Benjamin Mkapa Foundation na Serikali ya Ireland Waimarisha Sekta ya Afya Chemba Kupitia CHW

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 18 ก.ย. 2024
  • Benjamin Mkapa Foundation (BMF), kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Kamati ya Afya ya Mkoa wa Dodoma, na Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, imeshuhudia zoezi la uchaguzi wa Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii (CHW) katika vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Chemba.
    Zoezi hili linalenga kuhakikisha kila kitongoji kinapata wahudumu wawili wa afya, mmoja mwanamke na mmoja mwanaume, ambao watapatiwa mafunzo ya miezi sita chini ya mpango mpya jumuishi. Mafunzo haya yanalenga kuwawezesha wahudumu hawa kuwa na ujuzi na maarifa ya kutoa elimu na huduma za afya kwa jamii zao.
    Mpango huu unaofadhiliwa na Serikali Pamoja na Wadau wengine wakiwemo Serikali ya Ireland ni sehemu ya juhudi za kuimarisha sekta ya afya nchini, hususan katika ngazi ya jamii.
    Benjamin Mkapa Foundation kupitia progamu zake imekuwa mdau mkubwa wa kuboresha huduma za afya ngazi ya jamii, ikiwa imechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha huduma hizi katika vijiji 114 vilivyopo Wilaya ya Chemba, Mkoa wa Dodoma.

ความคิดเห็น •