KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA MORNING GLORY: THE SCHOOL OF HEALING: 18/ 07/ 2024

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 29 ส.ค. 2024
  • KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA MORNING GLORY: THE SCHOOL OF HEALING: 18/ 07/ 2024
    SEMINA YA NENO LA MUNGU:
    MADA:
    "HOFU YA MABADILIKO"
    (FEAR OF CHANGE)
    SOMO LA LEO:
    WATU WA AINA YA PILI AMBAO WANAWEZA KUKUUNGANISHA NA
    MFUMO WA KIMAONO.
    ( VISION CONNECTORS - TYPE TWO)
    Mwanzo 45 : 1 - 15
    Esta 5 : 9 - 14
    NENO KUU:
    "UTABARIKIWA UINGIAPO, UTABARIKIWA NA UTOKAPO"
    KUMBUKUMBU LA
    TORATI 28 : 6
    &
    Yohana 12 : 24
    24 Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.
    MAANDIKO YA LEO:
    Mwanzo 45 : 1 - 15
    1 Hapo Yusufu hakuweza kujizuia mbele yao wote waliosimama karibu naye. Akapiga kelele, na kusema, Mwondoeni kila mtu mbele yangu. Wala hakusimama mtu pamoja naye, Yusufu alipojitambulisha kwa nduguze.
    2 Akapaza sauti yake akalia, nao Wamisri wakasikia. Watu wa nyumba ya Farao nao wakasikia.
    3 Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ndimi Yusufu; baba yangu angali hai bado? Wala ndugu zake hawakuweza kumjibu, maana waliingiwa na hofu mbele yake.
    4 Yusufu akawaambia ndugu zake, Karibuni kwangu; basi, wakakaribia. Akasema, Mimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri.
    5 Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu.
    6 Maana miaka hii miwili njaa imekuwa katika nchi, na iko tena miaka mitano isiyo na kulima wala kuvuna.
    7 Mungu alinipeleka mbele yenu kuwahifadhia masazo katika nchi, na kuwaokoa ninyi kwa wokovu mkuu.
    8 Basi si ninyi mlionipeleka huku, ila Mungu; naye ameniweka kama baba kwa Farao, na bwana katika nyumba yake yote, na mtawala katika nchi yote ya Misri.
    9 Fanyeni haraka, mmwendee baba yangu, mkamwambie, Hivi ndivyo asemavyo mwanao Yusufu, Mungu ameniweka kuwa bwana katika Misri yote, basi unishukie, usikawie.
    10 Nawe utakaa katika nchi ya Gosheni, utakuwa karibu nami, wewe, na wanao, na wana wa wanao, na wanyama wako, ng'ombe zako, na yote uliyo nayo. Nami nitakulisha huko;
    11 maana bado imesalia miaka mitano ya njaa; usije ukaingia katika uhitaji, wewe, na nyumba yako, na yote uliyo nayo.
    12 Na tazama, macho yenu yanaona, na macho ya ndugu yangu Benyamini, ya kwamba ni kinywa changu mimi kinachosema nanyi.
    13 Nanyi mtamwarifu baba yangu habari za fahari yangu yote katika Misri, na za vyote mlivyoviona; mkafanye haraka kumleta huku baba yangu.
    14 Akaanguka shingoni mwa ndugu yake Benyamini, akalia; Benyamini naye akalia shingoni mwake.
    15 Akawabusu ndugu zake wote, akalia nao, baada ya hayo, nduguze wakazungumza naye
    Esta 5 : 9 - 14
    9 Basi Hamani alitoka siku ile kwa furaha na ukunjufu wa moyo; lakini Hamani alipomwona Mordekai mlangoni pa mfalme, ya kwamba hasimami wala kutetemeka mbele yake, alijaa ghadhabu juu ya Mordekai.
    10 Walakini Hamani akajizuia, akaenda zake nyumbani kwake; akatuma kuwaita rafiki zake na Zereshi mkewe.
    11 Naye Hamani akawasimulia habari za fahari ya mali zake, na wingi wa watoto wake, nayo mambo yote pia ambayo mfalme amemfanikisha katika hayo, na jinsi alivyompandisha juu ya maakida na watumishi wa mfalme.
    12 Zaidi ya hayo Hamani akasema, Naye malkia Esta hakumkaribisha mtu ye yote pamoja na mfalme katika karamu aliyoiandaa, ila mimi peke yangu; hata na kesho pia nimealikwa naye pamoja na mfalme.
    13 Bali haya yote yanifaa nini, pindi nimwonapo yule Mordekai, Myahudi, ameketi mlangoni pa mfalme?
    14 Basi Zereshi mkewe akamwambia, na rafiki zake wote, Na ufanyizwe mti wa mikono hamsini urefu wake, na kesho asubuhi useme na mfalme ili Mordekai atundikwe juu yake; ndipo utakapoingia kwa kicheko pamoja na mfalme karamuni. Basi neno likampendeza Hamani, akaufanyiza ule mti.

    Mhubiri: Rev. Dr. Eliona Kimaro
    Kwa maombi na ushauri :
    Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
    Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
    Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
    Simu: +255 713 553 443
    TH-cam: Kijitonyama Lutheran church
    Barua Pepe: Kijitonyamalutheran@gmail.com

ความคิดเห็น • 23

  • @roseasimwe827
    @roseasimwe827 หลายเดือนก่อน

    Ubarikiwe sana mchungaji Eliona Kimaro, Mwenyezi Mungu aendelee kukutumia

  • @judithabuko6006
    @judithabuko6006 หลายเดือนก่อน

    Adui zangu watanivusha katika jina la Yesu Kristo aliye hai

  • @JoshuaHilgath
    @JoshuaHilgath หลายเดือนก่อน

    MUNGU YUPO PAMOJA NAMI AMINA 🙏🙏🙏🙏

  • @neemamushi9675
    @neemamushi9675 หลายเดือนก่อน

    Ameeeeen

  • @jeremiaisowe4443
    @jeremiaisowe4443 หลายเดือนก่อน

    Amen

  • @mamatriplee5638
    @mamatriplee5638 หลายเดือนก่อน +2

    Namuombea Rafiki yangu Upendo mporaa anajua kubeba jambo la mtu kwa moyo mmoja. Mungu wa Mbinguni akazidi kumuinua.

  • @user-vb5dl7qq4o
    @user-vb5dl7qq4o หลายเดือนก่อน

    Amen🙏🏻🙏🏻🙏🏻

  • @judithabuko6006
    @judithabuko6006 หลายเดือนก่อน

    Ameeeen👏👏👏👏👏

  • @elias-op3mx
    @elias-op3mx หลายเดือนก่อน +3

    Ameeni mchungaji wetu mungu akulinde kwajili yetu wengi tunamatumaini nawewe

  • @miriamalute1540
    @miriamalute1540 หลายเดือนก่อน +1

    Ameen

  • @nakky379
    @nakky379 หลายเดือนก่อน

    Leo umenihubiria mim mwanzo mwisho, nawavusha marafk zng ila mm sasa napitaga njia za panya ili kutoboa yan yan😢 ila i know my God he is on the way for me, yan Mungu lazma atanionekania kama Yusuph miaka yang iliyoliwa na nnzige itarudishwa.

  • @AliceHatibu
    @AliceHatibu หลายเดือนก่อน +1

    Amen 🙏 🙏 🙏 🙏

  • @JemimaMalaika
    @JemimaMalaika หลายเดือนก่อน +1

    Ameeen naamini na mm nitavuka maan mm nilifanyika dalaj la watu kuvuka

  • @Madam255
    @Madam255 หลายเดือนก่อน +1

    Ameen and Ameeen

  • @hildagrant3802
    @hildagrant3802 หลายเดือนก่อน

    Nalifurahi Kwa kuwa naliteswa

  • @elyhillary2000
    @elyhillary2000 หลายเดือนก่อน +1

    Ameeeeeeeniii

  • @judithabuko6006
    @judithabuko6006 หลายเดือนก่อน

    Ahsante Yesu ahsante Mungu kwa ajili ya adui zangu nawaombea sana maisha marefu

  • @elias-op3mx
    @elias-op3mx หลายเดือนก่อน +1

    Namimi nimewashika mikono wengi nawanamafanikio makubwa kupitia mimi lakini mimi sijawai kua na mafanikio ya fulaha namimi nikama dalaja lawatu kuvuka ilasuo mimi kulivuka mchungaji lakini yote nimipango ya mungu

  • @user-ek3rs8km4k
    @user-ek3rs8km4k หลายเดือนก่อน

    Kila siku kila saa u mwaminifu Bwana

  • @roseasimwe827
    @roseasimwe827 หลายเดือนก่อน

    Ubarikiwe sana mchungaji Eliona Kimaro, Mwenyezi Mungu aendelee kukutumia

  • @NasraSaidi-dq7fh
    @NasraSaidi-dq7fh หลายเดือนก่อน

    Ameeeeen

  • @user-dr6hf7lx4g
    @user-dr6hf7lx4g หลายเดือนก่อน +1

    Amen🙏🙏

  • @matildamwakatuma1206
    @matildamwakatuma1206 หลายเดือนก่อน

    Amen