Mimi ninaweza kukusamehe dhambi zako? HD 1080p
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 16 ธ.ค. 2024
- Yoh 20:22-23
Wakristo wanamamlaka ya kusamehe dhambi?
Kwanza; Nani anasamehe dhambi kwa msingi wa Biblia
Maana ya aya hizi basi ni nini?
Nani anasamehe dhambi?
Zaburi 32:1-5
Zaburi 103:2-3
Marko 2:4-7
MUNGU PEKE YAKE ANASAMEHE DHAMBI!
Maana ya Yoh 20:23 ni nini basi?
Kwanza tuangalie dhambi katika mukhtada huo ni nini hasa
Yohana 15:22-24, 16:9
Dhambi husika ni kutokumwamini Yesu kama alivyo dihirishwa katika Biblia na hasa Agano jipya au Injili.
Yohana 3:19, 12:44-50
Sasa tunajua hasa ni dhambi ani inayohusika hapa
Vipi basi Tunasamehe dhambi au kumfunga mtu katika dhambi zake kwa vipi?
Tunapo eneza Injili na mtu anaposikia anapata changamoto ya kuikubali au kuikataa
Akukubali, anaungama dhambi anampokea Yesu kama mwaokozi wake na sisi kama wakilishi wa Injili tunaweza kumtangazia ”Umesamehewa dhambi zako” tunaweza kufanya hivyo kwa msingi wa neno la Mungu.
Ni Mungu anamsamehe ila sisi tunataarifia hhiyo habari
Ikiwa mtu hyo anakataa kupokea Injili, kutubu na kumkubali Yesu.
Pia kama wakilishi wa Injili tunaweza kumwambia matokeo yake, anabaki (kufungwa) katika dhambi zake
Kwa hiyo sisi kufunga au kufungua mtuu ni matokeao ya kueneza Injili siyo sisi tunaamua kufanya kama tunavyojisikia.
Yohana 20:22-23
22Alipokwisha sema hayo, akawapulizia na kuwaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu.
23Mkiwasamehe watu dhambi zao, wamesamehewa; msipowasamehe, hawasamehewi.”
Zaburi 32:1-5
1 Heri aliyesamehewa dhambi,
Na kuondolewa makosa yake.
2 Heri ambaye BWANA hamhesabii hatia,
Na ambaye rohoni mwake hamna hila.
3Nilipokosa kuungama dhambi zangu, mifupa yangu ilipooza
Kwa kulia kwangu mchana kutwa.
4Kwa maana mchana na usiku
Mkono wako ulinilemea.
Jasho langu likakauka hata nikawa
Kama nchi kavu wakati wa kaskazi.
5 Ndipo nikakuungamia dhambi yangu,
Wala sikuuficha upotovu wangu.
Nilisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA,
Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.
Zaburi 103:2-3
2Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA,
Wala usizisahau fadhili zake zote.
3 Akusamehe maovu yako yote,
Akuponya magonjwa yako yote,
Marko 2:4-7
4Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kulivunja wakaliteremsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza. 5Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako. 6Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao, 7 Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye
Mungu?
Yohana 15:22-24
22Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana kisingizio kwa dhambi yao. 23 Yeye anichukiaye mimi humchukia na Baba yangu. 24 Kama nisingalitenda kwao kazi asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia.
Yohana 16:7-9
7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitamtuma kwenu. 8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu. 9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi;
Yohana 3:19
19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.
Yohana 12:44-50
44 Naye Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenituma. 45 Naye anitazamaye mimi amtazama yeye aliyenituma. 46 Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani. 47 Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu. 48 Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho. 49Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenituma, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema. 50 Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo.
Asante Sana nashukuru Mwalimu kwa ufafanuzi Bora, ubarikiwe Sana
👍🙏karibu
Mungu akubariki mwalimu.
🙏