TCAA FUN RUN 2023
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 8 ม.ค. 2025
- TCAA iliandaa mbio za mashindano ya ridhaa “Fun Run” zilizoanzia Mlimani City na kuishia hapo zikiwa na lengo la kuhamasisha upandaji na utunzaji wa miti katika mikoa yenye ukame. Mbio hizo za kilometa 5 na 10 zilikuwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa TCAA.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ni taasisi ya umma yenye jukumu la kudhibiti sekta ya usafiri wa anga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mamlaka iliundwa kwa Sheria ya Usafiri wa Anga, Sura ya 80 (R.E 2006).
Majukumu ya kisheria ya Mamlaka ni kudhibiti masuala ya ki-usalama, ki-uchumi katika usafiri wa anga na kutoa huduma za uongozaji ndege.
Pia Mamlaka inatoa huduma za uongozaji ndege kwenye vituo vya ndege kumi na nne (14) ambavyo ni: Dar es Salaam, Kilimanjaro,Tanga, Arusha, Mwanza,Tabora,Kigoma, Dodoma, Iringa, Songwe, Songea, Mtwara, Zanzibar na Pemba