"HAKUNA MAHALI KATIBA INASEMA WATU WAOMBE KIBALI CHA KUANDAMANA" OLENGURUMWA AFAFANUA KIUNDANI

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 21 ก.ย. 2024
  • Mratibu kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Wakili Onesmo Olengurumwa ametoa ufafanuzi juu ya Haki ya kuandamana kwa raia katika nchi yao.
    Wakili Olengurumwa anatoa ufafanuzi huu ikiwa ni katika wakati ambao jeshi la Polisi limetoa tangazo la katazo la maandamano ya amani yaliyopangwa kufanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mnamo 23 Sept 2024.
    Wakili Olengurumwa amesema katiba inatoa Haki kwa raia kuandamana kwa amani ikiwa ni sehemu ya kuonesha au kupaza sauti juu ya mambo ambayo waandamanaji hawaridhiki nayo au kupongeza yale yaliyowaridhisha.
    “katiba yetu imeelekeza waandamanaji kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi kwa barua kwamba siku Fulani tunapanga kuandamana katika eneo Fulani na Fulani kwa hiyo tunaomba jeshi la Polisi wawepo kwa ajili ya kutulinda” amesema Wakili Olengurumwa.
    “Kwa hiyo watanzania waelewe kwamba Maandamano hakuna mahali popote unapotakiwa Kwenda kuomba kibali ili uandamane,yawe ni yale maandamano ya ghafla au yawe yale maandamano ya kupanga, hakuna mahali unapaswa Kwenda kuomba kibali, ni ambayo iko moja kwa moja” ameongeza Olengurumwa.
    Chadema wametangaza kufanya maandamano yao ikiwa ni sehemu ya kuishinikiza serikali kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya utekaji na mauaji ya wanachama wao ,vitendo ambavyo wanashikiza kupata majibu nah atua zilizochukuliwa mpaka sasa.

ความคิดเห็น • 1

  • @suwedwakil4392
    @suwedwakil4392 ชั่วโมงที่ผ่านมา

    Hata kiingereza hujui