NDEGE NYINGINE YAANGUKA MAREKANI, WALIOFARIKI HAWAJAFAHAMIKA
ฝัง
- เผยแพร่เมื่อ 7 ก.พ. 2025
- Ndege inaripotiwa kuanguka katika barabara karibu na Jumba la Maduka la Roosevelt mjini Philadelphia, Pennsylvania Ijumaa usiku, na kusababisha magari na nyumba zilizokuwa jirani kushika moto.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 12:30 jioni baada ya ndege iliyokuwa na watu wawili kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Kaskazini Mashariki mwa Philadelphia.
Mashuhuda wameripoti kuona moshi mzito ukifuka kutoka eneo la ajali, na vikosi vya uokoaji vimefika haraka kwenye eneo hilo. Hadi sasa, idadi ya waliofariki na majeruhi haijathibitishwa rasmi. Hata hivyo, vyombo vya habari vya ndani vinaripoti uwepo wa majeruhi kadhaa waliokimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Video inaonyesha ndege hiyo ikianguka kwa kishindo kwa mbali, huku mwanga mkali ukitanda eneo hilo.
Watu wawili wamethibitishwa kuwa ndani ya ndege hiyo. Hali zao bado hazijajulikana kwa wakati huu.
Vikosi vya uokoaji vinapambana na moto uliosambaa kwenye nyumba kadhaa kutokana na ajali hiyo karibu na Mtaa wa 2900 wa Cottman Avenue.
Ajali hii inatokea siku chache tu baada ya ndege ya abiria ya American Airlines kugongana angani na Helikopta ya Jeshi aina ya Black Hawk karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Reagan, na kuua watu 67.
Video na Ammar Masimba.
Mungu anajua Nini sababu tuzidi kujitakasa dalili za ujio wa Bwana Yesu
Tusali sana
Hakika tunapoelekea kubaya ulimwengu watoweka
Dunia inaondoka?