KUHARIBIKA MASHINE YA MAABARA HOSPITALI YA KIVUNGE, MHE HEMED SULEIMAN ATOA MAAGIZO MAZITO

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 17 ต.ค. 2024
  • Wilaya ya Kaskazini A: 16/12/2020.
    Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja kufuatilia Makubaliano yaliyopo baina ya Kampuni ya Pyramid iliyoko Dar es salaam na Taasisi ya Hipsi ya Zanzibar juu ya usimamizi wa Mashine Maalum ya uchunguzi wa Maabara iliyowekwa kutoa huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Kaskazini A iliyopo Kivunge.
    Agizo hilo la Mheshimiwa Hemed Suleiman alilolitoa wakati akifanya ziara ya ghafla katika Hospitali hiyo kuangalia uwajibikaji wa Watendaji wa Hospitali hiyo pamoja na huduma za Afya wanazopata Wananchi limekuja kufuatia Mashine hiyo kutofanya kazi kwa tatizo la kuungua kwa Taa wakati bado iko kwenye dhamana ya Kampuni hiyo.
    Amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Hipsi iliyoshirikiana na Kampuni hiyo ya Pyramid kutoa mrejesho wa Taarifa ndani ya masaa Kumi na Mbili na kupelekewa kwa Mkuu wa Mkoa Kaskazini na baadae kuwasilishwa kwake kwa hatua zitazostahiki.
    Mhesimiwa Hemed alisema licha ya kwamba Taifa limekuwa likipokea misaada na baadhi ya michango kutoka kwa Wafadhili na Taasisi za Kitaifa na Kimataifa kwa ajili ya huduma za Jamii lakini Serikali haitaridhia kuona Wananchi wake wanaendelea kukosa huduma za Afya kwa dharau za Mtendaji mmoja.
    Alisema Serikali italazimika kufuatilia mazingira halisi ya huduma za Maabara za Hospitali hiyo na pale itakapohisi kwamba wale waliopewa jukumu la kutoa huduma hizo hawako makini haitasita kuachana nao na badala yake italazimika kununua Mashine nyengine.
    Akizungumzia huduma za Damu salama, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka Watendaji wa Kitengo cha Damu salama kwenye Hospitali hiyo ya Wilaya kutobweteka kwa kusubiri Wananchi kuchangia Huduma hiyo inayohitaji Elimu na uhamasishaji mkubwa.
    Mheshimiwa Hemed alisema Watendaji wa Kitengo hicho wanapaswa kutoa Taarifa kwa Wakuu wa Wilaya na Mkoa kwani wao tayari wana uzoefu mkubwa katika shughuli za uhamasishaji wa uchangiaji damu wanazokuwa wakizitekeleza kila Mwaka.
    Akisalimiana na Wananchi waliofika Hospitali hiyo kupata huduma za Afya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman aliwahakikishia Wananchi hao kwamba Serikali Kuu imejizatiti katika kuona huduma za Afya zinawafikia popote walipo.
    Mheshimiwa Hemed alisema changamoto zinazowapata Wananchi wakati wa huduma hizo ikiwemo baadhi ya ukosefu wa Dawa wanazoandikiwa na Dakatari zitatafutia njia ya kuziondosha kwa Vile Serikali bado inaendelea na Sera zake za kutoa Matibabu Bure.
    Mapema Daktari Dhamana wa Hospitali ya Wilaya ya Kaskazini A iliyopo Kivunge Dr. Tamimu Said Hamad alisema huduma za Afya katika Hospitali hiyo zimeimarika kiasi kwamba hata malalamiko ya baadhi ya Wagonjwa yanaendelea kupungua siku hadi siku.
    Dr. Tamimu alisema zipo changamoto za kubanduka kwa Dari na kupasuka kwa baadhi ya kuta na Vyumba vya Jengo jipya la Hospitali hiyo jambo lililowatia hofu hasa kwenye vyumba wanavyolazwa Wagonjwa wanaopatiwa huduma za Afya.
    Nao kwa upande wao baadhi ya Wananchi waliofika kupata huduma za Afya Hosptalini hapo wamemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar jinsi wanavyoendelea kupata faraja kutokana na huduma wanazopata jambo linalowatia moyo.
    Hata hivyo Wananchi hao waliishauri Serikali kuendelea kufuatilia huduma za Afya zinazotolewa na baadhi ya Hospitali Nchini ambapo wapo baadhi ya Watendaji wanaendelea kuwasumbuwa Wagonjwa.
    Walisema usumbufu huo mara nyingi hutokea 112 na pale mgonjwa anapotakiwa kufanya vipimo kutokana na mradhi yanayomsumbua inakuwa mtihani mkubwa jinsi anavyozunguusha hadi kukata tamaa

ความคิดเห็น •