenye uzima.Kwa sababu damu imebeba uhai,kwa maana nyingine damu ya Yesu iliyomwagika msalabani ni uhai wake mwenyewe.Yesu ni Mungu, kwahiyo Mungu aliamua kutumia uhai wake mwenyewe kutukomboa.Kwa maana hiyo kila wakati unapoongelea damu ya Yesu unaongelea uhai wa Mungu mwenyewe.
    Damu hubeba fidia ya kile kilichofanyika, ndio maana Biblia inasema pasipo kumwagika kwa damu hakuna ondoleo la dhambi. Kuna dhambi ambazo zilifanyika kwenye vizazi vya nyuma na zikatuingiza kwenye mateso, lakini leo tumejifunza namna ambavyo tunaweza kuitumia damu ya Yesu (yaani uhai wa Mungu mwenyewe) kutoka katika hivyo vifungo. Haijalishi walichinja wanyama gani na wakatoa sadaka za damu,haijalishi walitumia damu za watu lakini tunayo damu ipitayo damu zote,damu inenayo mema kuliko ile ya Habili!
    Hii ni damu inayozungumza, popote ambapo umeonewa na kukandamizwa itasimama na kuongea kwa niaba yako namna ambavyo imekukomboa,popote adui anapokudai itasimama na kusema namna ambavyo imekulipia deni zote pale msalabani.
    UNAWEZA WASILIANA NASI AU KUTUMA SADAKA YAKO KWA NAMBA HIZI : +255 657 173 322 AU +255 764 888 810
    Unaweza kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii
    Like our Facebook: / therealityof. .
    Follow our Instagram: / realityofch. .
    Subscribe our TH-cam: www.youtube.co....
    Also Subscribe Roc worshippers youtube channel: / @rocworshipperz
    and Subscribe Pastor Sunbella Kyando TH-cam
    / @pastorsunbellakyando
    #RealityofChrist #PastorSunbellaKyando #PastorJohnSembatwa

ความคิดเห็น • 14