TUFUNUWE KITABU (SILSILA 27): Maisha ya Habib Ahmad bin Sumeit kwenye Sufis and Scholars of the Sea

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 26 ธ.ค. 2024

ความคิดเห็น • 42

  • @kassimhaji1141
    @kassimhaji1141 2 ปีที่แล้ว +1

    Mashallah hongera Kwa uchambuzi wako Allah akubarik

  • @mwatumsaidi5104
    @mwatumsaidi5104 2 ปีที่แล้ว +6

    Masha Allah yaanii tungejuwa zanzibar ilivokiwa kusingekuwepo hata baa moja Allah awarahamu wote waliotangulia ameen

  • @azizamri1522
    @azizamri1522 2 ปีที่แล้ว +7

    Tumepoteza dini na maadili yetu na tumebeba uchafu wa tabia. Allah Yisturna. Mwenyezi Mungu awape maulamaa wetu Janat Al Firdaus Ya Rab. Nakushukuruni sana kwa kutufunulia kitabu hiki.

  • @Yayouselim
    @Yayouselim 3 หลายเดือนก่อน

    Uchambuzi mzuri sana unajuwa jusa yupo vzuri sana

  • @fafanua
    @fafanua 2 ปีที่แล้ว +6

    Jazaka Allahu Kher! Fascinating historical fact of great significance on Zanzibar- education, faith and health.
    Thank you for insightful summary and thank you Prof. Bang for bringing to light the glory of Islamic scholar in overall, civilization- ethical n moral - and development of Zanzibar.
    Hopefully this historical book will revived interest of knowledge.

  • @Ahmadasshii-raazy8888
    @Ahmadasshii-raazy8888 2 ปีที่แล้ว +1

    ALLAH awaraham masheikh wa masheikh zetu awape pepo ya juu pamoja na BWANA WETU MUHAMMAD صلى الله عليه وآله وسلم na ndugu zetu walitoa darsa hii ALLAH awape swiha na maarifa zaidi waweza kuelimisha jamii yetu kuhusiana na historia yake ya khususan kidini na kisiasa

  • @fathiyasalim3946
    @fathiyasalim3946 2 ปีที่แล้ว +3

    Amina yaarabi. Tumekufahamu Ismail ni kweli umefanya kazi kubwa ya kutuchambulia kitabu hiki. Maskini znz yetu

  • @fatmasaid9765
    @fatmasaid9765 2 ปีที่แล้ว +2

    Mashaallah nimepata kujua mengi kutoka kwenu Allah akupeni afya njema Inshallah

  • @fatmasaid9765
    @fatmasaid9765 2 ปีที่แล้ว +3

    Allah amrehemu amjaalie kaburi yake rowdha min riyadhi jana

  • @khamisabdul4416
    @khamisabdul4416 2 ปีที่แล้ว +1

    mashaallah Allah awajazee kherry

  • @abubakarrahim8482
    @abubakarrahim8482 2 ปีที่แล้ว +3

    Mashaa Allah mungu awaweke mupate kutuelemisha zaidi na leo tumejifunza mengi kuhusiana na maulama walotuletea elimu kwenye mwambao wa pwani na vile vile Kuna kitabu kinachoitwa THE SERVANTS OF THE SHARIA kinazungumzia maulama waliokuwa pande za barawa somalia 🇸🇴 mwaka wa 1893--1900.

    • @yassinmkubwayassin688
      @yassinmkubwayassin688 2 ปีที่แล้ว +2

      hiki kitabu nimekisikia 'THE SERVANTS OF THE SHARIA' lakini kinapatikana wapi ?

    • @fathiyasalim3946
      @fathiyasalim3946 2 ปีที่แล้ว +2

      Nadhani Ismail akisoma atakujuilisha kinapatikanwa wapi.

    • @ismailjussa7644
      @ismailjussa7644 2 ปีที่แล้ว +2

      @@fathiyasalim3946 hichi kitabu kinahusu Barawa, Somalia kwa mujibu wa aliyetoa taarifa. Binafsi ndiyo kwanza nimekisikia hapa.

    • @abubakarrahim8482
      @abubakarrahim8482 2 ปีที่แล้ว +1

      @@ismailjussa7644 ama kwa hakika mheshimiwa Ismail jussa kitabu kinauzwa kwenye mtandao wa Amazon na TH-cam Chanel yao hao wabarawa ni Banadir factor

    • @abubakarrahim8482
      @abubakarrahim8482 2 ปีที่แล้ว +1

      @@ismailjussa7644 ningependa pia utuelemishe na sisi maliwali walowekwa na sultan said Barqash maeneo ya pwani hadi mogadishu nasisi wenzenu tulioko somalia tupate kuelimika kihistoria na kazi walio ifanya

  • @saidkhamis1061
    @saidkhamis1061 2 ปีที่แล้ว

    Mashaallah
    Jazakumlkheir
    Na inasikitisha kwa kweli ...na shukran Sana kwa uchambuzi mzuri Sana kitabu hiki na vinginevyo

  • @guledomary2812
    @guledomary2812 2 ปีที่แล้ว

    Ma Sha Allah kongole zenu sheikh Mohammed Ghasan na sheikh Ismail Jusa Allah awalipe Kwa juhudi kubwa.

  • @khatibal-zinjibari6956
    @khatibal-zinjibari6956 2 ปีที่แล้ว +1

    Shukrani sana Sheikh Mohammed na Mheshimiwa Ismail kutufunulia kitabu cha Profesa Anne K. Bang kwa utafiti wa hali ya juu kukhusu Mufti al-Habib Ahmed al-Sumait (1861-1925) wa Dola ya Zanzibar. Mufti Ahmed al-Sumait alikuwa Mshauri Mahiri wa Mfalme Abdul Hamid Majid (1876-1909) wa Dola ya Othmaniyah. Alimtunukia Mshauri wake nishani ya juu kwa kazi nzuri aliyoifanya. Kadhalika, Mufti Ahmed al-Sumait hakuacha kuitangazia Dola ya Zanzibar kimataifa mpaka kuwa Makao Makuu ya Pan-Islamism na Islamic Modernism. Maelezo zaidi soma:
    Kwa vile Mfalme Abdul Hamid aliwataka Umoja wa Waislam kuondosha Ukoloni nchini mwao, alimteuwa Sheikh Abdul Qadir al-Danna kuwa Balozi wa Dola ya Zanzibar aliyejitambulisha kwa Sayyid Khalifah bin Said bin Sultan (1888-1890), mfuasi wa Pan-Islamism sawa na Sayyid Ali Humoud (1902-1911) aliyekuwa mgeni wa Mfalme Abdul Hamid wa Uturuki. Sayyid Ali Humoud ni Mfalme peke wa Zanzibar aliyesoma Uingereza lakini aliuchukia sana Ukoloni wa Kiingereza mpaka walimvua Usultan na kwenda Ufaransa. Profesa B. G. Martin aliandika:
    "The known anti-British attitudes of (Sultan) Ali bin Humoud his strong sympathies for Pan-Islamism and his friendship with the Sultan of Turkey......And the popularity of of the Pan-Islamic ideas among Zanzibari Muslims was the naming of (Sultan) Abdul Hamid II as Khalifah in the Friday prayers on Zanzibar and mainland (Dar es Salaam, Tanga and Bagamoyo).....Then Zanzibar had a Pan-Islamic newspaper [AL-NAHDAH] with a good number of subscribers [p. 175].
    Chuki ya Makafiri wa Kingereza kwa Zanzibar na Dola ya Othmaniyah ni Uislam. Kabla ya Zanzibar walimpinduwa Mfalme wa Abdul Hamid kwa kumtumia Mustafa Kemal Atartuk (1881-1938) alitangaza Nchi Haina Dini, kupiga marufuku adhan, Hijabu na mila za Kiislam lakini aliruhusu mila za Kimagharibi. Kabla ya hapo, Mufti al-Habib Ahmed bin Sumayt alisambaza harakati za Pan-Islamism na Islamic Modernism kea utaalam ndani ya Dola ya Zanzibar na Tanganyika kama Profesa B. G. Martim alivyoeleza:
    "Ahmed bin Sumayt (1861-1925), the greatest Muslim intellectual of East Africa was an associate of Sultan Abdul Hamid II. Summit introduced the ideas of Pan-Islamism in Zanzibar and mainland Tanganyika from an intellectual viewpoint while Sayyid Ali bin Hamud who had been educated in Britain supported Pan-Islamism and established political association with Ottoman Sultan Abdul Hamid II." [pp. 541].
    Sayyid Ali bin Humud alianzisha Skuli ya Humud (Sasa Skuli ya Kidongo Chekundu) na kumuajiri Sheikh Abdul Bari al-Ajz kutoka Chuo Cha Al-Azhar. Kati ya wanafunzi wake ni Mufti Hassan bin Ameir al-Shirazi, Sheikh Abdullah Saleh al-Farsy na Sheikh Fattawi bin Issa al-Shirazy. Walisoma AL-NAHDA (The Revivalist) lililoanzishwa na Seif Hamoud Faisal (1916-1961) kupigania Uislam, Uzanzibari, kupinga Ubaguzi na Ukoloni wa Kiingereza:
    "We have realized the need for unity and cooperation among the all sections and elements of the Zanzibaris, and we intend to eradicate communal discrimination in the country, a disease that has stood as a stumbling block in the way of progress....We are Zanzibaris in and out and detest any methods used to inculcate racial discrimination.........." [AL-NAHDAH; November 6, 1952].
    Jarida la AL-NAHDAH likisomwa Msikiti Gofu, Msikiti Barza hadi Algeria, Libya, Morocco na Omani. Baada ya Muungano, Zanzibar haitambuliki tena duniani hata Tanganyika mpaka usema Tanzania au Tanzania Visiwani.

    • @khatibal-zinjibari6956
      @khatibal-zinjibari6956 2 ปีที่แล้ว +1

      Samahani sana jina la makala ni:
      RELATIONS BETWEEN THE OTTOMAN EMPIRE AND THE ZANZIBAR SULTANATE (1877-
      1907): DOCUMENTS FROM OTTOMAN ARCHIVES IN ISTANBUL

    • @GumzolaGhassani
      @GumzolaGhassani  2 ปีที่แล้ว

      Shukrani sana sana Sheikh Khatib kwa maalumati haya

  • @fathiyasalim3946
    @fathiyasalim3946 2 ปีที่แล้ว +1

    Alhamdulillah. Kwanza nimpe hongera huyo Mwana mama alofanua utafiti huu. Ambao ni hazina kubwa ya kujua historia hii.
    Pili Allah akupe umri na swiha njema mchambuzi Ismail. Ukweli nimefaidika na mengi kuhusu Uladi hu na uhusiano wao kwa Zinjibar. Ismail Allah akupe afya njema yaani namna unavyoichambua hii story unajihisi kama na mie nilikuwepo enzi hizo. Ukoo wa Bin Sumeit umeanzia mbali sana. Jee huyu Bin Sumeit wa mwisho ameacha kizazi kinachoendelea??

    • @ismailjussa7644
      @ismailjussa7644 2 ปีที่แล้ว +2

      Naam, amewacha kizazi kinachoendelea kupitia mtoto wake wa kike na wajukuu na vitukuu wapo. Hata kwenye kitabu hichi pia wametajwa. Lakini muda haukuruhusu kugusia kila kitu.

  • @asilclub
    @asilclub 2 ปีที่แล้ว

    لا اله الا الله محمد رسول الله

  • @MohamedAli-rl8cl
    @MohamedAli-rl8cl 2 ปีที่แล้ว +1

    Hii ni njia sahihi mno. Nakuomba ufanye ufichuzi na tupate kusikia kupitia channel hii sauti za wanazuoni kama sleman al alawiy na habib omar n.k

    • @khatibal-zinjibari6956
      @khatibal-zinjibari6956 2 ปีที่แล้ว +1

      Ninapendekeza Kitabu Hichi Kisomeswe Vyuo Vikuu Vya Zanzibar Kama Dodoma Watakubali Kwa Kisingizio Kuwa Elimu Ya Juu Ni Ya Muungano.

  • @saidsalim453
    @saidsalim453 2 ปีที่แล้ว +1

    Tunaomba msaada wa kupata hvi vitabu, kiukweli mumetsaidia sana kuingiwa na hamu ya kusoma vitabu, lkn changamoto ni namna ya kupata vitabu haswa vinavyohusu zanzibar yetu..

    • @ismailjussa7644
      @ismailjussa7644 2 ปีที่แล้ว +2

      Shukran sana. Lakini ndugu yangu jukumu hilo sisi hatutoliweza. Sisi tunasaidia kukufikishieni yaliyomo kwenye vitabu tunavyovizungumza hapa na mara nyingi mtu ana nakala yake moja tu. Kazi ya kutafuta kitabu tunaomba ibakie kwenu.

  • @shemsafahmy393
    @shemsafahmy393 2 ปีที่แล้ว +1

    Mwalimu "Mohd" jitahid ukitoa salamu usiongeze hili neno "TAALA" maana halipo kisheria... na badala yake ni *Asalam alaykum warahma tullah wabarakatuh"*

  • @BinAli-m8e
    @BinAli-m8e 15 วันที่ผ่านมา

    Ni Historia yenye kusisimuwa....

  • @111dudi
    @111dudi 2 ปีที่แล้ว +3

    Wabantu ambao walikuja Afrika ya Mashariki na hasa mwambao yika Afrika magharibi,ndio wanaodai kuwa wao ni wazalendo,na ndio wenye nchi.Waarabu na Makabila ambayo asili yake kaskazini kama wairaq, warangi, wahehe na wengineo hawaonekani katika tawala za nchi. Dini iliyofika Afrika mashariki mwanzo kwa zaidi ya miaka elfu ni uislam,lakini leo hii muislam anaonekana ni mgeni katika mfumo wa maisha ya nchi hizi, na imefikia hadi ya "mswahili" kuonekana ni mtu muongo muongo. Nchi za Kiarabu zinahitaji kukaa na kuzungumza jambo la usawa wa uzalendo jatika Afrika mashariki.

    • @khatibal-zinjibari6956
      @khatibal-zinjibari6956 2 ปีที่แล้ว +3

      1] Asili ya ya AFRIKA ni Tunisia.
      2] Neno BANTU halikuwepo kabla ya Wilhelm Bleek (1827-1875), Mkaburu wa Kijarumani.

    • @abubakarrahim8482
      @abubakarrahim8482 2 ปีที่แล้ว

      @@khatibal-zinjibari6956 nikweli kabisa wangreza ndio waliokuja kuleta vurugu Africa na walikuja kubatiza watu na kuwapa majina hata hilo Jina Bantu lilitenegenzwa na wakoloni.

    • @khatibal-zinjibari6956
      @khatibal-zinjibari6956 2 ปีที่แล้ว

      @@abubakarrahim8482 SWADAKTA! Hii ni kwa sababu ya kwamba Dini ya Kiislam ilifika Afrika, khususan Ethiopia, Somali na Zanzibar kabla ya Mtume Muhammad (SAW) kuhamia Madina.
      Waingereza walikuja kuleta vurugu Afrika kwa sababu ya imani yao ya Kikafiri (Sio Ukiristo) dhidi wa Uislam. Kabla ya kuondoka Afrika waliwafundisha akina Julius Nyerere kuendeleza vurugu la Mapinduzi Matukufu (Holy Revolution), kuzambaza Ukafiri na Usekula dhidi ya Uislam.

  • @gojvon116
    @gojvon116 2 ปีที่แล้ว +1

    sheik kidogo umekosea ,kwa kiarabu mmoja ni عالم na wengi ndio wanaitwa علماء usikosee lugha tafadhali

  • @jarsjam8894
    @jarsjam8894 ปีที่แล้ว

    Umefanya makosa kuvaa hiyo kofiya unaingia chooni na mwahala mwengine mchafu

  • @masoudalriyamy6298
    @masoudalriyamy6298 2 ปีที่แล้ว

    Taala inatokea wapi katika salamu nipe dalili ya hiyo taala katika salamu

    • @osmanha6915
      @osmanha6915 2 ปีที่แล้ว +2

      Ebu jaribu kuficha ujinga wako.

    • @fathiyasalim3946
      @fathiyasalim3946 2 ปีที่แล้ว +3

      Changia au uliza masuali ya kuzidi kuwaelewa Masheikh wetu. Sio unauliza upuuzi wa ushindani wa kijinga.

    • @fathiyasalim3946
      @fathiyasalim3946 2 ปีที่แล้ว +3

      Masuali ya kipuuzi kamuulize Borafya mpuuzi wee