TENZI NAMBA 73 YESU ZAMANI BETHILEHEMU
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 17 ม.ค. 2025
- 73. YESU ZAMANI BETHILEHEMU
1. Yesu zama Bethilehemu,
Aliyezaliwa kwa aibu,
Ndiye mwakozi wa ulimwengu,
Akaja kwa mimi.
Akaja kwa mimi; akaja kwa mimi;
Ndiye mwaokozi wa ulimwengu,
Akaja kwa mimi.
2. Yesu akafa msalabani,
Kuniponya akalipa deni,
Ni la ajabu ya jinsi gani
Kunifia mimi!
Kunifia mimi! Kunifia mimi!
Ni la ajabu ya jinsi gani
Kunifia mimi.
3. Ni yeye huyo tangu asili;
Na nilipotanga-tanga mbali
Alikuja kwa upole, kweli
Kuniita mimi.
Kuniita mimi; Kuniita mimi;
Alikuja kwa upole, kweli
Kuniita mimi
4. Yesu kristo atarudi tena,
Hilo lanifurahisha sana.
Yeye Bwana akionekana
Kunijia mimi.
Kunijia mimi, kunijia mimi,
Yeye Bwana akionekana
Kunijia mimi