MIAKA MIWILI YA RAIS SAMIA NA MAFANIKIO YA TCAA
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 23 ม.ค. 2025
- Bodi ya Wakurugenzi , Menejimenti na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri
wa AngaTanzania TCAA inaungana na watanzania wote kumpongeza
Mheshimiwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili
madarakani. Tumeshuhudia mageuzi makubwa ya Serikali ya awamu ya sita
katika kukuza Sekta ya usafiri wa Anga Nchini.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ni taasisi ya umma yenye jukumu la kudhibiti sekta ya usafiri wa anga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mamlaka iliundwa kwa Sheria ya Usafiri wa Anga, Sura ya 80 (R.E 2006).
Majukumu ya kisheria ya Mamlaka ni kudhibiti masuala ya ki-usalama, ki-uchumi katika usafiri wa anga na kutoa huduma za uongozaji ndege.
Pia Mamlaka inatoa huduma za uongozaji ndege kwenye vituo vya ndege kumi na nne (14) ambavyo ni: Dar es Salaam, Kilimanjaro,Tanga, Arusha, Mwanza,Tabora,Kigoma, Dodoma, Iringa, Songwe, Songea, Mtwara, Zanzibar na Pemba