AHSANTE LYRICS - MERCY MASIKA & PAUL CLEMENT

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 10 ต.ค. 2024
  • 1 Wakorintho 1:9
    Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu.
    2 Wathesalonike 3:3
    Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu.
    *Mercy Masika & Paul Clement - Ahsante Lyrics
    *Lyrics By Partialyrics
    SWAHILI LYRICS
    Nauona uaminifu wako
    Katika kila jambo
    Kwa vile unavyotenda mema
    Nauona uaminifu wako
    Katika upendo wako
    Kwa vile unavyopenda
    Nauona uaminifu wako
    Katika damu yako
    Kwa vile unavyonena mema
    Naiona neema yako
    katika maisha yangu
    kwa vile umeniweka vyema
    Amani yako yatiririka
    Ndiwe unijaliaye
    kukaa vyema
    Uaminifu wako watiririkia
    Umenitia furaha moyoni mwangu
    Umeniponya magonjwa
    yangu yote
    Ewe Yesu
    Ukaukomboa uhai wangu
    na kaburi
    Ewe Yesu
    Nashukuru
    Asante kwa yaliyopita
    na ya sasa umeyatimiza
    wewe ni mwaminifu
    Asante kwa yanayokuja
    Naamini utayatimiza
    wewe u mwaminifu
    Nikitazama fadhili zako
    Ninaona fikra zako
    kwa namna unavyoniwazia
    Na nikisema hunipendi
    najidanganya mwenyewe
    Na sijaona thamani ya
    upendo wako
    Uaminifu wako watimilika
    Sababu jina lako ni mwaminifu
    Mwaminifu ni Mungu
    Mungu ni Mwaminifu
    Uaminifu wako ni wa milele
    Uaminifu wako haupimiki
    kwa njia ya matendo yangu
    Hata nikikosea haupimiki
    kwa njia ya makosa yangu
    Hata nikipatia haupimiki
    kwa njia ya kuweza kwangu
    Uaminifu wako unabaki
    (Palepale palepale palepale)
    Kwenye kiwango cha
    uaminifu wako
    Hee unabaki
    (Palepale palepale palepale)
    Asante kwa yaliyopita
    na ya sasa umeyatimiza
    wewe ni mwaminifu
    Asante kwa yanayokuja
    Naamini utayatimiza
    wewe u mwaminifu
    Uaminifu wako
    Ee Bwana
    Wadumu milele hata milele
    #paulclement
    #mercymasika
    ‪@Ambmercymasika‬
    ‪@paulclement_‬
    ‪@partialyrics‬

ความคิดเห็น • 8