USHUHUDA WA MAKUTANO | MUONGOZO WA KUJIFUNZA BIBLIA | ALHAMISI, NOV 7, 2024

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 25 พ.ย. 2024
  • “Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake” (Yohana 7:37, 38).
    Yohana alirekodi, mara nyingi, Yesu akitoa kauli kwa ujasiri “kumhusu Yeye Mwenyewe, kuhusu ukweli kwamba Yeye alikuwa ni nani na kile alichokuja kufanya.
    Aya zilizonukuliwa hapo juu, kutoka kwenye Yohana 7:37, 38 ni mfano mwingine wa kile Yesu alichosema kumhusu Yeye Mwenyewe na kuhusu kile ambacho angewatendea wote wanaomjia. Haya yalikuwa madai yanayoshangaza pia.
    Wakati Bwana Yesu aliponena kwa Wayahudi waliohudhuria ile Sikukuu ya Vibanda, ni mwitiko gani uliotoka kwa wengi waliokuwa kwenye kusanyiko? (Taz. Yohana 7:37-52).
    Baadhi yao walisema alikuwa Nabii kama Musa alivyotabiri zamani (taz Kum. 18:15-19). Wengine walifikiri Yesu ndiye Kristo. Lakini hii ilileta hoja kwamba Masihi asingetokea Galilaya, kwamba ilipasa awe wa ukoo wa Daudi, na kwamba ilimbidi azaliwe ndani ya Bethlehemu-yote hayo yakiwa kweli juu ya Yesu (linganisha na Mathayo 1-2), ingawa wengi hawakuonekana.
    Hata maofisa wa kumkamata walizuiwa na Yeye na ufasaha wa Maneno yake. Mafarisayo wakawajibu wale watumishi kwa swali lingine: “ ‘Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo?’ ” (Yn. 7:48). Swali hili kutoka kwa Mafarisayo lilimpa Yohana fursa tena kumleta Nikodemo, ambaye baada ya kukutana na Yesu, alikuwa akitafuta kumlinda Yesu kutokana na hila zao. “Je, sheria yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia na kujua anachofanya?” (Yohana 7:51).
    Je, katika wakati wowote, Nikodemo aliwahi kumkubali Yesu kama Masihi? Ingawa tukio hili halithibitishi kwamba alikuwa amemkubali hivyo, kati ya kitendo hiki na kile alichokifanya baada ya Yesu kufa (taz. Yohana 19:39, 40), Biblia inatupatia ushahidi thabiti kwamba kwa kweli Nikodemo hatimaye alimwamini Yeye.
    Na kwa hivyo, jibu la swali lao lilikuwa, ndiyo, kwa kweli, mmoja wa Mafarisayo alimwamini Yeye.
    Soma Yohana 7:49. Viongozi walikuwa wanasema nini kilichoonesha dharau kwa umati uliomfuata Bwana Yesu? Kuna fundisho gani hapa kwa ajili yetu?

ความคิดเห็น • 1