Karibu Ufahamu Maana Halisi Ya " Utatu Mtakatifu "

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 3 ต.ค. 2024
  • Tumsifu Yesu Kristo ... Milele Amina
    Karibu Katika Channel Yetu Yenye Lengo La Uinjilishaji
    Msimuliaji : Rose James Kipeleka
    Muandaaji : Nemes Victor Michael
    Tufuatilie Hapa Zaidi
    Soma Zaidi Pia _ yesuanaokoa.bl...
    MUNGU MMOJA, NAFSI TATU (UTATU MTAKATIFU WA MUNGU)
    Nafsi ni nini?
    Kabla ya kuendelea kumjua Mungu katika nafasi tatu anazochukua yaani nafsi tatu ambazo ni Mungu Baba, Mungu mwana na Roho Mtakatifu, hebu tuangalie nini maana ya nafsi? Kwa lugha ya kigeni, neno nafsi linajulikana kama “soul’ wakati neno roho linajulikana kama “spirit”. Mungu ni Roho na wakati huo huo ni Nafsi tatu ndani ya Roho moja. Tofauti na mwanadamu ambaye ana roho, nafsi na mwili, Mungu hana mwili wa nyama na damu kama hii tuliyonayo sisi wanadamu au viumbe wengine mfano wanyama.
    Nafsi ni hisia au matamanio yanayoongoza matendo au tabia za mwili. Kwa maana nyingine, nafsi ni hisia au matamanio yanayoamua ubinadamu wa mtu. Nafsi za wanadamu zinaishi kwa kufuata matamanio ya vitu vionekanavyo kwa macho hapa duniani. Na ndio sababu mwanadamu anayeishi kwa kufuata tamaa za nafsi yake kamwe hawezi kumpendeza Mungu. Hata hivyo, roho ya mwanadamu inaishi kumpendeza Mungu ikishindana na nafsi. Hadi pale mwanadamu anapopokea neema ya kuongozwa na Roho Mtakatifu ndipo roho yake itaweza kuishinda nafsi na hivyo kuisha maisha ya kumpendeza Mungu.
    Kwa hiyo, matendo ya Mungu yamegawanyika katika makundi makuu matatu ambayo yanatufanya tumuone Mungu mmoja ndani ya nafsi tatu. Matendo hayo ndiyo tabia za Mungu. Hebu tuangalie tabia au matendo hayo ya Mungu katika nafsi tatu.

ความคิดเห็น • 1

  • @Lee-je6ge
    @Lee-je6ge 3 หลายเดือนก่อน

    Amina