WAZIRI MCHENGERWA: TAARIFA MUHIMU KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE, (COMBINATION 49)

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 8 ก.ย. 2024
  • #samiasuluhuhassan #wanawake
    Serikali kupitia TAMISEMI imetoa fursa kwa Wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2023 kuongeza au kufanya marekebisho ya machaguo mapya ya tahasusi (combination) baada ya kuongezwa kwa tahasusi mpya 49 kutoka 16 zilizokuwepo awali na kufanya tahasusi za kidato cha tano kufikia 65.
    Akiongea leo Jijini Dar es salaam, Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema Serikali kupitia TAMISEMI imekamilisha zoezi la awali la kuingiza kwenye kanzidata taarifa zilizo kwenye fomu za uchaguzi za Wanafunzi kama zilivyojazwa na Wanafunzi wakiwa Shuleni.
    “Napenda mtambue kuwa Mabadiliko ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023 na Mitaala ya Elimu kwa Kidato cha Tano yameanza kutekelezwa, ambapo utekelezaji huo umehusisha uanzishaji wa tahasusi mpya 49, kutoka 16 zilizokuwepo awali hadi kufikia tahasusi 65”
    “TAMISEMI inatoa fursa kwa Wahitimu kubadili machaguo ili kutoa nafasi kwa Wanafunzi kusoma combination itakayomuandaa kuwa na utaalamu stahiki katika maisha yake ya baadaye hii ni kwakuwa wakati wa ujazaji fomu za machaguo ya awali tahasusi mpya 49 hazikuwepo kwenye orodha na matokeo ya kidato hayakuwa yametoka”

ความคิดเห็น •