Bi. Naomi Waqo: Bustani ya Kumbukumbu Mlima Kofia Mbaya ni heshima stahiki kwa waliofariki.

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 15 ก.ย. 2024
  • Mwakilishi akina mama jimbo la Marsabit Bi. Naumi Waqo ambaye pia ni mwanachama wa kamati ya bunge kuhusu michezo na utamaduni ametaka serikali ya kaunti ya Marsabit kutenga kipande cha ardhi kwa ajili ya ujenzi wa Bustani ya Kumbukumbu kuwakumbuka viongozi waliofariki katika ajali ya ndege miaka 18 iliyopita wakitafuta amani.
    Bi. Naumi amesema ajali hiyo imeiacha familia za marehemu katika hali mbaya ya kimaisha kiwango cha kuandaa harambee kuchangisha kusomesha watoto wa marehemu.
    Amesema kama mwanachama wa kamati ya bunge kuhusu michezo na utamaduni atashinikiza fedha kutengewa ujenzi huo.
    Bi Naumi amewataka wakazi wa jimbo hili kuishi kwa amani na upendo ili kutoa heshima kwa viongozi hao waliofariki katika ajali hiyo.
    Amesema viongozi hao walikuwa wakitumikia taifa hili ajali hiyo ilipotokea na kwa maana hiyo wanastahili heshima.
    Naumi amependekeza bustani hiyo kujengwa haraka iwezekanavyo.
    Ametaka siasa kutokuingizwa katika shughuli hiyo ya ujenzi wa Bustani hiyo ya Kumbukumbu na kuongeza kuwa ndoto yake ya kujengwa bustani eneo hilo sasa imetimia.
    Naibu Gavana wa Marsabit Solomon Gubo ametoa hakikisho kuwa serikali ya Kayo itashirikiana na wadau wote kufanikisha ujenzi wa Bustani hiyo ya Kumbukumbu.

ความคิดเห็น •