MAFURIKO DAR: BAJAJ YAZAMA KWENYE MAJI na KUPINDUKA, ABIRIA ALIYENUSURIKA KUSOMBWA NA MAJI AFUNGUKA

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 6 ก.พ. 2025
  • MAFURIKO DAR: BAJAJ YAZAMA KWENYE MAJI na KUPINDUKA, ABIRIA ALIYENUSURIKA KUSOMBWA NA MAJI AFUNGUKA
    Ama kweli usicheze na mafuriko! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatilia tukio la dereva Bajaj mbishi aliyelazimisha kukatisha barabara inayotokea maeneo ya Ubungo Shekilango Bandari kavu Dar na kujikuta wakielemewa na maji yaliyojaa kwenye barabara hiyo na Bajaj hiyo kuzima ikiwa katikati ya dimbwi la maji.
    Kufuatia hali hiyo dereva huyo hakuwa na jinsi zaidi ya kushuka kwenye dimbwi hilo na kujaribu kuisukuma Bajaj hiyo ikiwa na mteja ndani lakini zoezi hilo lilionekana kuwa gumu mpaka aliposaidiwa na Wasamaria Wema waliokuwa eneo hilo.
    Wasamaria hao walisaidia kuinasua Bajaj hiyo ndipo mteja aliyekuwemo Bibi Kizee aliweza kushuka na kuzungumza na Global Tv.
    Bibi Kizee huyo alielezea dakika kadhaa za mateso alipokuwa katikati ya dimbwi hilo na ambapo pia alielezea masikitiko yake kwa kuharibika kwa baadhi ya vitu alivyokuwa navyo.
    Sambamba na dereva Bajaj huyo pia walionekana waendesha bodaboda na magari wengine nao wakipita kwa shida eneo lililoonekana kutokuwa na njia nyingine mbadala karibu na eneo hilo zaidi ya kukatisha hapo.
    Sambamba na vyombo vya moto pia walionekana wanafunzi wanaoishi upande wa pili dimbwi hilo wakivuka kwa taabu huku wakihatarisha usalama wao kutokana na kuingia kwenye maji hayo yanayotokea viwandani ambayo huenda yakawa na kemikali za viwandani na kuwadhuru. Habari hii imeletwa kwenu na mwandishi wetu, Richard Bukos wa Global Tv.
    CHOTA MAPENE ndiyo mchongo mpya town! Kwa shilingi 1,000 tu, yaani BUKU unajichotea mapene kibao au kupata nafasi ya kujishindia ZAWADI MBALIMBALI KILA SIKU, KILA WIKI kupitia Global TV, Global Radio na mitandao ya kijamii!
    ========================
    Ingia kwenye simu yako📲, sehemu ya kufanyia malipo, andika namba ya kampuni 553111, kumbukumbu namba 255 au andika neno GLOBAL. Weka kiasi cha shilingi 1,000, weka namba yako ya siri, thibitisha na tuma.👍 PEASA UTATUMIWA MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO!🤝👍💰
    ============================================================
    ⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI?
    ⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 713 750910), ( +255 783453136)
    ⚫️ Email: globaltvonlinenews@gmail.com
    ⚫️ OUR PLAYLISTS:
    ⚫️ MICHEZO na BURUDANI: • Habari zote za michezo...
    ⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: bit.ly/mikasa_y...
    ⚫️ GLOBAL RADIO TV: bit.ly/255globa...
    ⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: bit.ly/exclusiv...
    ⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: ndstream.net/gl...
    ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
    ⚫️ ANDROID:bit.ly/38Lluc8
    ⚫️ iOS:apple.co/38HjiCx

ความคิดเห็น • 4

  • @faiditv5535
    @faiditv5535 ปีที่แล้ว +2

    Waandishi pia muwe msaada sio kuripoti tu kwanini mnawaacha wanafunzi huku mkijua kunakemikali?

  • @Sharefa-v6n
    @Sharefa-v6n ปีที่แล้ว

    Duuu Kaz imeanza tena

  • @mankinemansulikine-2220
    @mankinemansulikine-2220 ปีที่แล้ว +1

    Ivi uyo mwenye bajaji akuona km ayo maji mengi

  • @OG_20
    @OG_20 ปีที่แล้ว

    Was it necessary kumuita huyo mama wa watu bibi kizee...seriously??