BREAKING: IGP SIRRO AMPANDISHA CHEO ALIYETOA WAZO LA KITUO..

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 17 ก.ย. 2024
  • BREAKING: IGP SIRRO AMPANDISHA CHEO ALIYETOA WAZO LA KITUO..
    Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) nchini Tanzania, Simon Sirro amempandisha cheo Christina Onyango kuwa mkaguzi msaidizi wa Polisi. Awali Christina alikuwa konstebo.
    Hivi karibuni Christina alitunukiwa shahada ya udaktari katika Chuo Kikuu cha Lead Impact kilichopo Marekani kutokana na utendaji wake.
    Askari huyo alitoa wazo la kuanzishwa kituo cha huduma ya pamoja kati ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam na taasisi nyingine za Serikali zinazojishughulisha na masuala ya kupinga ukatili wa kijinsia ambacho kipo katika Hospitali ya rufaa ya Amana manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam.
    Machi 11, 2020, IGP Sirro alimpongeza kwa barua na kumpandisha cheo kuwa mkaguzi msaidizi wa polisi na kumuelekeza Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kumvalisha cheo kipya.
    Leo Alhamisi Machi 26, 2020, Kamanda Mambosasa amemvalisha cheo Christina na kumpongeza kwa kuliwakilisha jeshi hilo vizuri katika jamii.
    UNA HABARI? WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE
    ( +255 784 888982)
    ( +255 676 229628)
    Email: globaltvbest@gmail.com
    abbymrisho@gmail.com
    HABARI MPYA DAILY:
    bit.ly/habarimpya
    HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA:
    bit.ly/mikasa_y...
    GLOBAL RADIO TV:
    bit.ly/255globa...
    EXCLUSIVE INTERVIEW:
    bit.ly/exclusiv...
    Subscribe Global TV, Channel itakayokupa Habari na matukio ya kipekee nchini Tanzania
    Subscribe bit.ly/globaltv...

ความคิดเห็น • 23