TUHUMA NZITO: POLISI WADAIWA KUGAWANA MILIONI 9 za MFANYABIASHARA na MTUHUMIWA MANYARA...

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 2 เม.ย. 2023
  • TUHUMA NZITO: POLISI WADAIWA KUGAWANA MILIONI 9 za MFANYABIASHARA na MTUHUMIWA MANYARA...
    Hii ni taarifa kutokea Magugu Mkoani Manyara ambapo inahusu wizi wa zaidi ya Mil 9. Inadaiwa mnamo January Sita mwaka ishirini na tatu mfanyabiashara wa huduma za fedha HASSAN ALLY NGARE kutoka Ngarenegro Agency aliibiwa zaidi ya tsh Mil 9 na aliyekuwa mfanyakazi wake Peter Stanley.
    Inaelezwa kuwa baada ya tukio hilo NGARE alikwenda kutoa taarifa polisi lakini inadaiwa hakupata ushirikiano wa moja kwa moja kitendo ambacho kilimfanya aingie mtaani mwenyewe na kuwakamata wanaodaiwa kuwa watuhumiwa waliohusika kupanga chama ya kumuibia fedha hizo.
    Katika siku tofauti na maeneo tofauti NGARE aliwakamata watuhumiwa watano akiwemo aliyekuwa mfanyakazi wake Peter Stanley anayedaiwa kuwa mtuhumiwa namba moja na kuwafikisha katika vituo vya polisi vya magugu na Babati vilivyopo mkoani manyara.
    Baadae watuhumiwa hao wote waliachiwa kwa dhamana ikielezwa uchunguzi unaendelea dhidi yao,
    lakini maelezo hayo ni tofauti na Minong'ono iliyopo mitaani inayodai polisi wanachelewesha shauri hilo kwa kudaiwa kuwa waligawana fedha alizoiba mtuhumiwa huyo.
    Wanadai kipindi NGARE alipokwenda kuripoti tukio la kuibiwa polisi walimpigia simu Mtuhumiwa na kumwomba kiasi Cha fedha ili wafute kesi yake.
    Minong'ono hiyo imetufanya tumtafute kamanda wa jeshi la polisi la mkoa wa manyara ACP GEORGE KATABAZI ili ayatoe madukuduku yaliyomo mitaani juu ya sakata hilo.
    ⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: ndstream.net/globalradio/
    ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
    ⚫️ ANDROID:bit.ly/38Lluc8
    ⚫️ iOS:apple.co/38HjiCx
    ⚫️ VISIT COMEDY PLAYLIST: • GLOBAL COMEDY/MOVIES
    ⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI?
    ⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 713 750910), ( +255 783453136)
    ⚫️ Email: globaltvonlinenews@gmail.com OR abbymrisho@gmail.com
    ⚫️ OUR PLAYLISTS:
    ⚫️ MICHEZO na BURUDANI: • Habari zote za michezo...
    ⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: bit.ly/mikasa_ya_kusisimua
    ⚫️ GLOBAL RADIO TV: bit.ly/255globalradio
    ⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: bit.ly/exclusive_interviews
    ⚫️ Subscribe Global TV bit.ly/globaltvonline

ความคิดเห็น • 149

  • @josephmugala1970
    @josephmugala1970 ปีที่แล้ว +7

    Nikawaida ya police wa Tz,
    Bora hata hawajakuua ndugu.

  • @lilianwaflotina1288
    @lilianwaflotina1288 ปีที่แล้ว +1

    aki ya mungu yaani polis badala ya kutoa msaada na wao wanachukua kweli pesa mwanaharamu

  • @fatumasukwaju226
    @fatumasukwaju226 ปีที่แล้ว +3

    Samehe tu.yasikukute mabaya zaidi ya hayo.kikubwa uzima.Duwa la mwenye kudhurumiwa alikwami ,Mlilie Allah kesha ukilia.😭😭😭😭😭🙏

    • @enezermwafrica7443
      @enezermwafrica7443 ปีที่แล้ว

      Asamehe Milioni 9 kwani aliziokota? We unaweza au unarahisisha kwa mwenzako tu🤷 jasho la Mtu achana nalo kabisa we ndugu!

  • @stanleyjohn1361
    @stanleyjohn1361 ปีที่แล้ว +5

    Jeshi la polisi linahusika na matukio mengi ya kitapeli hata kamanda wa polisi mkoa anajitetea tu kwa vyovyote polisi watabebana kwenye hilo tukio

    • @leokamil6284
      @leokamil6284 ปีที่แล้ว +1

      Kabisa ni sawa na ile ya Mtwara sio waaminifu

  • @mwalimuwakowakiswahili8754
    @mwalimuwakowakiswahili8754 ปีที่แล้ว +6

    Ndio maana wengine wanachukua Sheria mkononi na kuua lakini vyanzo ni watu tunaowategemea kutusaidia.

  • @salomewandya7257
    @salomewandya7257 ปีที่แล้ว +3

    Wote wazilipe hizo pesa polisi janjajanja nyingi sana

  • @oscarkasalile3966
    @oscarkasalile3966 ปีที่แล้ว

    Polisi polisi polisi. Mnajizalilisha sana tena sana. Nchi hii ninakila sababu ya kujakugombea urais vitu kama hivi sintataka kuona uchafu kama huu .

  • @shabanikitula645
    @shabanikitula645 ปีที่แล้ว

    Njaa Kali hawa

  • @karimmveyange2558
    @karimmveyange2558 ปีที่แล้ว

    Heee! Hii ndiyo Polisi ta TZ Bwanaaa. Porojo.Tutarudi sheria MIKONONI HIVI PUNDE

  • @SaidiNzoa
    @SaidiNzoa ปีที่แล้ว +1

    Hata aibu yana mungu tusaidie sana

  • @gibsonjosephat6352
    @gibsonjosephat6352 ปีที่แล้ว +3

    Polisi mnakera Sana na mnajaaa mno.

  • @jumapiliissa4835
    @jumapiliissa4835 ปีที่แล้ว

    Hiiniatali sana pole sana

  • @bushirihamisi3819
    @bushirihamisi3819 ปีที่แล้ว +3

    Wafukuzwe kazi haraka hao police hao ndio wanao lichafua jeshi la police

  • @josephusimbanilo9500
    @josephusimbanilo9500 ปีที่แล้ว +3

    Sasa wanachunguza nn wakati Alie chukua hizo pesa kasema wamegawana na police. Kamanda anapo ongea ajue anaongea na watu wenye akili.

  • @mwalimuwakowakiswahili8754
    @mwalimuwakowakiswahili8754 ปีที่แล้ว +2

    Nchi imeoza.

  • @paulinakawishe7210
    @paulinakawishe7210 ปีที่แล้ว

    Mama samia aingilie kati maan hapo hakutendewa haki kabisa

  • @aminakawawa5800
    @aminakawawa5800 ปีที่แล้ว +2

    Arusha kila siku matukio dah 🤲🤲🤲🤲

    • @hellendaniel3809
      @hellendaniel3809 ปีที่แล้ว

      We nae huna listening skills. Umesikia magugu mkoa Manyara bado unasema Arusha. Kiboooo uwe unasikiliza vzr

  • @michaelmwedimage5515
    @michaelmwedimage5515 ปีที่แล้ว +4

    Hakuna upelelezi hapo Daaaaa R.i.p Baba ulisema tutakukumbuka kweli kwenye hili nakukumbuka.

  • @babalao910
    @babalao910 ปีที่แล้ว

    Bora JKT.

  • @christianlutego1288
    @christianlutego1288 ปีที่แล้ว

    Maneno mengii haya a maana yoyote, km kiongozi ilitakiwa kuchukua hatua tu , daah PolisiTz njaa zitawauwa

  • @aloispolenichinga3828
    @aloispolenichinga3828 ปีที่แล้ว

    Wamesahau mambo ya zanzibar kilicho mkuta yule polisi shoga

  • @lailalaila8206
    @lailalaila8206 ปีที่แล้ว

    tz jmn polic sio waminifu kabsaa nawao ni wezi wakubwaa mtu kashakiri sasa mnachunguza nn na mnapeleleza kitu gan sio kama mnarea majambazi kwenye jeshi ra polic mnayafanya mambo makubwa wakanti ni simpori

  • @gaspeldaniel1140
    @gaspeldaniel1140 ปีที่แล้ว +3

    Hili jeshi kama ningekua Raisi ningelifuta kabisa. Na kazi hii ningewapa jkt.

  • @emmanuelsitayo1977
    @emmanuelsitayo1977 ปีที่แล้ว

    Duh!
    Tumefika hapo jamani?
    Kweli urefu wa kamba una matatizo yake.

  • @saidchombo5952
    @saidchombo5952 ปีที่แล้ว

    Ata yeye kala hzo pesa, yaani hapo alieiba ndio wanamlinda alieibiwa imekula kwake, daah! inauma sana

  • @robertphilip385
    @robertphilip385 ปีที่แล้ว

    Wananjaa Kali Hawa police wetu

  • @mwanatz5980
    @mwanatz5980 ปีที่แล้ว +2

    Yani kama watu wa kukamatwa kwanza ni police😅kwakula rushwa japo sio wote lakini wengi wao wanajali matumbo yao tu nasio kulinda Raia na Mali zao 🤸

    • @umsulaiman7468
      @umsulaiman7468 ปีที่แล้ว

      Hapo police anasema alie ibiwa aje ofisin hana haya anataka rushwa upelelezi gani huo kama sinja tu we sema tu alipe rushwa n pesa yake mumpe hivi serikal mko wapi police ndo wakumtetea akapewa pesa yke kesi ya dakika moja tu mkurudishia pesa yke lakin kwa njaa wanamzungusha jaman acheni dhulma hasan ndugu yangu nenda katowe rushwa utarudishiwa pesa yko nusu
      Mtihan jaman police badiliken mnaichafuwa tanzania

  • @jimmymbella997
    @jimmymbella997 ปีที่แล้ว +6

    Polisi Tanzania wana njaa sana mshahara nimdogo sana, wanajikuta wanakula rushwa bila kificho, ila hawa polis hawa, wangetukabidhi wananchi tudili nao tu wenyewe wangenyooka basi tu.😞😞😞

    • @jitabojilala6162
      @jitabojilala6162 ปีที่แล้ว

      Polis shida sio mishahara unaijua mishahara yao???? Ni roho ya kikatili tu

  • @saidasimba9979
    @saidasimba9979 ปีที่แล้ว +3

    Jina la polisi wangebadili tu liitwe kulingana na kazi wanazofanya et mnasemaje wananchi

  • @chiefnumborecords4819
    @chiefnumborecords4819 ปีที่แล้ว +1

    Mbona ata hayo maelezo ya huyo kamanda mwenyewe yanatia shaka sana Tena sana mmmmmh

  • @tztanzania2262
    @tztanzania2262 ปีที่แล้ว

    Tumchangie hassan walau bukubuku aendelee na BIASHARA yake mi nipo tayar walau buku1

  • @ecastephane5347
    @ecastephane5347 ปีที่แล้ว

    Uyo Mzee ao police 👮🏿‍♀️ wata muuwa police wa Tz nawajua sana ili wapoteze ushaidi kwanz anavyo ongea ana onyesha ana anajua kila kitu niko paleeeeeeh wasipo muuwa basi wata mjerui

  • @wilfredaxwesso7394
    @wilfredaxwesso7394 ปีที่แล้ว

    Umsikilize vip kamanda kwani wew hupokei ripoti kutoka kwa watendaji wako na kama haujaletewa ripoti unapopata malalamiko je hujui jukumu lako hadi useme aje ofisini kwako?

  • @dicksonkilupa2258
    @dicksonkilupa2258 ปีที่แล้ว +2

    MAFUA YA WAONEZI YASIPONE HADI WATUBU.

  • @saidchombo5952
    @saidchombo5952 ปีที่แล้ว

    Maswali mazuri sana sema mjibuji ndo chenga

  • @khamisseif9775
    @khamisseif9775 ปีที่แล้ว

    Dooo Nduguyangu Kwa maneno ya Kamanda apo umepigiwa hakuna haki itakayopatikana maana Kamanda anajikanyaga tu

  • @godsonmalisa2544
    @godsonmalisa2544 ปีที่แล้ว

    Ushahidi Gani Tena?mbona Kila kitu Kiko wazi?Hakika Polisi wetu ni hatari sana.RPC unaongea Nini?Kwa Nini usiamze na hao askari wako?Hq

  • @williammbuzimai5744
    @williammbuzimai5744 ปีที่แล้ว

    Mmmmmmh,
    Awe makini wakati wakufika ofisini kwa kamanda,,
    Binafsi nashindwa kumuelewa kabisaaaa.

  • @kiumbenatural-ii5jb
    @kiumbenatural-ii5jb ปีที่แล้ว

    Aibu kubwa sana

  • @kaizambagwa5128
    @kaizambagwa5128 ปีที่แล้ว

    Ndomaana mganza wamechoma kituo kwaajili ya ujinga wenuuu

  • @saidchombo5952
    @saidchombo5952 ปีที่แล้ว

    Polisi anakuwa hana majibu ya msingi duuh! Mtihani sana

  • @allykassim1120
    @allykassim1120 ปีที่แล้ว

    Dah! Kweli huu ni muda wa kupiga Dili hatal

  • @MtuSafi
    @MtuSafi ปีที่แล้ว +1

    Mambo ya Hamza hayo halafu baadae mje kusema gaidi.

  • @babrashabanu7073
    @babrashabanu7073 ปีที่แล้ว +3

    Polisi ni matakataka

  • @joshuamwanilwa4157
    @joshuamwanilwa4157 ปีที่แล้ว +1

    Police wamezoeya kazi

  • @enezermwafrica7443
    @enezermwafrica7443 ปีที่แล้ว

    Yakithibitishwa hayo yanayosemwa mh!..warudishe Fedha, wafukuzwe Kazi na wafungwe!🔗

  • @jitabojilala6162
    @jitabojilala6162 ปีที่แล้ว

    Polis hawa Mungu anawaona ,mtakuja kuwalipa haya yote mnayoyafanya haya

  • @thomassalvatory8303
    @thomassalvatory8303 ปีที่แล้ว

    ushaibiwa unasikia majibu ni kurushiana mzigo sio ufuatiliaje hapo give up and learn to keep off people watu ni wabaya so best soln ni ku keep off people iwe fundisho kwako usimsaidie mtu yeyote

  • @marcynhumbi3534
    @marcynhumbi3534 ปีที่แล้ว +1

    Yaani police ni tatizo sana yaani wakae tu nawajitafakari,na chanzo cha matatizo ukichunguza ni police.Police wanatamaa police wana roho mbaya yaani police sio sehemu salama.Kwanza mi nawachukia police mno

  • @pendo8082
    @pendo8082 ปีที่แล้ว +1

    Kweli maisha ni magumu duh

  • @mangulimanguli3974
    @mangulimanguli3974 ปีที่แล้ว

    Kesi ya nyani umpelekee ngedele, Police wa Tanzania lao moja wanakula na ao wakubwa wao

  • @mapangaramadhani9056
    @mapangaramadhani9056 ปีที่แล้ว

    Mi sina ham na police wa TZ Et ukitaka haki nenda police hicho kitu hakipo bado dhulma ni kubwa, mama anapashwa kuliangalia hili. Kesi ya mwizi na mtuhumiwa yupo toka mwezi wa kwanza haijafikishwa mahakamaniiiii. alafu anakuja kiongozi wa police wa juu anatetea ujinga.

  • @sidebadru2493
    @sidebadru2493 ปีที่แล้ว

    Hii ndio Mana raia wanachukua sheria mkono askar wanabebana sana

  • @walidmgonja3644
    @walidmgonja3644 ปีที่แล้ว

    Hata maelezo anayotoa kamanda wa polisi yanatia shaka juu ya uadilifu wake,huenda naye ni sehemu ya tatizo.

  • @petermboje5839
    @petermboje5839 ปีที่แล้ว

    Acha siasa kamanda hutoshi kuwa kamanda wa police mkoa ewe hewa kabisa

  • @noelbryson7840
    @noelbryson7840 ปีที่แล้ว +1

    Uniibie pesa zangu alafu uniambie umegawana na polisi halafu nikuache salama? … Hii mechi ingeishia mtaani tena mapema sana..

  • @iddykwangaya2794
    @iddykwangaya2794 ปีที่แล้ว

    Sasa huyo afisa mwenyewe mbona anamung'unya maneno tu..nyie mmemuelelewa anachokiongea jamani?

  • @magallahramadhani8762
    @magallahramadhani8762 ปีที่แล้ว +2

    Hii ndiyo police Tanzania

    • @leokamil6284
      @leokamil6284 ปีที่แล้ว

      Ni kweli ndio zao hizo

  • @ezekielloylepayon5042
    @ezekielloylepayon5042 ปีที่แล้ว

    Huyu mlalamikaji ana Mungu sana maana mpka sasa hamza wa pili angetokea huku manyara

  • @euphrasiantawatawa1510
    @euphrasiantawatawa1510 ปีที่แล้ว

    Baadhi ya police ni wapuuzi sana,na ndiyo chanzo cha kuishi maisha ya wasiwasi na hofu nyingi kwa mtuhumiwa,hata kama police wamemuhakikishia ulinzi kwake kama ana akili timamu hana amani na hatakuwa na amani maishani mwake,atafute pesa amlipe aliyemibia direct aishi kwa amani mtaani,aachane na police,njaa na kujiendekeza zimewashusha sana thamani ya kazi ya police

  • @DonMooSTUDIO_Express
    @DonMooSTUDIO_Express ปีที่แล้ว +1

    Kila nikiandika comment nafuta... ngoja nisiandike zaidi ya hapa

  • @yohanakamota2587
    @yohanakamota2587 ปีที่แล้ว

    Hayo maelezo ya kamanda hayana matumain kwa mlalamikaji mi ushauri hata huyo kamanda afanyiwe uchunguzi haiwezekani kesi inataka kuwachoma hata wao alafu mtuhumiwa Yuko huru kwa zamana nin hiyo au wanalegeza wakali ya mlalamikaji

  • @fredytarimo9107
    @fredytarimo9107 ปีที่แล้ว

    Duuuu IGP ingilia kati hili huyu police hafai kukalia hicho kiti. Maelezo yake inaonyesha huu mchezo anaujua mwanzo mwisho.

  • @yusuphkassimu227
    @yusuphkassimu227 ปีที่แล้ว +1

    Polisi Tanzania 🏃🏃🏃🏃🏃🏃

  • @thomassalvatory8303
    @thomassalvatory8303 ปีที่แล้ว

    ukifungua biashara ajiri ndugu yako ili akikuibia ni kama msaada kwa ukooo hawa watu baki usiwasaidie hata anadanja hapo muangalie muambie ni maamuzi yako hili jambo limenisikitisha sanaaa unatafuta pesa kwa shida mtu ambaye hajui misingi ya hizo pesa anakuibia soln ni usimsaidie mtu yeyote ndugu yako tuu

  • @alphoncekahayi8719
    @alphoncekahayi8719 ปีที่แล้ว +1

    Hapa hakuna jeshi ni genge tu la wahuni wengi hawana weledi wanafanya kazi kama vibaka.

  • @martinemaganga5253
    @martinemaganga5253 ปีที่แล้ว +2

    Duuu, polisi bwana 🤣🤣🤣🤣

    • @salomewandya7257
      @salomewandya7257 ปีที่แล้ว

      😄😄😄😄😄😄

    • @leokamil6284
      @leokamil6284 ปีที่แล้ว

      Kwa kuruka ndio wenyewe ile ya Mtwara tu imefukiwa hawa sio waaminifu

  • @happynelson1180
    @happynelson1180 ปีที่แล้ว

    Polisi kuwadhurumu wananchi yanatokea bongo tu huku majuu mambo kama hayo hayakei bongo ingeanzisha sheria ya kila mwananchi afungue BankID ili watu waitumie kulipa kila kitu ili hata ukiibiwa kwenye mitandao itaonyesha pesa imeenda kwa nani na utarudishiwa pesa zako sababu utakuwa na ushahidi watu wengi huku majuu tunatumia BankID imesaidia sana kupunguza wizi kuliko kutembea na pesa

  • @GabuNyambali-em5eg
    @GabuNyambali-em5eg ปีที่แล้ว

    Polisi wa ichi hii ni zaidi ya majambazi

  • @rosetreffert6727
    @rosetreffert6727 ปีที่แล้ว

    Jeshi mnatia aibu sana kamanda unajikanyaga hata huna majibu sahihi, utapeli

  • @Chemba67
    @Chemba67 ปีที่แล้ว

    HIVI KWA MATUKIO HAYA NA MENGINEYO IMANI KWA JESHI LA POLISI ITATOKA WAPI??? WASHENZI SANA HAWA NDOROBO

  • @mashramadhani1989
    @mashramadhani1989 ปีที่แล้ว

    Police hapo ndipo mnakuwaga mnafeli rushwaaaaaa

  • @jastinpiniel4447
    @jastinpiniel4447 ปีที่แล้ว

    polisi ni shida sana tena sana upumbavu tu

  • @ramadhaniamri3465
    @ramadhaniamri3465 ปีที่แล้ว

    RIP Baba Magufuli Tutakukumbuka.

  • @bushirihamisi3819
    @bushirihamisi3819 ปีที่แล้ว

    Uchunguzi wa nn kannda wakati wezi wapi na wanao lichafua jeshi la police wapo

  • @saidhassan7779
    @saidhassan7779 ปีที่แล้ว

    BORA KUSIWE NA KAZI YA POLISI LIWEPO JWTZ

  • @abdalahfundi7936
    @abdalahfundi7936 ปีที่แล้ว

    Wanapeleleza nini wakati mtuhumiwa kakiri jamani jamani polisi pua kabisa🤣🤣🤣

  • @sudymgeni701
    @sudymgeni701 ปีที่แล้ว

    Hapana kamanda inaelekea ujui kinacho endelea.fatilia kama mtuu miwa mmeshindwa mkamata.inakuaje.wacha majibu mepesi.msiwape watu hasira

  • @jumaomari3842
    @jumaomari3842 ปีที่แล้ว

    Kwaiyo.nyinyi.mnatafuata.upelelezi.gani.wakati.muizi.mnamjua.mimi.binafsi.nawachukia.sana.kwa.tabia.zenu.ndio.

  • @fidelludemwa7223
    @fidelludemwa7223 ปีที่แล้ว

    Hapa Kuna shida

  • @daslamonline4665
    @daslamonline4665 ปีที่แล้ว

    Aende kwa mkuu wa wilaya

  • @bettykasase1267
    @bettykasase1267 ปีที่แล้ว

    Hakuna msaada

  • @gabrielymatembo8770
    @gabrielymatembo8770 ปีที่แล้ว

    Mbona ulisema alikuwa hapokei simu sasa hao polisi waliongea naye vipi

  • @amiribakari2528
    @amiribakari2528 ปีที่แล้ว

    Sasa unafikiri angesema nn zaidi ya alichokisema..kwamba jeshi la police linaendelea na uchunguzi..sasa kazi kwako wewe uliebiwa.ndo maana watu wengine wanamalizana huku huku ukipeleka police imekula kwako..

  • @JumanneNguja-hw3kd
    @JumanneNguja-hw3kd ปีที่แล้ว

    We

  • @denispaulo1295
    @denispaulo1295 ปีที่แล้ว

    Jama ajitaidi afike kwa IGP

  • @gaspercharles2244
    @gaspercharles2244 ปีที่แล้ว

    Hayo ndio yanayofanyika Tanzania yetu polisi wanafanya hivyo hata mm nilishafanyiwa hivyo.

  • @juliuskitaluka1206
    @juliuskitaluka1206 ปีที่แล้ว

    Police amchunguze police mazingaombwe

  • @mdemualphonce1559
    @mdemualphonce1559 ปีที่แล้ว

    Hawa ni shida

  • @petermboje5839
    @petermboje5839 ปีที่แล้ว

    Kamata askari wote hao

  • @aishachambo8663
    @aishachambo8663 ปีที่แล้ว

    Polisi wamezoe wizi Mtwara wamemuibia mtu na kumtoa uhai adi leo hakuna kilicho fanyika

  • @mosesbarnabas3379
    @mosesbarnabas3379 ปีที่แล้ว

    Kesi ya nyani hawezi kuhukumu ngedere

  • @kabwelasutiviraka4765
    @kabwelasutiviraka4765 ปีที่แล้ว

    Hii nchi Tanzania ni nchi ya mavi kunuka na hao wanyama police ni washenzi na wezi tu hawana hata maana , halafu mkuu wa nchi yupo huyo bibi tozo busy na vikao na kuomba omba waziri wa mambo ya ndani yuko kimya , haikuwa ajabu wananchi geita kuchoma kituo cha police maana wamechoka na hao wahuni na wezi police, na lazima kuwe na chombo maalumu cha ku deal na uhalifu wa police

  • @benjaminhabwendelo2178
    @benjaminhabwendelo2178 ปีที่แล้ว

    Hakuna lolote upelelezi wa nini mwizi amekamatwa na fedha amekili kweli fedha ameiba na kagawana na polisi mizunguko ya nini?

  • @stellajorojick9663
    @stellajorojick9663 ปีที่แล้ว

    Kwa nini alomdamini hajalipa?

  • @kilogreekachananawatuwasio4054
    @kilogreekachananawatuwasio4054 ปีที่แล้ว

    Huyu mkuu hanayohongea mwizi hinajulisha hii pesa kala himepita mikononi mwake jambazi mkubwa 😂

  • @hapaupdates9277
    @hapaupdates9277 ปีที่แล้ว

    MAJAMBAZI HAYO

  • @ibrahimgwasma1223
    @ibrahimgwasma1223 ปีที่แล้ว

    Hilo ni kosa la madai cyo jinai

  • @mdemualphonce1559
    @mdemualphonce1559 ปีที่แล้ว

    Upelelezi huo hauna weledi jamani hauzidi siku tatu hapo vipi?

  • @nderingomunis5398
    @nderingomunis5398 ปีที่แล้ว

    Upelelez gan bhn mda unaenda iyo hela ndo maisha ya uyo mtu