RAIS DKT. MAGUFULI AKAGUA MAGARI YA JESHI YATAKAYOTUMIKA KUSAFIRISHA KOROSHO

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 9 พ.ย. 2018
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 10 Novemba, 2018 amekagua magari ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyoandaliwa kwa ajili ya kubeba korosho za wakulima endapo wanunuzi binafsi hawatatii maagizo ya Serikali ifikapo Jumatatu tarehe 12 Novemba, 2018 saa 10:00 Jioni.
    Mhe. Rais Magufuli amefanya ukaguzi huo katika Kambi ya Jeshi ya Twalipo, Kikosi cha Usafirishaji cha 95KJ Mgulani Jijini Dar es Salaam ambapo magari 75 yenye uwezo wa kubeba tani 1,500 kwa mpigo yameandaliwa kwa ajili ya kubeba korosho katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani na Tanga.
    Akizungumza na Maafisa na Askari wa JWTZ waliokuwepo wakati wa ukaguzi huo, Mhe. Rais Magufuli amesema endapo wanunuzi binafsi hawatatii maagizo ya Serikali ya kununua korosho za wakulima kwa bei isiyopungua shilingi 3,000 kwa kilo sambamba na kutii agizo lililotolewa jana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, hakuna mnunuzi yeyote atakayeruhusiwa kununua korosho na Serikali itachukua hatua ya kutumia JWTZ na Bodi ya Mazao Mchanganyiko kununua korosho zote za wakulima kwa bei ya zaidi ya shilingi 3,000 kwa kilo.
    Mhe. Rais Magufuli amebainisha kuwa baada ya kununua korosho, Serikali itatafuta soko na korosho nyingine zitabanguliwa kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi.
    “Nataka kuwahakikishia wakulima wa korosho Serikali ipo na itaendelea kuwapigania, ikifika Jumatatu saa 10:00 jioni, hawa wanunuzi binafsi hawajajitokeza na kueleza watanunua tani ngapi, Serikali itanunua korosho zote na fedha za kununulia zipo” amesema Mhe. Rais Magufuli.
    Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali inalazimika kuchukua hatua hizi baada ya wanunuzi binafsi kufanya mgomo wa kununua korosho kwa kusuasua licha ya kufanya nao mazungumzo na kufikia makubaliano tarehe 28 Oktoba, 2018 Jijini Dar es Salaam.
    Katika mazungumzo hayo Serikali iliungana na msimamo wa wakulima wa korosho wa kukataa bei ya kati ya shilingi 1,900 hadi 2,700 kwa kilo, na hivyo kukubaliana kuwa korosho zitanunuliwa kwa bei isiyopungua shilingi 3,000 kwa kilo.
    Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na kufikiwa kwa makubaliano hayo wanunuzi binafsi wameendelea kutotii kwani kati ya kampuni 37 zilizoomba kununua korosho ni kampuni 14 tu ndizo zimejitokeza na ununuzi unafanyika kwa kusuasua.
    “Nimefurahi sana kwamba Jeshi letu la Ulinzi Tanzania lipo tayari kufanya operesheni hii na tunaweza kuiita OPERESHENI KOROSHO, nimeambiwa kuwa kuna takribani tani 210,000 za korosho, kule Lindi na Mtwara kuna maghala yanayoweza kuhifadhi tani 77,000 na hapa Dar es Salaam kuna maghala yanayoweza kuhifadhi zaidi ya tani 90,000 pamoja na maghala mengine, natarajia kuona zoezi hili linakamilika haraka.
    “Na kutokana na jambo hili, sasa JWTZ kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ianze kufikiria kuanzisha kiwanda kikubwa cha kubangua korosho, hata kama itakuwa ni kwa Serikali kutoa fedha za kujenga kiwanda hicho, tuanze kuachana na uuzaji wa korosho ghafi, huo ni utumwa, tuwe na viwanda vyetu na vijana wetu wapate ajira” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
    Mapema akitoa taarifa ya maandalizi ya kutekeleza jukumu hilo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen. Venance Mabeyo amesema JWTZ imetayarisha magari ya uwezo tofauti 75 yenye uwezo wa kubeba jumla ya tani 1,500 kwa mpigo na kwamba tani nyingine 500 zitabebwa na meli ya kijeshi (Landing Craft) ambayo inaweza kutia nanga mahali popote katika ufukwe wa bahari.
    “Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu tupo tayari kutekeleza jukumu hili” amesema Jen. Mabeyo.

ความคิดเห็น • 342

  • @mohamedkilemile3058
    @mohamedkilemile3058 5 ปีที่แล้ว +12

    Kama unakubali JPM ni Konki, Konki, Konki master, gonga like hapa.

  • @edsonlaurencemwagamasasi9074
    @edsonlaurencemwagamasasi9074 5 ปีที่แล้ว +42

    Mungu libariki Jeshi la wananchi la TANZANIA... Mungu ibariki Tanzania... Ameeeeeeen.... love you so much TANZANIA my beloved Country... my Proud of mother Land

    • @richard.rkilonzo7538
      @richard.rkilonzo7538 5 ปีที่แล้ว +1

      Jeshi la Tanzania safi sana. Ushauri wangu ni gharama sana kutumia magari ya Jeshi kusomba korosho. Utatumia mafuta mengi sana na watu watafanya deal kwenye mafuta. Mimi kama mwenyeji wa East Afrika tunajijua. Wataiba mafuta utafukuza kila mtu. Fuata ushauri wa MP Bashe sijajua wa wapi wafanya biashara wanunue korosho kwa bei ta 2700/= Tanzanian shillings Serekali ichangie ile 300/= Tanzania shillings inabakia. Huyu Bashe alitakiwa azaliwe Kenya. Anajua Hesabu sana.

    • @edsonlaurencemwagamasasi9074
      @edsonlaurencemwagamasasi9074 5 ปีที่แล้ว

      Ninaimani mkuu wa nchi kajipanga katika hilo....

    • @enockchasama4644
      @enockchasama4644 5 ปีที่แล้ว +1

      Edson Laurence Mwagamasasi yukosawa mweshimiwa

  • @Saintman1966
    @Saintman1966 5 ปีที่แล้ว +39

    Hiv ndivyo inavyotakiwa katk taifa kuw na msimamo chany kwa ajili ya wananchi mungu ibarik Africa mungu ibariki tanzania na serikali na majeshi yetu wananchi tupo nyuma yenu

    • @barakaraymond3542
      @barakaraymond3542 5 ปีที่แล้ว +1

      Nafurahi sana kuona utayari wa Jeshi langu kuwasaidia wananchi MUNGU awatangulie katika kaz hii ya ujenzi wa taifa

    • @Saintman1966
      @Saintman1966 5 ปีที่แล้ว

      @@eliyawilliammagesamarwa8413 hakikaaa kweli inabid tuzid kukesha na kumuombea rais wetu kwa pamoja azid kutupigania

  • @modestusndunguru4479
    @modestusndunguru4479 5 ปีที่แล้ว +19

    safi Sana rais wetu..... hapa kazi tuuu .....nimeamin rais wetu hataki masihara kwenye maisha ya watu.... good good... goooooooooodddd..... awamu hiii rais.. tunae hadi rahaa

  • @dr.hamiduibrahim1307
    @dr.hamiduibrahim1307 5 ปีที่แล้ว +37

    Tukiacha masuala ya kisiasa, huyu ni Rais wa viwango vya hali ya juu kuwahi kutokea barani Africa kwa miaka ya hivi karibuni.
    Kikubwa ni sisi wenyewe kumuunga mkono katika vita hii ya ki uchumi maana ni ngumu kuliko vita ya mtutu wallah. Ila Binafsi nafsi yangu ni nyeupe kabisa kwa huyu jamaa..
    Mungu Ibariki Africa Mungu Ibariki Tanzania mungu yabariki majeshi yetu matiifu. 🙏🙏🙏

    • @saidpalamsemaukwelilazimaa814
      @saidpalamsemaukwelilazimaa814 5 ปีที่แล้ว +1

      Me napendanga huwa hasomi .yani yanatoka pale pale.

    • @robertmichael8023
      @robertmichael8023 5 ปีที่แล้ว

      Dr. Hamidu Ibrahim 🙏

    • @zefamange7281
      @zefamange7281 5 ปีที่แล้ว

      Sanaaaa

    • @sambobby4387
      @sambobby4387 2 ปีที่แล้ว

      i guess Im asking the wrong place but does any of you know a method to get back into an Instagram account??
      I stupidly lost my account password. I love any assistance you can offer me.

  • @sylvestrengwelu2012
    @sylvestrengwelu2012 5 ปีที่แล้ว +1

    Thanks, Thanks for your proper understand and so for your heartily support and poor people as well.

  • @DrFatmaKhanPanAfrikan
    @DrFatmaKhanPanAfrikan 5 ปีที่แล้ว +15

    Baada ya Korosho, Tanzanite, Almasi, Dhahabu na Gesi tupate FEDHA ZA HARD CURRENCY.

  • @mwamengele
    @mwamengele 5 ปีที่แล้ว +26

    Huyu ndio Konki Master Mkuu

  • @Tino_Official_tz
    @Tino_Official_tz 5 ปีที่แล้ว +36

    Naipenda nchi yangu nalipenda Jeshi langu. Kuwa mwanajeshi ulikuwa ndoto yangu💥🔥💥

    • @erickkomba4465
      @erickkomba4465 5 ปีที่แล้ว

      Mungu akubariki Rais JPM tuko pamoja.

    • @miketimejah4280
      @miketimejah4280 5 ปีที่แล้ว

      Augustine Ernest Tino uko kikosi gani

    • @shadowmedia7644
      @shadowmedia7644 5 ปีที่แล้ว

      Augustine Ernest Tino kama mim ndugu Yang

  • @abeidmayanga809
    @abeidmayanga809 5 ปีที่แล้ว +18

    mzee magu nina laki moja yakukupa sasa mtume kijana wako yeyote ajeachukue safi safi sanaa

    • @255LK
      @255LK 5 ปีที่แล้ว

      Abeid Mayanga angalia usitafutwe na vibaka wakajifanya wawakilishi wa JPM😂🤣🤣🤣🤣🤣😂😂🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣😂

    • @jamilmwinge3695
      @jamilmwinge3695 5 ปีที่แล้ว

      😁😁😁

    • @shannymrope6225
      @shannymrope6225 5 ปีที่แล้ว

      Na ww laki moja yako lete ulipe watu pesa za korosho ,wengi hatujalipwa hali mbaya nyie mnamsifia ss tunaumia tu

  • @frankmadulu9514
    @frankmadulu9514 5 ปีที่แล้ว +4

    Sijapata bahati ya kukupa mkono kwa kazi nzuri unazozifanya! ila naomba ukiiona comment yangu nipate hiyo fursa ! wasiokuelewa watapata tabu sana! Mungu akulinde! baba

  • @reonaldmichaeli3525
    @reonaldmichaeli3525 5 ปีที่แล้ว +32

    Hilo zoezi likikamilika anza zoezi la kununua dhahabu na almasi na kutunza kwenye mabenki wamezoea kutuchezea kwa muda mrefu sana ,pia ni moja ya kupanua uchumi wa inchi na ajira kwa vijana

  • @josiajacob4911
    @josiajacob4911 5 ปีที่แล้ว +9

    mungu akubariki rais wetu ...hakika tungekupata muda mrefu tungefika mbali sana mm niko tayar kukusaidia kaz yyote bila malipo

  • @salummasoud5778
    @salummasoud5778 5 ปีที่แล้ว +25

    Huyu Rais angeiongoza hii Nchi Mara tu baada ya Uhuru tungekuwa mbali sana kiuchumi.

    • @isayamax4476
      @isayamax4476 5 ปีที่แล้ว +2

      Mungu ibariki Tanzania..mungu m'bariki Magufuli..amen

    • @ibrahimumombasa9474
      @ibrahimumombasa9474 5 ปีที่แล้ว

      Kila mtu na kipindi chake na wakati wake.

    • @magoshaclement3088
      @magoshaclement3088 5 ปีที่แล้ว

      Usifananishe korosho na ukoloni . Each History should be judged according to its age and impartiality... Kwa kifupi umemtusi Nyerere. Ingawa kila mtu sisi wanahistoria tunamheshimu

    • @zefamange7281
      @zefamange7281 5 ปีที่แล้ว +1

      Nilikua namwona nyerere alikuwa raisi bora kumbe magu ndie raisi bora kuliko

    • @salummasoud5778
      @salummasoud5778 5 ปีที่แล้ว

      Zefa Mange Sote tusubiri 2025 tutapata jibu sahihi ya swali lako.

  • @MichaelPaulTZ
    @MichaelPaulTZ 5 ปีที่แล้ว +30

    Wafanyabiashara w Korosho walikuwa wanabeep sasa wamepigiwa.
    Cha msingi tujenge viwanda vya kubangua korosho vya kisasa.

    • @manyotaskipper5765
      @manyotaskipper5765 5 ปีที่แล้ว +2

      Mzee baba kwa mwendo huu vitajengwa tu Viwanda MAGU HAJAJA IKULU KWA UDHAMINI WA WAFANYA BIASHARA NDOMANA HAWAOGOPI

  • @SabosoR
    @SabosoR 5 ปีที่แล้ว +26

    niko tayari kujitolea kuendesha gari ktk zoezi hili iwapo mtahitaji madereva wa akiba

    • @stevenrameck6179
      @stevenrameck6179 5 ปีที่แล้ว +2

      Saboso Rufomoka magufur rais wetuuu jamaan mungu akup miak ming saaan ongoz mpank uzehek ndoo usitaf nakukubar

    • @DrFatmaKhanPanAfrikan
      @DrFatmaKhanPanAfrikan 5 ปีที่แล้ว +2

      AlHaamduLILLAH
      Maa-Shaa-Allah
      UBaarikiwe sana ndugu

    • @hamzabingwe4178
      @hamzabingwe4178 5 ปีที่แล้ว

      Saboso Rufomoka😀😀😀😀😀😀😀😀

    • @veronikadalali7251
      @veronikadalali7251 3 ปีที่แล้ว

      Aaaaaaaah' pole yako

  • @hoseazakayo3779
    @hoseazakayo3779 5 ปีที่แล้ว +3

    Jeshi letu la wananchi wa Tanzania liko vizuri Sana linapendeza MUNGU bariki Jeshi letu MUNGU bariki Tanzania ♥♥

  • @neemajoshuaer9562
    @neemajoshuaer9562 5 ปีที่แล้ว +11

    Saf sana Mungu aendelee kukubariki Rais wetu azidi kukupa ujasiri

    • @thaubannaftali1439
      @thaubannaftali1439 5 ปีที่แล้ว

      Neema huyu jamaa ni jembe

    • @jamesluke2446
      @jamesluke2446 5 ปีที่แล้ว

      Piga kazi baba jwtz wiiiiiiii

    • @ramarsalehe8332
      @ramarsalehe8332 5 ปีที่แล้ว

      Neeema

    • @faidaemmanuel60
      @faidaemmanuel60 5 ปีที่แล้ว

      Neema Joshuaer gud

    • @ellykimu9288
      @ellykimu9288 5 ปีที่แล้ว

      hata mbinguni hakuna mzaha ukihasi na usanii your deleted. magufuli dont fear any one show us the way

  • @jaffaribori443
    @jaffaribori443 5 ปีที่แล้ว +6

    Hayo ndio maneno, KWANZA KOROSHO HAZILIWI NA WADUDU HILO ZAO NIKAMA HASALI AU TENDE, nunu weka ndani tutauza mwakani hata mwaka wa kesho na ikiwa ni hasara sawa kwani hasara haikuwanza leo.

  • @jonasamos555
    @jonasamos555 5 ปีที่แล้ว +24

    Hii ni zawadi Kutoka kwa Mungu

    • @mohamedikaesa2601
      @mohamedikaesa2601 5 ปีที่แล้ว +1

      Hakuna. wakufanana. naraisi. huyu
      mwenye.huruma..mchapakazi
      mwadilifu. habagui. hachagui
      mungu. mbariki. Sana. sana
      nimkombozi. Wetumpka.
      Daima.magufuli.woeeeeeeeee

  • @alphoncesendama9607
    @alphoncesendama9607 5 ปีที่แล้ว +30

    mmmmmhu hiiii Kali toka nmekua hiii naona mpya mzeee baba hatishiki na wauza uza

    • @neemajoshuaer9562
      @neemajoshuaer9562 5 ปีที่แล้ว +1

      Wanaleta mgomo baridi sasa wamekutana na chuma

    • @DrFatmaKhanPanAfrikan
      @DrFatmaKhanPanAfrikan 5 ปีที่แล้ว +3

      KAMWE, HATISHIKI NA HATOTISHIKA MWENYE-ENZI-ALLAH-SUBHANA-MLEZI YUKO PAMOJA NA WAKWELI.

    • @jaykillermsodoki1386
      @jaykillermsodoki1386 5 ปีที่แล้ว +1

      @@neemajoshuaer9562 watapata tabu sana

    • @jaykillermsodoki1386
      @jaykillermsodoki1386 5 ปีที่แล้ว

      @@neemajoshuaer9562 0788796943 nitafute plz

    • @neemakilomoni4258
      @neemakilomoni4258 5 ปีที่แล้ว +1

      Alphonce Sendama ya kawaida tu kwa mtu muelewaji na mwenye kujiamini kwa utetezi wa raia wanyonge na nchi yake unyanya saji wa wakulima wa korosho umekwisha sasa

  • @jamesngundateresia2600
    @jamesngundateresia2600 5 ปีที่แล้ว +22

    Mzee wa kazi huwaga sikupatii picha wewe ni zaidi ya kifaru

  • @amedeusmassawe5685
    @amedeusmassawe5685 5 ปีที่แล้ว +4

    Kanyaga twende Mzee hiyo ndyo sura yako ya kazi tunayo ifahamu

  • @dicksonaroka6961
    @dicksonaroka6961 5 ปีที่แล้ว +38

    Ukisikia Tanzania wamempata Konki master sasa ndo hawamu hiii hakuna kudekezana iwe isiwe...... mungu akupe uzima uzid kuikomboa Tanzania yetu.

  • @maazamdungwa3326
    @maazamdungwa3326 5 ปีที่แล้ว +7

    Huyu ni rais wa aina yake haijawahi kutokea tz,,yuko tayar inch ifirike ila tu kwa ajiri ya wanyonge,,mungu anakuona jpm na akuongoze kwa mipango yako

    • @vicentshimiyu9700
      @vicentshimiyu9700 5 ปีที่แล้ว

      Mungu akutangulie katika kazi kubwa na nzito uliyonayo Baba wa taifa la sasahivi vijana tuko nawe Magufulification of Tanzania

  • @iddally4073
    @iddally4073 5 ปีที่แล้ว +5

    Huyu ni rais wa vitendo na maamuzi nakupenda rais wangu.

  • @masigomhoja5182
    @masigomhoja5182 5 ปีที่แล้ว +25

    jamani tangu uingie madarakani mheshimiwa sijawahi kujutia kulipa kodi jamani watanzania tulipe kodi munaona? kinachohalibika?

    • @johnhaulepesambili6905
      @johnhaulepesambili6905 5 ปีที่แล้ว +1

      Huyu ndo Rais wa maisha yangu sijutii kuangalia hotuba zake

  • @isaacmsn9
    @isaacmsn9 5 ปีที่แล้ว +7

    That is what they call a twenty first century president of Africa

  • @moimashole992
    @moimashole992 5 ปีที่แล้ว +7

    Siku zote nikisikiliza hotuba yako huwa natokwa na machozi ya furaha mungu azidi kukubarki mkuu wangu dah eeeeeeeh mungu tunashukuru kwa zawadi uliyo tupatia tunaomba umuongoze rais wetu amalize awamu yake salma salimini

  • @kabefiramadhani7610
    @kabefiramadhani7610 5 ปีที่แล้ว +20

    Hakuna kubembeleza mwaka huu
    😀😀😀😀

  • @paulmaduhu6172
    @paulmaduhu6172 5 ปีที่แล้ว +1

    Hongera sana jwtz kw juhudi zenu, mungu awabariki sana

  • @DrFatmaKhanPanAfrikan
    @DrFatmaKhanPanAfrikan 5 ปีที่แล้ว +3

    AlHaamduLILLAH.
    Maa-Shaa-Allah UBaarikiwe Sana Sana Sana Mpendwa Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Magufuli.
    Pole sana na majukumu ya ziada, njama zakukujaribu zitafanywa na hao wachache wasiyo penda maendeleo ya Wananchi na Maendeleo ya Nchi yetu .. Waranguzi hawa. Mwenye-Enzi-Allah-Subhana-Mlezi Atakujaalia kufanikisha yote uliyo dhamiria. Aamiyn. NAKUPENDA SANA

  • @abdallahsaid5497
    @abdallahsaid5497 5 ปีที่แล้ว +4

    Yani mzee baba mwaka 2020 usifanye kampeni good

  • @joasalfred4503
    @joasalfred4503 5 ปีที่แล้ว +3

    🙏🙏🙏🙏🙏🙏 huyu ndo rais wangu,Mungu akuweke daima.Nakuombea uzima tele ili ukaiongoze nchi yangu Tanzania.

  • @fbr5113
    @fbr5113 5 ปีที่แล้ว +3

    Wafute uraia hao wanaoihujumu nchi pamoja na familia zao, ni sumu kali sana hizo. Walipandikizwa zamani, ukiwachunguza kwa kina utagundua wote sio Watanzania wale wanaoiyumbisha nchi. Wamebana kila kona ili uchumi wa nchi uyumbe. Safi sana Rais wetu hakuna lisilowezekana chini ya jua. Umekuwa ukimtaja na kumtukuza sana Mungu hivyo hawezi kukuabisha, atakuwezesha kwa kila jambo. Amina.

  • @saidlwambo1995
    @saidlwambo1995 5 ปีที่แล้ว +1

    Surely Military is final for solving many problems which facing by National

  • @mohameddias5536
    @mohameddias5536 5 ปีที่แล้ว +4

    Baba la baba kwanza anajua wanajeshi wake kwa majina.. God bless you Mr. President

  • @mudathiriali1801
    @mudathiriali1801 5 ปีที่แล้ว +1

    Truth of being a leader of people is like this, Mr president ur Highness truth never lie.

  • @stevenkipara9310
    @stevenkipara9310 5 ปีที่แล้ว +2

    safi sana my presendet Kwaku ona mbali na kuikomboa inchi yetu

  • @charlesmakuri792
    @charlesmakuri792 5 ปีที่แล้ว +7

    Sijui ukiongea huwa wanakuelewa

  • @azizisalimu3828
    @azizisalimu3828 5 ปีที่แล้ว +21

    Huyu mzee ni Fire...Hahahaha

  • @MrLogalaa
    @MrLogalaa 5 ปีที่แล้ว +2

    Safi sana Mheshimiwa ..korosho ni dhahabu ..supermarket korosho kilo moja inkaribia 40k halafu watu kununua kwa 3k bado wanazingua..

  • @majaliwabwitonde7749
    @majaliwabwitonde7749 5 ปีที่แล้ว

    Mungu wa Amani, upendo, mfunike Rais wetu chini ya uvuli wa mbawa zako. Apate nguvu na afya ya kutenda aliyotumwa na watanzania kwa ajili yao. Amina

  • @malangmendy3416
    @malangmendy3416 5 ปีที่แล้ว +1

    I really love this leader in Tanzania so much because her speak his language to his people

  • @samuelmtasha9272
    @samuelmtasha9272 5 ปีที่แล้ว +2

    Mungu akubariki sana Rais wetu mweeeee! Akulinde na mabaya yote katika jina la Yesu, amen! 🙏

  • @sebastiansalamba8236
    @sebastiansalamba8236 5 ปีที่แล้ว +3

    Tunataka kutuma hela ya mafuta naomba namba ya mpesa,tumechoka na mabepari rais wetu uko vizuri eeee uko sawa hakuna bembeleza hapa

  • @josephmlela9757
    @josephmlela9757 5 ปีที่แล้ว +2

    Dah,,,, msimamo mzur Mh. Rais wangu

  • @thegoldendeer4736
    @thegoldendeer4736 5 ปีที่แล้ว +21

    TANGAZENi Na wananchi watakaopenda kujiunga na zoezi hilo ..Naamin tutajitokeza

    • @DrFatmaKhanPanAfrikan
      @DrFatmaKhanPanAfrikan 5 ปีที่แล้ว +1

      Safi sana.

    • @ayoubnyame6287
      @ayoubnyame6287 5 ปีที่แล้ว

      Aisee uyu ngoshaa ni hataree yani kwa uchapaji kazi mi naona bola uchaguzii usikuwepo mpaka mwisho wa maisha yake ili mioyo yetu itulie Safi Sana mkuu.. Mungu akulinde tuone mafanikio ya Taifa letu.KaZiKaZi.💪💪

  • @alphoncesendama9607
    @alphoncesendama9607 5 ปีที่แล้ว +15

    mzeee wa amri hatishiki hata kidogo duuuh maaana ............

  • @amosikabalata6381
    @amosikabalata6381 5 ปีที่แล้ว +4

    Huyu ndo anastahili kuitwa hata konk mia mbili. Nimekuelewa my President.

  • @YamunguYb
    @YamunguYb 5 ปีที่แล้ว +17

    Piga kazi baba hakuna Kuyumba

    • @paschalsamsagala9739
      @paschalsamsagala9739 5 ปีที่แล้ว

      Nipo tayari kushiriki katika zoezi hilo hata kubangua tuu!!!👏👏

    • @yasinmwacha5849
      @yasinmwacha5849 5 ปีที่แล้ว

      Yamungu Athuman ycjc

  • @f.a6043
    @f.a6043 5 ปีที่แล้ว +2

    Much Respect Mr. President. salute!

  • @chidiomari.65
    @chidiomari.65 5 ปีที่แล้ว +9

    👍👍👍👍

  • @ngoshabeatus1545
    @ngoshabeatus1545 5 ปีที่แล้ว

    Hyo jezi ya jeshi nalielewa sana lazma moto ukawake huko nangwanda pga kazi mzee baba tukopamoja asyekuelewa lazma ajibebe safar hii

  • @samuelmwaipopo1302
    @samuelmwaipopo1302 5 ปีที่แล้ว +5

    Mheshimiwa tujenge viwandwa vya kuongeza thamani. tunakuunga Mkono juhudi za kumkomboa mkulima wa Tanzania.

  • @kelvinmwananzum6289
    @kelvinmwananzum6289 5 ปีที่แล้ว +1

    Vizr sana rais wetu n hatua nzr, hakika ww n mkomboz wetu lakn angalia pia na mazao mengne pia kwan so kila sehemu wanalima korosho tunakutegemea..

  • @dr.hamiduibrahim1307
    @dr.hamiduibrahim1307 5 ปีที่แล้ว +14

    Sasa Taifa stars wakishindwa kufuzu AFCON Nadhani Mzee baba unda timu ya jeshi pekee na kazi yao iwe ni mpira tu. Hakuna kumbembeleza mtu.

    • @frankkashner
      @frankkashner 5 ปีที่แล้ว +1

      Wakabangue korosho

    • @ktravel3527
      @ktravel3527 5 ปีที่แล้ว

      Lazima wabangu kwanza korosho kwa meno😂😂😂

    • @khalidkaijage8264
      @khalidkaijage8264 5 ปีที่แล้ว

      Dr. Hamidu Ibrahim hahahaaa mkn mzee

  • @tumainimikina8807
    @tumainimikina8807 5 ปีที่แล้ว

    Asante nakuelewa sana

  • @alphoncemario5998
    @alphoncemario5998 5 ปีที่แล้ว +6

    kuna haja ya ww kuongezewa muda maan uko makin na kazi yko

  • @freddymello3227
    @freddymello3227 5 ปีที่แล้ว +2

    VIVA J.P.M, VIVA JWTZ
    tuko pamoja nanyi katika safari hii ya kumkomboa mtanzania mnyonge.

  • @matingo-bk1248
    @matingo-bk1248 5 ปีที่แล้ว +1

    Good idea

  • @wilsonjohn1919
    @wilsonjohn1919 5 ปีที่แล้ว +3

    Wamezowea kutupunja hao saaaana amir jeshi mkuu hapa kazi tu

  • @jamesngundateresia2600
    @jamesngundateresia2600 5 ปีที่แล้ว +9

    MZEEE BABA JPM MZEE BABA

  • @mgoledaudi7598
    @mgoledaudi7598 5 ปีที่แล้ว +1

    Safi sana Rais wetu Mungu akubariki

  • @ccmtunatekeleza2898
    @ccmtunatekeleza2898 5 ปีที่แล้ว +4

    Hapa kazi tu

  • @ladisthadeo1573
    @ladisthadeo1573 5 ปีที่แล้ว +1

    Nafikiri tulichelewa sana kupata Rais wa namna hii . Tunawapongeza wote waliohakikisha huyu Mzee Magufuli anakuwa Rais wetu .
    Songa mbele Mh.Kamanda mkuu Rais wetu mpendwa .

  • @hakitv4717
    @hakitv4717 2 ปีที่แล้ว

    Wapi like zangu kwa aliyeona wanajeshi wetu wamekaa kwenye viti vyenye rangi moja na wamekaa mkao wa aina moja wote.

  • @modestusndunguru4479
    @modestusndunguru4479 5 ปีที่แล้ว +1

    mzeee Baba gooood

  • @salummasoud5778
    @salummasoud5778 5 ปีที่แล้ว +7

    Safari hii WADOSI watatia Akili, wamezoea kuchezea sana Wakulima wetu. Mwaka Jana mchezo walio ufanya kwenye Mbahazi wakadhani na mwaka huu watafauru kucheza na Korosho. IMEKULA KWAO.

  • @kifarusongeaolg9726
    @kifarusongeaolg9726 5 ปีที่แล้ว +3

    mabeo anaongea kama kamanda sura yakazi kweri 🙌🙌

  • @harunimfaume6280
    @harunimfaume6280 5 ปีที่แล้ว

    daah aisee ww rais wawanannchi uko pamoja na wanannchi ongera sana mungu akupe maisha malefu uzid kuongoza tanzaniaa mungu akutangulie

  • @sadockkabuko8735
    @sadockkabuko8735 5 ปีที่แล้ว +10

    JWTZ# JPM

  • @dorcasdarshin8976
    @dorcasdarshin8976 5 ปีที่แล้ว +12

    Mzee baba endelea naiona Tanzania sasa

  • @michaelmzava7682
    @michaelmzava7682 5 ปีที่แล้ว +1

    Magufuli Mungu azidi kukubariki sana tuko pamoja nawewe Nakupenda Tanzania

  • @fbr5113
    @fbr5113 5 ปีที่แล้ว +1

    Mungu azidi kukupa ulinzi na kujiamini na azidi kukufungulia njia uikomboe Tanzania inayoteswa na Watanzania wanaoshirikiana na mabeberu wa nje. Mungu atakuwezesha utaupita huo mtihani wa wanaoigomea kuinunua korosho wakifikiri Tanzania italala njaa wanasahau kama sikuhizi unapata pesa nyingi kwenye madini. Yaani kudhibiti wizi wa madini pale ulicheza zaidi ya pele. waambie wahame nchi hawatufai hao

  • @vivianaugustino244
    @vivianaugustino244 5 ปีที่แล้ว +1

    Mungu akupe miaka ming,na her dunian,safi,sanaaaaa,,,,

  • @flaviusmwemezi9961
    @flaviusmwemezi9961 5 ปีที่แล้ว +2

    Baba la Baba Dingiilai aina mawiuwiu tumekumanya sana tukimaliga makorosho tufungulie MaGold banking tuwe na utajir wa store kama England japo store zao za wizi

  • @neyozitta1331
    @neyozitta1331 5 ปีที่แล้ว +2

    Wasiokwenda na speed hii, watapata taabu sana

  • @shaabans.marijani9659
    @shaabans.marijani9659 5 ปีที่แล้ว

    The head conk master who direct whatever he want,also he can do in whatever case.I love my president magufuli for his lovely job. Be happy all the time Allah stand for those who do better for the interest of all.

  • @franciscomohamedjumanne1136
    @franciscomohamedjumanne1136 5 ปีที่แล้ว +4

    ambaye hajapongeza ni yule ambaye tu hajakupa kura kwasababu ya upumbavu wa kuremotiwa,

    • @zefamange7281
      @zefamange7281 5 ปีที่แล้ว +1

      Mimi sikumpa kura 2015 lkn 2020 kura yake nimeshika mkonon

    • @franciscomohamedjumanne1136
      @franciscomohamedjumanne1136 5 ปีที่แล้ว

      Zefa Mange ,safi sana hongera kwa kujitambua

    • @zefamange7281
      @zefamange7281 5 ปีที่แล้ว

      Asante Bob, shida yangu ni maendeleo na sio vyama

  • @lussakumussa5385
    @lussakumussa5385 5 ปีที่แล้ว

    Mungu ibariki Tanzania Tuna imani na Rais wetu

  • @hamisabdallah3244
    @hamisabdallah3244 5 ปีที่แล้ว +3

    Tulikuwa tunamtaka Rais mwenye maamuzi magumu kama huyu

  • @nyeguyemachozijacob7443
    @nyeguyemachozijacob7443 5 ปีที่แล้ว

    Asante sana Rais wetu sisi vijana tunakuombea Piga Kaz nasisi tuko na sapoti kubwa tunakupenda sana Raisi wetu mpendwa Mungu akulinde zaidi

    • @nyeguyemachozijacob7443
      @nyeguyemachozijacob7443 5 ปีที่แล้ว

      Tunaomba mkuu wetuu uongeze Magari zaidi ya jeshi ili jeshi letu tukufu lifanye kazi na Mungu awe sambamba na jeshi letu la JWTz AMEN

  • @mohamedih.machirika6793
    @mohamedih.machirika6793 5 ปีที่แล้ว

    mungu ibariki Tanzania na kazi zamikono yao!!!

  • @sullemankova9307
    @sullemankova9307 5 ปีที่แล้ว +2

    Duh ! awali ilikua Oparesheni Sangara _ Sasa ni zamu ya Oparesheni Korosho

  • @nathankihiyo9293
    @nathankihiyo9293 5 ปีที่แล้ว +2

    😂😂😂Jamani Nape Nnauye hajaiona hii!!? Kwakuwa tumeona akikosoa basi japo apongeze na hili ili tusimfikili kivingine.
    Hongera Magufuli

  • @amosmbese8217
    @amosmbese8217 5 ปีที่แล้ว

    Wow kazi kazi

  • @sengahamisi2994
    @sengahamisi2994 5 ปีที่แล้ว +1

    safi sana

  • @shindanopapaya2084
    @shindanopapaya2084 5 ปีที่แล้ว +1

    Safi sana Tanzania kwanza wengine watapata taabu sana Jpm oyeee awamu ya 5 kwa ujumla mmeeleweka watanzania tupo nyuma yenu shikamoooni jeshi letu pendwa JWTZ watanzania tunawapenda sana pigeni kazi

  • @kilulumtunyungu9369
    @kilulumtunyungu9369 5 ปีที่แล้ว +1

    Saaaaafiiii mzee baba

  • @Given-Norman
    @Given-Norman 5 ปีที่แล้ว

    Huyo ndiyo Konki Konki Konki master mkuu, noma sana hakuna kulemba mzee baba.

  • @masigomhoja5182
    @masigomhoja5182 5 ปีที่แล้ว +4

    rais wetu jamani mbona mungu alichelewa kukuleta naamini muda ndiyo huu watanzania tupewe nini?

    • @zefamange7281
      @zefamange7281 5 ปีที่แล้ว

      Kweli hata Mimi naamin alichelewa kuja

  • @raphaelpaschal7892
    @raphaelpaschal7892 5 ปีที่แล้ว +4

    nauko NSSF NA PPF mze tutazame kwajicho la upole huku ulaiyani maisha nimagumu

  • @magrethluisluis204
    @magrethluisluis204 5 ปีที่แล้ว +1

    🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏 safi sanaaaaaa baba kaza mwendo sie tuko nyuma yako

  • @mutalemwagabriel2277
    @mutalemwagabriel2277 5 ปีที่แล้ว +2

    Mwaka elfu mbili na Mia moja watanzania watakuwa wanajivunia huyu mtu rais wetu😂😂😂😂😂

  • @amneymtullah148
    @amneymtullah148 5 ปีที่แล้ว +5

    Ss hizi ndo konk 3 za JPM

  • @zefamange7281
    @zefamange7281 5 ปีที่แล้ว

    Safi sanaaa commando wangu. Wafanya biashara wa Tanzania wamezoea kuchezea serekali

  • @athumanomary1438
    @athumanomary1438 5 ปีที่แล้ว +1

    Ewe mwenyez MUNGU ewe mwenyez MUNGU tunazidi kukuomba enderea kumuongoza raisi wetu kwa kazi kubwa san kwa kuriongoza taifa retu la TANZANIA ewe mwenyez MUNGU mkuu

  • @shekhekhandereizer559
    @shekhekhandereizer559 5 ปีที่แล้ว +2

    korosho ni zetu. wakulima niwetu. najeshi ni letu. magari. vifaru ni vyetu sante Mr President magu tz mbele

  • @sullemankova9307
    @sullemankova9307 5 ปีที่แล้ว +1

    Duh ! awali ilikua Opareshi Sangara ....sasa imefika zamu ya Opareshi Korosho