Kijana Dereva wa Lori Afariki Kwenye Ajali akiwa Kenya Kikazi | Boss wake Aongea kwa Uchungu Msibani

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 16 ต.ค. 2024
  • Kijana anayejulikana kwa Jina la Augustino Bruno Kindole mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa Kijiji cha Wangama Kata ya Luhota wilaya ya Iringa mkoani Iringa ambaye ni Dereva wa gari (Lori) aina FAW mali ya kampuni ya John Galt Hauliers amefariki Dunia katika ajali iliyotokea Jumapili ya Julai 21, 2024 akiwa kikazi na Lori hilo la mizigo nchini Kenya akitokea nchini Tanzania.
    Mkurugenzi wa Kampuni ya John Galt and Phoenix Hauliers ambaye pia ni Mdau wa Maendeleo wilaya ya Kilolo-Iringa, Aidan Mlawa, amefika na kushiriki mazishi ya Kijana Dereva wake anayejulikana kwa jina la Augustino Bruno Kindole (28) aliyefariki katika ajali ya gari (Lori) mali ya kampuni hiyo iliyotokea Jumapili ya Julai 21, 2024 maeneo ya Denge-Kinango (Puma Ward) nchini Kenya akiwa na mzigo kutoka nchini Tanzania.
    Mazishi ya kijana huyo (Marehemu Augustino Kindole) yamefanyika Kijijini kwao Wangama kata ya Luhota wilaya ya Iringa mkoani Iringa ambapo kampuni ya John Galt Hauliers chini ya Uongozi wa Mkurugenzi wake Aidan Mlawa ilijitoa kushughulikia na kusimamia taratibu na gharama zote za kusafirisha Mwili wa marehemu mpaka kuhakikisha umefikishwa mkoani Iringa nyumbani kwa wazazi wa marehemu.
    Akizungumza wakati wa mazishi, Aidan Mlawa amesema ameguswa na ameumizwa sana na kifo cha Mfanyakazi wake aliyekuwa akimuamini mpaka kumpa kazi kwenda nchi za nje huku akisema kuwa yeye katika kampuni yake, anazingatia sana utu wa binadamu kuliko thamani za mali ndio maana amejitoa kusimamia taratibu za kusafirisha mwili na mazishi kabla ya kuanza kuhangaikia mali zake.
    Mazishi ya Kijana huyo (marehemu Augustino Kindole) yamefanyika Julai 24, 2024 kijijini kwao katika makabuli yaliyopo Kata ya Luhota wilaya ya Iringa mkoani Iringa.
    Marehemu Augustino Bruno Kindole (28) aliyefariki katika ajali ameacha Mke na watoto wawili wadogo.
    Subscribe (Focus Digito TV) ili usipitwe na Video mpya zinazotoka kila siku.
    Focus Digito TV inakupa Maudhui Mazuri yanayohusu Habari, Elimu, Mitindo ya maisha, Michezo na Burudani.
    Focus Digito TV is here to provide you with contents about News, Education, Lifestyles, Sports and Entertainments.
    #FocusDigitoTV
    ..................
    Tufuatilie Zaidi kupitia:
    INSTAGRAM, TIKTOK, FACEBOOK, TWITTER (X), THREADS NA GOOGLE WEBSITE YETU YA FOCUS DIGITO TV
    Focus Digito TV is one of the best info-edu-tainment Online Media conveying contents for the Public Interest.
    Asante kwa kuchagua kutufuatilia | Thanks for Subscribing
    We Love You | Tunakupenda
    Regards
    Team FocusDigitoTV

ความคิดเห็น • 9