HOTUBA KAMILI YA RAIS MAGUFULI AKIWA MUSOMA - 05/09/2018

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 1 ธ.ค. 2024
  • Rais Magufuli leo tarehe 05 Septemba, 2018 ameendelea na ziara yake katika mkoa wa Mara ambapo amezindua mradi wa maji safi na usafi wa mazingira wa Manispaa ya Musoma, kufungua barabara ya Simiyu/Mara - Musoma na kisha kuhutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja Mukendo Musoma Mjini.
    Katika hotuba yake Rais Magufuli ameelezea kutoridhishwa na hatua zinazochukuliwa na viongozi wa Wizara, Mkoa wa Mara na vyombo vya dola dhidi ya mfanyabiashara Nyakilang’ani ambaye amelalamikiwa na wananchi wa Mwisenge katika Manispaa ya Musoma kuwa baada ya kuuziwa hoteli ya Musoma amezuia wananchi kukatiza katika eneo hilo wanapotaka kwenda katika mwambao wa ziwa Victoria na hivyo kulazimika kuzunguka umbali mrefu.
    “Hoteli hii imechukuliwa tangu miaka 10 iliyopita, haijaendelezwa, wananchi wanakosa ajira, Serikali inakosa mapato halafu viongozi mpo mnamuangalia tu, huyohuyo Nyakilang’ani amepewa mradi wa maji wa mji wa Bunda huu mwaka wa 8 na mpaka sasa hautoi maji, viongozi mpo hamchukui hatua.
    “Sasa nataka hoteli ya Musoma iliyojengwa na Baba wa Taifa kwa nia yake njema ya kuiendeleza Musoma ichukuliwe kwa sababu ameshindwa kuiendeleza” amesisitiza Rais Magufuli.
    Rais Magufuli pia amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Mara kuwa Serikali itahakikisha inaujenga kwa kiwango cha lami uwanja wa ndege wa Musoma ili uweze kupokea ndege kubwa na ndogo, na kukamilisha ujenzi wa hospitali ya Musoma haraka ili ifanane na hadhi ya hospitali iliyopo katika Mkoa aliozaliwa Baba wa Taifa.

ความคิดเห็น • 32

  • @joelkiiru1223
    @joelkiiru1223 หลายเดือนก่อน

    John Pombe Magufuli is the greatest elected president to ever exist in known history, am always sad when I listen to his speeches but I'll still litsen and download all of them whenever they pop up.

  • @mahmoudaziz6281
    @mahmoudaziz6281 6 ปีที่แล้ว +3

    my president magufuli. nakupenda mungu ndo anajua. napenda kwenye ziara zako niuzurie lkn sina uwezo. nakufuati kupitia TH-cam.mi napenda utuongoze wewe miaka 50 tu. naisi akuna mtanzania yeyote atakae kwenda ulaya au nchi jirani kutafuta maisha.

  • @jamesngundateresia2600
    @jamesngundateresia2600 6 ปีที่แล้ว +5

    BABA DUNIA ZIMA INAKUELEWA SANA MIMI NI SHAHIDI MWAMINIFU

  • @henrysterling5133
    @henrysterling5133 5 หลายเดือนก่อน

    Mungu akuweke mahara pema😢

  • @shabanrajab3559
    @shabanrajab3559 6 ปีที่แล้ว +3

    Jamaa Yuko sawa duhh lahaja Zote anazipata duhh n

  • @joshuanjole578
    @joshuanjole578 6 ปีที่แล้ว +1

    Hongera raisi wetu

  • @donyisrich2973
    @donyisrich2973 6 ปีที่แล้ว

    Chapa kazi my prsident

  • @philipojosephlukumay3965
    @philipojosephlukumay3965 6 ปีที่แล้ว +3

    Sijui kama Watanzania wengi wanafuatilia hizi hotuba kwa umakini kama mimi🤓
    Mimi naamini rais wetu JPM ni Mungu kamleta wakati huu
    Kama kweli gesi asilimia 70 inachukuliwa maana yake huo uchumi wetu hautokaa uboreke kama tutaendelea na mifumo iliokuwepo.
    Rais wangu endelea na moto huo huo watanzania wenye akili watakuelewa tu

  • @jackhans7708
    @jackhans7708 2 ปีที่แล้ว

    Ninakukuri mzeee na nitakukubali daima

  • @jamesngundateresia2600
    @jamesngundateresia2600 6 ปีที่แล้ว +1

    Mambo ni hivi👏👏👏👏

  • @rashidiomary1324
    @rashidiomary1324 6 ปีที่แล้ว +3

    mzee Mimi nakushukuru kwa kitu kimoja mwaka huu nacho ni kutomtumbua makonda, amefanya mambo makubwa sana tangu umteue

  • @petermwenda5179
    @petermwenda5179 6 ปีที่แล้ว

    I m a respect my President

  • @jilugalamarco9308
    @jilugalamarco9308 6 ปีที่แล้ว +1

    do it and redo it tirelessly

  • @jamesngundateresia2600
    @jamesngundateresia2600 6 ปีที่แล้ว +1

    Watu kama wote good kamanda
    LUGOLA UPO BABA

  • @frankmganda116
    @frankmganda116 6 ปีที่แล้ว +1

    Hakika ninge kuwa na uwezo kila ungekuwa unatembea mikoani ningekuwa na udhuria maana hotuba zako zote zinagusa maisha ya watanzania tulio wengi asa sisi masikini hakika tunaomba uendelee kuwepo niseme nini mzee

  • @abdulrazakyussef3177
    @abdulrazakyussef3177 6 ปีที่แล้ว +1

    Baada ya second term, (ukiondoka) angaza macho ili upate Sokoine mwingine aje awe rais wa wananchi siyo wa ''wenye-inchi''

  • @trophainamagogwa9590
    @trophainamagogwa9590 6 ปีที่แล้ว +2

    Lugha zooote unajua aise unafaa kuongoza

  • @rashidiomary1324
    @rashidiomary1324 6 ปีที่แล้ว

    ili kiongozi awe bora anatakiwa aingie gerezani kwanza asote akili ndo huwa zinakaa vizuri

  • @kallahassan4896
    @kallahassan4896 6 ปีที่แล้ว +1

    baba osijali tupo pamoko

  • @rashidiomary1324
    @rashidiomary1324 6 ปีที่แล้ว +1

    watu wa musoma nyuso zao hazina stress

  • @toshindugwa1085
    @toshindugwa1085 3 ปีที่แล้ว

    Sijui wapi watanzania hawakukuelewa,ila sasa maneno yako yanaishi ulivyojitabiria mwamba

  • @habilicharles4410
    @habilicharles4410 6 ปีที่แล้ว +1

    Je ninani kama Magufuli? jibu hakunaaaaaa

  • @rashidiomary1324
    @rashidiomary1324 6 ปีที่แล้ว

    kwanza mzee ungeanza na lukuvi yeye kwa nini hakuumaliza huo mgogoro

  • @samsomkaziyoba9958
    @samsomkaziyoba9958 3 ปีที่แล้ว

    mm GI. Vi YMCA fadw

  • @leonviskb8012
    @leonviskb8012 6 ปีที่แล้ว

    Tunawahona tunawahona munakula tu ubuyu ahhn subcriber chanily yetu pls