AHMED ALLY : AWAPONGEZA WATANI WAO YANGA KWA KUTWAA UBINGWA WA NBC TANZANIA BARA

แชร์
ฝัง
  • เผยแพร่เมื่อ 16 พ.ค. 2024
  • Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amewapongeza wapinzani wao, Yanga SC kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa mara ya 30 sasa huku wakiwa wamechukua ubingwa huo mara tatu mfululizo.
    Ahmed amesema hayo baada ya Yanga kutwaa Ubingwa huo kwa kumfunga Mtibwa Sugar na kufikisha alama 71 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
    “Kwenye maisha unapopata kitu kibaya kinakuongezea nguvu ya kutafuta, sare ambayo tumeipata dhidi ya Kagera Sugar imetuongezea nguvu ya kupambana kupata nafasi ya pili. Vita yetu rasmi ni kuhakikisha tunaipata nafasi ya pili ili twende tukashiriki ligi ya mabingwa msimu ujao.
    “Tunawapongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa, haikuwa safari nyepesi, mbio zilikuwa kubwa lakini lazima mtu mmoja awe bingwa. Hatuna budi kumpongeza yanga kwa kutwaa Ubingwa.
    “Sisi kama Simba tuna mengi ya kujilaumu, tuna mengi ya kujifunza, kujikosoa na kujirekebisha. Tunao wajibu wa kukaa chini na kufikiria tunakosea wapi msimu wa tatu sasa bila taji.
    “Hii imemalizika, sasa tunapigania nafasi ya thamani ya ushindi wa pili. Kwa sasa
    Bbbbbbbbbbb
    Ahmed Ally amesema kuwa timu yao wanapaswa kupambana kufa na kupona kuhakikisha wanamaliza katika nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya NBC ili msimu ujao waweze kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
    Ahmed amesema hayo mara baada ya kutua Dar wakitokea Bukoba ambako Simba ilikuwa na mchezo wa Ligi dhidi ya Kagera Sugar, mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 katika Dimba la Kaitaba.
    “Sare dhidi ya Kagera Sugar
    “Tunatembea juu ya Kamba nyembamba ambapo chini yake kuna bwawa la mamba, ukiteleza kidogo tu chali umeliwa na mamba, unakosa nafasi ya pili unakwenda kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika.
    “Kombe la Shirikisho sio baya, ni michuano mikubwa ya tatu barani Afrika, ina thamani kubwa mno, achana na maneno ya wapuuzi kwamba ni kombe la looser, kwa hiyo sio mbaya kwenda kushiriki lakini kwa ukubwa wetu sisi Simba SC, tunapaswa kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
    “Kwa hiyo mechi chache zilizosalia, tunapaswa kuwa makini wa asilimia 100 ili tupate ushindi.
    Endapo Azam na Simba kila mmoja atashinda michezo yake yote, basi watalingana alama na mshindi wa pili ataamriwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
    Katika hatua nyingine, Bingwa (mshindi nafasi ya kwanza) ambaye ni Yanga ana nafasi ya moja kwa moja ya kushiriki Klabu Bingwa Afrika pamoja na mshindi wa nafasi ya pili. #simba #biashara #simbanayanga #trending #dar #yanga#trending#msimbazi

ความคิดเห็น •