Ndugu, hebu niambie wimbo kama huu wawezaje kukosa kuyafanya machozi yasitiririke ukumbukapo enzi hizo? mimi ni mkenya lakini sanduri hii iliweza kunibadilisha rohoni mwangu kiwango cha kujitambulisha kama mojawapo wa hao watanzania. Hawa vijana walijua kazi yao sana, sauti zao zanikumbusha mengi sana ya uzuni na raha pia. Long live TZ, long live Kenya. Ombogo. Fl.
Humu watu wameimba, wameifungua sanaa, ujumbe umewekwa wazi, vyombo vimepigwa kwa kusikitika sanaa, na vimekubali sanaa. Mwenye hisia za karibu na ukikumbuka hawa walishatangulia mbele ya haki lazima chozi likutoke.....kazi nzuri mliifanya, ahsante kwa alama na tunu hiii, mpumnzike kwa amani.
Wapumzike kwa amani nguli wetu katika sanaa ya muziki. Hizi ni miongoni mwa nyimbo zilizouwa zinatambulisha Taifa popote duniani. Vijana wenzangu wa sasa wanaweza kuzipuuza lakini zimebeba mengi zaidi ya ujumbe.
Me kijana Kaka lakini nashindwa kusikiliza bongo flavor hizi ndio ngoma zangu,, sikiliza kinanda Cha abel baltazar na solo ya mulenga hatari Sana hizi kazi
Maalim Gurumo na Maalim kinyasi Hamisi Juma na vocalist wengine mahili katika wimbo mzuri usiochosha masikioni,, daaah!!!@ Celina piga konde Moyo....... I love this song forevermore.
Wimbo huu ulikubalika na watu wote. Wapigania uhuru wa PAC na ANC za Afrika ya kusini waliokuwa wanaishi hapa nchini wakati wa harakati za ukombozi, waliuvulia kofia wimbo huu. ❤
GOD bless the most beatyfull land of africa mabonde na milima i wish nisinge ondoka the amazing land one day i will be back am just crying in the heart of ulaya
Kwangu huu ndio wimbo wapili wa DDC Milimani park kwa ubora. Nambari moja ni "Sauda Unatutia aibu"....Cosmas anasikika vizuri sana humo ndani. Mungu akupe maisha marefu....Oh Celina piga konde moyo oooh Celina utafanikiwa ooh Celina....aahhh mwaka 1982 wanirudia...
Nakumbuka sauti ya Maalimu ngurumo. Nilikuwa mtoto, lakini nakumbuka vizuri sana hizi beat zake. Mungu awalaze pema wengi waimbaji waliotangulia mbele ya haki
La hasha bwana Charles O. Masewe. Huu ni mwaka wa 1978. Na huu wimbo ni KIJEMBE kwa Juwata(Nuta) baada ya Muhidin Gurumo(RIP) KUIHAMA jUWATA NA KUJIUNGA NA DDC Mlimani Park. Kuhama kwa Muhidin kwenda Mlimani Park kulizua maneno, uhasama na chuki nyingi kutoka kwa Juwata kwani Muhidin alikua nguzo muhimu tangu wakiitwa NUTA - waliyumba yumba kidogo.Kwa hivyo "'Celina''(Juwata) hapa anaambiwa ajipige moyo konde na kuangalia mbele kwani Muhidin kesha kwenda. Huu ni baadhi ya nyimbo za DDC Mlimani park za mwanzo mwanzo kabisa hata Bitchuka alikua bado kujiunga na DDC hapa.
Once upon a time, there used to be an announcer on the Voice of Kenya swahili service, Ali Sahlim Manga. With his infectious laugh introducing salamu za wanajeshi, he was always sure to spin one of DDC's greats ---weekend, baruwa kutoka kwa mama. And I would pray it would be CELINA. The sax would kill me in this, Michael Enock he is I think. Supreme!
@@isayamazani22 Also known as King Enock... I think he was from Zambia, went to to join the Dar es Salaam based Music Band... Alifanya kazi kubwa pamoja na wakongwe wengine kama Gulumo, Abel Bartazar na wengineo wengi... Tukiwa wadogo miaka ya 80s tunasikia nyimbo hizi Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD), saa sita mchana au saa nane kipindi cha Salaam Mkulima, Malima Ndelema akiunguruma.
Samahani sana ndugu Mawazo ,nilikuwa namjibu mtu mwingine aliyesema nasota katikati ya Ulaya kwa wimbo mwingine na kwa bahati mbaya niligusa jina lako kimakosa samahani alisema najuta kwa nini niliondoka nyumbani.
@Fiskarrr Vocals ni Muhidin Mwalimu, Hamisi Juma (RIP) na Cosmas Chidumule. Lead guitar Abel Balthazar (RIP), bass Joseph Mulenga (RIP), rhythm Abdallah Gama. Drums Habib Abbas 'Jeff'. Marijani Rajab alifariki 1992.
Nimejitahidi kadiri ya uwezo wangueeeee, Wazazi wako waliniwekea vikwazo VINGI!!!!!!- Nia yangu na madhumuni yangu ilikuwa tufunge ndoa na tuishi sote kama mke na mume Celina. NYIMBO YA JANA; LEO; KESHO NA MILELE.
Nikisikia wimbo huu, nakumbuka nyumbani mabibo,barabara ya mabibo, kabla haijajengwa. Kwa sasa mashine ya mbao. Eneo hili ilimopita barabara, mlikuwa na makaburi, mashamba ya mpunga, na miti ya miembe. Nakumbuka kampuni ya moremo ikijenga barabara ya mabibo. Wimbo, unanikumbusha mengi
ajabu ni kwamba huu wimbo kenya haukujulikana sana. when i visited tzin november last year i was surprised to learn that it was such a big big hit from the ddc milimani park and also one of their very frst songs.
+nicholas murithi Nyimbo nyingi za Tanzania zilikua zikivurumishwa katika radio ya Kenya,wakati huo ikiwa ni moja tu nayo ni VOK na baadae KBC.Hata huu wimbo ulikua ukichezwa ingawa sio sana.Mimi binafsi kwa mara ya kwanza niliusikia VOK miaka ya '77/78 /79 huko.
asánte tzboy ukitaka kujua kwamba wewe ni mzalende kaa majuu, unanikumbusha mbali karibu na asubui yani zamaaniii RTD sita ya mchana natoka shule ya msingi korogwe huku na wahi lunch home kipoindi cha mchana mwema.abdi haibe abdisa kb sweden God bless motherland.
Moja kati ya nyimbo nzuri sana za DDC miaka hiyo ya 1978 nikiwa darasa la 5, nikisikiliza MCHANA MWEMA, RTD kupitia National 2_7_7 yenye sanduku la mbao. Walale peponi magwiji hao wa muziki wa dansi uliokuwa unaitambulisha Tz kwa aina hii ya muziki. Ooh Celina piga konde moyo, ooh Celina, tutafanikiwa ooh Celina mamah.
Nilikuwa na miaka 13 nasoma darasa la tano 1978 Nyamighadu shule ya msingi namkumbuka sana marehemu Babu yangu Lucian Ghughulu na marehemu Sabina Limingwa
Mzee Gurumo alikuwa DDC zamani akahamia msondo Ngoma leo Mzee ni mgonjwa sana nyumbani kwake na wana Msondo wamemtenga na wala hawana habari nae lakini huu ni mtihani wa ulimwengu hutokea kwa kila mtu lakini ushukuru kibanda ya kujihifadhi unayo na mama watoto wako anakutunza nakuombea afya njema.
Mimi natoa shukrani kubwa sana kwa msanii Diamond kwa kumtukuza mwimbaji wetu wa miziki ya kitanzania gari mpya ili imsaidie, sio hao wengine wanaomtukuza kwa maneno matupu tu bila kitu ingawa yeye ameutukuza mziki mpaka amefikia umri huu. tunamwombea umri mrefu mzee Gurumo.
Huu wimbi ni true story kwa Joseph Bartholomew Mulenga ambaye alimpenda Celina lakini wazazi wake wakamwekea vigingi na Celina akataka kujiua ndiyo message halisi
Waimbaji katika wimbo huo ni Cosmas, Maalim Kinyasi na Gurumo, solo(Mulenga),bas(Abel),rithym(Gama),tumba(Jamwaka),sax(King Enock),hiyo timu kwa kweli haitasahaulika katika muziko wa nchi hii, mziki huu hata Kama timu yako Kulwa au Doto(Kariakoo)imefungwa wewe sikiliza Celina (Mliman) unasahau machungu yako ya kufungwa
Tizedboy, kulikuwa na mpango kwamba zile lyrics za nyimbo zilizo kwenye ile page yako uzihamishie JAMIIFORUMS. Tafadhali kama inawezekana wasiliana na jamaa wa forum, wakupatie kisehemu na utuwekee hizi nyimbo na yale maneno yake. Thanks very much kwa kupost hizi nyimbo. Unatunza sana sehemu ya historia yetu ya Tanzania. Bod bless.
nakumbuka nyumbani Rufiji enzi hizo kila kitu bure tu utavunja mua ndizi maboga mapapai yanaoza hakuna wa kumuuzia tulikua tunakula na hakuna wa kukuuliza yani we acha tu hapa nakumbuka mbali sana.
Ndugu, hebu niambie wimbo kama huu wawezaje kukosa kuyafanya machozi yasitiririke ukumbukapo enzi hizo? mimi ni mkenya lakini sanduri hii iliweza kunibadilisha rohoni mwangu kiwango cha kujitambulisha kama mojawapo wa hao watanzania. Hawa vijana walijua kazi yao sana, sauti zao zanikumbusha mengi sana ya uzuni na raha pia.
Long live TZ, long live Kenya.
Ombogo. Fl.
Humu watu wameimba, wameifungua sanaa, ujumbe umewekwa wazi, vyombo vimepigwa kwa kusikitika sanaa, na vimekubali sanaa. Mwenye hisia za karibu na ukikumbuka hawa walishatangulia mbele ya haki lazima chozi likutoke.....kazi nzuri mliifanya, ahsante kwa alama na tunu hiii, mpumnzike kwa amani.
Nilikuwa skuli, katika umri wa utineja na tulizikia nyimbo hizi redioni hususan vipindi vya mchana mwema, ombi lako nk
Haisee.old.is.gold
Nakumbuka.mbari.sana.nikiwa.shure.yamsingi.kangetutya.bunda.nawakumbuka.hawa.jescka.john.kim.samson.ngwashi.merik.haisee.ilikua.hatar.sana.
@@jacob2382Ni shule na siyo Shure.
Zingatia matumizi ya L na R
Wapumzike kwa amani nguli wetu katika sanaa ya muziki. Hizi ni miongoni mwa nyimbo zilizouwa zinatambulisha Taifa popote duniani. Vijana wenzangu wa sasa wanaweza kuzipuuza lakini zimebeba mengi zaidi ya ujumbe.
Me kijana Kaka lakini nashindwa kusikiliza bongo flavor hizi ndio ngoma zangu,, sikiliza kinanda Cha abel baltazar na solo ya mulenga hatari Sana hizi kazi
Patrick liyai apumzike kwa amani Muhidn mtunzi na mwenye Sauti ya kufana
Wimbo mtamu,taratibu na wenye mpangilio wa kuaminika,maneno yamewekwa kwenye mizani ya ufasaha na yakafuzu zuuu!! Muziki kama dawa.Pure niceness...
inanikumbusha mwaka 79 nikiwa mdogo mpaka leo ubora wake upopalepale zamani waliimba ddc bendi bado mpya apo
Maalim Gurumo na Maalim kinyasi Hamisi Juma na vocalist wengine mahili katika wimbo mzuri usiochosha masikioni,, daaah!!!@ Celina piga konde Moyo....... I love this song forevermore.
Wimbo huu ulikubalika na watu wote.
Wapigania uhuru wa PAC na ANC za Afrika ya kusini waliokuwa wanaishi hapa nchini wakati wa harakati za ukombozi, waliuvulia kofia wimbo huu. ❤
GOD bless the most beatyfull land of africa mabonde na milima i wish nisinge ondoka the amazing land one day i will be back am just crying in the heart of ulaya
Nakumbuka marafiki wangu ambao wengi sasa ni mrehem na wengine wazee mno maisha yanaenda kasi Sana bora watu wamrie mungu
Saa tank unusu hadi saa saba,
Nyimbo hizi zilituliza mioyo ya wagonjwa , kipindi cha ugua pole, hospitality kuu ya mumblli
Kwangu huu ndio wimbo wapili wa DDC Milimani park kwa ubora. Nambari moja ni "Sauda Unatutia aibu"....Cosmas anasikika vizuri sana humo ndani. Mungu akupe maisha marefu....Oh Celina piga konde moyo oooh Celina utafanikiwa ooh Celina....aahhh mwaka 1982 wanirudia...
Kwa kweli Cosmas ni nguli Now ni Mchungaji wa kanisa la TAG hapa Tanzania
mlimani wanatoa celina kupata wakatoa mpenzi zarina.....kwa kweli tulienjoy mwaka 79....
Mwaka 1978 ulivuma sana huu wimbo utunzi wake Joseph Bartholomeo Mulenga 'King Spoiler" na kisa cha kweli
Duuh hii ngoma naisikiliza kila siku ngoma tamu sijawahi sikia aiseee duuuh...haiwezi kujirudia mara mbili.
NAKUMBUKA wakatri nilifika pale tanzania, WIMBO nzuri sana, GABY!
Ulikuwa na umri gani?
Nakumbuka sauti ya Maalimu ngurumo. Nilikuwa mtoto, lakini nakumbuka vizuri sana hizi beat zake. Mungu awalaze pema wengi waimbaji waliotangulia mbele ya haki
Mziki mzuri sana, utaendelea kuishi vizazi na vizazi.
Maalim Muhiddin was a real singer. I used to listen to his music in 1974.
La hasha bwana Charles O. Masewe. Huu ni mwaka wa 1978. Na huu wimbo ni KIJEMBE kwa Juwata(Nuta) baada ya Muhidin Gurumo(RIP) KUIHAMA jUWATA NA KUJIUNGA NA DDC Mlimani Park. Kuhama kwa Muhidin kwenda Mlimani Park kulizua maneno, uhasama na chuki nyingi kutoka kwa Juwata kwani Muhidin alikua nguzo muhimu tangu wakiitwa NUTA - waliyumba yumba kidogo.Kwa hivyo "'Celina''(Juwata) hapa anaambiwa ajipige moyo konde na kuangalia mbele kwani Muhidin kesha kwenda. Huu ni baadhi ya nyimbo za DDC Mlimani park za mwanzo mwanzo kabisa hata Bitchuka alikua bado kujiunga na DDC hapa.
naupenda saaana huu wimbo jmn 😘😘😘😘 2020
Once upon a time, there used to be an announcer on the Voice of Kenya swahili service, Ali Sahlim Manga. With his infectious laugh introducing salamu za wanajeshi, he was always sure to spin one of DDC's greats ---weekend, baruwa kutoka kwa mama. And I would pray it would be CELINA. The sax would kill me in this, Michael Enock he is I think. Supreme!
Michael Enock was also known as Ticha(teacher) as he was a full musician capable of playing all instruments and also vocal
And elizabet obege .lat V.O.K
@@isayamazani22 Also known as King Enock... I think he was from Zambia, went to to join the Dar es Salaam based Music Band... Alifanya kazi kubwa pamoja na wakongwe wengine kama Gulumo, Abel Bartazar na wengineo wengi... Tukiwa wadogo miaka ya 80s tunasikia nyimbo hizi Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD), saa sita mchana au saa nane kipindi cha Salaam Mkulima, Malima Ndelema akiunguruma.
Asante sana ngimbo iko sawa sawa
Hazitasahaulika
Samahani sana ndugu Mawazo ,nilikuwa namjibu mtu mwingine aliyesema nasota katikati ya Ulaya kwa wimbo mwingine na kwa bahati mbaya niligusa jina lako kimakosa samahani alisema najuta kwa nini niliondoka nyumbani.
Asante sana kwa wimbo huu, good old days!!!. RIP Gurumo
WE acha tu !
Mimi kwa ukweli sipendi TBC ! Haitambuliki, Tadio ni RTD ( Radio Tanzania Dar ). Nyimbo zao zilikua viti mno
Bass: Abel Balthazar
Rhythm: Abdallah Gama
Solo: Joseph Mulenga
Keyboards: George Kessy
Vocals: Gurumu Muhidin, Hassan Bichuka
Vocalists are Hamisi Juma, (r.i.p) Ngurumo (r.i.p) Chidumule, Assosa, Bitchuka not joined yet then.
Asante sana kwa kutukumbusha magwiji hawa, Hilo gitaa la Bass linaniua mimi jamani Abel, Mungu AWABARIKI sana popote mlipo.
Bichuka hakuwepo wimbo huo alikuwa Bado yuko Juwata😅
@@charlesbayona9090 Asante kaka
Hii ndio kazi ya mkono penda sanaaa maudhui ujumbe viko wazi tumepoteza
Kweli hii ndyo ilikuwa inaitwa mzik R I P wote mlioshirk kweny wimbo huuu king mwindini ngurumo mwamba
@Fiskarrr Vocals ni Muhidin Mwalimu, Hamisi Juma (RIP) na Cosmas Chidumule. Lead guitar Abel Balthazar (RIP), bass Joseph Mulenga (RIP), rhythm Abdallah Gama. Drums Habib Abbas 'Jeff'. Marijani Rajab alifariki 1992.
Magoma safi, nilikua nikwasikiza xana kipindi cha ugua pole ,hospitality ya mumbling UGUA pole
wimbo bora kwa wakati wote "oo Celina piga konde moyo utafankiwa"
Hakika ni kibao kisichochuja kitaishi milele katika muziki wa dansi
Sauti ya marehemu Muhidim Maalim "Gurumo" inasikika barabara!
Kwakweli
Ningelikuwa na uwezo ningehamrisha hizi Ngoma ziwe zikichezwa Kwa vituo vyote vya radio kutokea hapa Kenya hadi afrika kusini
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote
how can anyone dislike this?
This song reminds me of the old good times in 1979 while working at Mkunya Newala District by then
..wimbo mzuri sana siwezi kuchoka kuusikiliza pongezi kwao DDC Mlimani Park
Nyimbo zinaujumbe mzuri sana
Nimejitahidi kadiri ya uwezo wangueeeee, Wazazi wako waliniwekea vikwazo VINGI!!!!!!- Nia yangu na madhumuni yangu ilikuwa tufunge ndoa na tuishi sote kama mke na mume Celina. NYIMBO YA JANA; LEO; KESHO NA MILELE.
Ni taaaaaamu!
Kipngetich, Kenya
Namshukuru sana Mungu kwa haya maisha haijarishi nna shida ama raha kikubwa nina uzima m
Nikisikia wimbo huu, nakumbuka nyumbani mabibo,barabara ya mabibo, kabla haijajengwa. Kwa sasa mashine ya mbao. Eneo hili ilimopita barabara, mlikuwa na makaburi, mashamba ya mpunga, na miti ya miembe. Nakumbuka kampuni ya moremo ikijenga barabara ya mabibo. Wimbo, unanikumbusha mengi
maujumbe ya ajabu yanakufanya mwili usisimke!damn I love this band!
Selina kiukweli zamani raha sana
Mzee alijitugiya yy sasa dio aliyemfiya mama yetu ampe afiya
ajabu ni kwamba huu wimbo kenya haukujulikana sana. when i visited tzin november last year i was surprised to learn that it was such a big big hit from the ddc milimani park and also one of their very frst songs.
+nicholas murithi
Nyimbo nyingi za Tanzania zilikua zikivurumishwa katika radio ya Kenya,wakati huo ikiwa ni moja tu nayo ni VOK na baadae KBC.Hata huu wimbo ulikua ukichezwa ingawa sio sana.Mimi binafsi kwa mara ya kwanza niliusikia VOK miaka ya '77/78 /79 huko.
Wacha utani ndugu yangu mpendwa. Hi nyimbo ulikua moto sana hapa Kenya miaka hiyo. Pengine wewe ulikuwa hujui mambo ya miziki
asánte tzboy ukitaka kujua kwamba wewe ni mzalende kaa majuu, unanikumbusha mbali karibu na asubui yani zamaaniii RTD sita ya mchana natoka shule ya msingi korogwe huku na wahi lunch home kipoindi cha mchana mwema.abdi haibe abdisa kb sweden God bless motherland.
Moja kati ya nyimbo nzuri sana za DDC miaka hiyo ya 1978 nikiwa darasa la 5, nikisikiliza MCHANA MWEMA, RTD kupitia National 2_7_7 yenye sanduku la mbao. Walale peponi magwiji hao wa muziki wa dansi uliokuwa unaitambulisha Tz kwa aina hii ya muziki. Ooh Celina piga konde moyo, ooh Celina, tutafanikiwa ooh Celina mamah.
Nilikuwa na miaka 13 nasoma darasa la tano 1978 Nyamighadu shule ya msingi namkumbuka sana marehemu Babu yangu Lucian Ghughulu na marehemu Sabina Limingwa
Nakumbuka miaka ya 80 kukiwa na redio Moja kwa mjumbe radio Tanzania aise maisha yalikuwa Raha sana ,umoja ushirikiano
one of the great songs in Afrika
Sauti ya Comando Ngurumo, pumzika kwa amani
Nakumbuka kwa Mara kusijia wimbo ni mwaka 1995 wakati huo nk drs la 2 so mchezo selinaaaa! RTD
selina
kwakuwa imekuwa hivyo sioni sababu ya kujiua kwa ajili yangu.hoooo Celina pigs kondo moyo. ooooo Celina utafanikiwa.Ujumbe murua mama zetu walipewa
Rip kamanda Gurumo
Patricksagai5067 Sagai5067 8
INANIKUMBUSHA WAKATI MGUMU WA VITA VYA UGANDA 1979
Wanikumbusha Duli Amin Dada
Nakumbuka 1979 mwezi wa march ndio nilisikia huu wimbo kwa mara ya kwanza. Huu ulikua mwanzo wa Mlimani park Ochestra bado haijadhaminiwa na DDC.
Mzee Gurumo alikuwa DDC zamani akahamia msondo Ngoma leo Mzee ni mgonjwa sana nyumbani kwake na wana Msondo wamemtenga na wala hawana habari nae lakini huu ni mtihani wa ulimwengu hutokea kwa kila mtu lakini ushukuru kibanda ya kujihifadhi unayo na mama watoto wako anakutunza nakuombea afya njema.
Da, Mungu weeee. Nashindwa kulia au kucheka. Nakumbuka enzi hizo hapa Sikonge nikiwa na Marehemu Baba, Mama, na kaka yangu. RIP all.
Wimbo Mzuri Sana "Kikosi Cha Dhahabu DDC " , 1970s Mwishoni ,Mafunzo na Wosia Ndani Yake
Joseph Felician Lugakingira
Hatareee tupu hapo... Akina Abel bartazal,, mulenga gurumo Hamis Juma ( maalim kinyasi) na wengine kibaaaoooo
R.I.P Gurumo.... We miss you....
It was a well composed song wish up coming artist can produce such educative hits
Ujumbe mzuri sana..Hii ngoma huwa inanikumbusha TK Pub..Tukiwa na TK,Muya,Ally,Mzee Mchome,G,na wengineo..Old is gold.
Celina piga moyo konde nasilia raha sana ninaposikiliza wimbo, gitaa sauli yaani we acha 2021
Who is listening to this song* 2021
2024👋
juma kids
In 2024
2024❤
I'm really starting to like these guys Brilliant!
Selina! Wimbo unanikumbusha mbali sana. Nahisi machozi yanataka kutiririka, nimewakumbuka wengi waliotangulia mbele ya haki.
Ama...Ahsante sana kwa wimbo huu,,,,Ni wakati ule tulipokuwa vijana na sherehe kemkem...machozi nikikumbuka!
Pumzika kwa amani Mzee wetu Muhidin Gurumo kwa kweli huu muziki unanikumbusha mbali sana
Huo ni wakati amabo nyimbo zilikuwa zikiimbwa na musiki ukipigwa❤
No music were as educative as these numbers. How I wish our younger musicians can be as creative!!
Inanikumbusha miaka ya 1979 huko Kwakivesa Handeni,mkoani Tanga
Mimi natoa shukrani kubwa sana kwa msanii Diamond kwa kumtukuza mwimbaji wetu wa miziki ya kitanzania gari mpya ili imsaidie, sio hao wengine wanaomtukuza kwa maneno matupu tu bila kitu ingawa yeye ameutukuza mziki mpaka amefikia umri huu. tunamwombea umri mrefu mzee Gurumo.
MOHAMED OMAR diamond katoa gari gani mbona kituko
Huu wimbi ni true story kwa Joseph Bartholomew Mulenga ambaye alimpenda Celina lakini wazazi wake wakamwekea vigingi na Celina akataka kujiua ndiyo message halisi
Nani walipiga solo & rythm guitars maana bass najua ni Mwanyiro
Ehhh bwanee, enzi hizo ulijua unatafutiwa mwari wa kisawa, aliyekosa alikua ni mmoja, let's celebrate these amazing lyrics, it doesn't happen today
Nyimbo za kwanza baada ya kuanzishwa sikinde wananuziki wengi wakitokea dar international...utunzi wake Joseph Mulenga
Wimbo huu nimeusikia mwanzo mingi iiopita na nafurahi kuupata tena. Thanks.
nakumbuka nyumbani machozi yananimwagika ooh Home sweet home
Waimbaji katika wimbo huo ni Cosmas, Maalim Kinyasi na Gurumo, solo(Mulenga),bas(Abel),rithym(Gama),tumba(Jamwaka),sax(King Enock),hiyo timu kwa kweli haitasahaulika katika muziko wa nchi hii, mziki huu hata Kama timu yako Kulwa au Doto(Kariakoo)imefungwa wewe sikiliza Celina (Mliman) unasahau machungu yako ya kufungwa
Asante sana kaka
Da! enzi hizo ,nilikua na miaka 50, yani nakumbuka mbali sana
Acha uongo wewe
"Celina" inanikumbusha sana 1979 nikiwa mwanafunzi UDSM
Lawrence Mwakyambiki one year later(1980),my mother gave birth to me.heshima yako mzee mwakyambiki.lol
Nina meaka mmoja hapo shikamoo baba lawrence
Daa nyimboii inikumbusha mbalisana nikisikiliza adimachoziyanatoka kweliumliumeenda
jifaraja na fundisho kwa kizazi cha sasa na vijavyo. Vizur xan inapendeza.
tize boy bro,tuletee wimbo talaka ya hasira ddc mlimani.....
sauti nzuri, mungu awarehemu maalimu khamis juma kinyasi na mzee muhudin gurumo
Wimbo celina una ujumbe,burudani na ufikirishaji.
Daah nimezaliwa mwaka 1984 huu wimbo ni mzur sana
I remember those days during my school time in 1977 at ifunda technical secondary school
huu wimbo unaleta hisia sana...kiasi kwamba ukijifungia chumbani peke yako !! hunaweza chukua maamuzi magumu kiukweli...
Adam Mwanjugilo hahahahahahha
Ndongoma zng naielewa sn hii ngoma mawazo daaah nishida
Inankusha 1979 wakati huo nikiwa Tanga na watoto wenzangu pipi tunanunua sent 25, sent 50 mpaka sh 1. Maisha yalikua raha sana.
Kuna nyimbo kama izi unasikiliza na unainjoy vizuri sana
Jamal hata mimi wimbo huu unanikumbusha safari za mchana kurudi nyumbani kupata chakula cha mchana baada ya kutoka shule
Nimeishiwa maneno ndugu zangu.....
2023 still this song rocks..
Nukumbuka kwa mara kusikia wimbo ni mwaka 1982 nikiwa form two Gikumene Sec sch Meru. VOK changuo lako. Mumzike kwa amani Mr M.D.J Eddy Fundo
aisee zamani walifaidi sana
Selina,sijaona muziki Wa kulinganisha kutoka muziki Wa leo
Aisee real music
Hawa waliibeba tz kimuziki, pumzikeni mashujaa wetu
Wimbo mzr mno nakumbuka mafiki wazamani wengine sijui walipo wengine marehe pmaka sasa
Safi sana vijana mjifinze namna hii enjoy mpaka basi
Sipper old is gold
Simply....... ICONIC!!!!!!
nakumbuka nikiwa Azania high school enzi za Mwl kitukufu RIP Mwl wangu kitukufu
Rhythm iliyopigwa hapa!!!!¡❤
Tizedboy, kulikuwa na mpango kwamba zile lyrics za nyimbo zilizo kwenye ile page yako uzihamishie JAMIIFORUMS. Tafadhali kama inawezekana wasiliana na jamaa wa forum, wakupatie kisehemu na utuwekee hizi nyimbo na yale maneno yake. Thanks very much kwa kupost hizi nyimbo. Unatunza sana sehemu ya historia yetu ya Tanzania. Bod bless.
Huu ndiyo muziki wenye maadili
Yanikumbusha zile siku za mwaka wa 1979-80 tukiwa wakaazi wapya katika wilaya ya Uasin Gishu.
Daaah nyimbo hizi za zamani zilikua cimchezo
nakumbuka nyumbani Rufiji enzi hizo kila kitu bure tu utavunja mua ndizi maboga mapapai yanaoza hakuna wa kumuuzia tulikua tunakula na hakuna wa kukuuliza yani we acha tu hapa nakumbuka mbali sana.
Umeshau maji ya kujwa bure....unabisha hodi nyumba ya mtu uanomba maji unapewa haman shida.
Ulikuwa Ruwe hiyo kaka😅😅